Haya majukumu ya Makamu ya Rais anaagizwa na Rais?

Zipuwawa

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
3,051
653
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya
Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku
hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini
au yuko nje ya nchi.

Je haya majukumu ya Makamu wa Rais Yeye kuwa wa Kutembea na mikasi na Kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo na hata mashule , hospital, na huduma za maji hata kama hazijakamilika. Makamu wa rais Toka ateuliwe yeye amekuwa akitembea tu kufungua miradi mbalimbali hata kama haijakamilika Je hizi ndizo kazi alizo tumwa au kuagizwa na Rais?
Je viongozi wetu wanafuata katiba? Makamu wa Rais tumeshuhudia toka aanze kazi amekuwa akitembea na mikasi akiwa na Msururu wa Magari kwa kwenda kufungua miradi ambayo ingeweza hata kufunguliwa na wakuu wa mikoa au wilaya. Nauliza huu si ufisadi mwingine kwa gharama kubwa za misafara ya Ndani isiyokuwa na Tija?
Je wamekubaliana na rais kuwa makamu awe wa kuzunguka nchi nzima na Rais kuzunguka Dunia nzima? Tuangalie leo hii hali ya nchi migogoro ni mingi lakini Rais na Makamu wake wapo kwenye safari zisizokuwa na tija.

Ni bora tuiangalie katiba yetu inayowabeba watawala kwa kuendelea kuwaburuza tumeona jana Spika wa Bunge akizungumzia Katiba je haya ya Viongozi wa juu hawaijui katiba? au katiba ni kwaajili ya kuwabana watawaliwa tu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom