Haya majina anayomwita mama yake mnayaonaje?

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
423
451
Wakuu habari za muda huu, hongereni kwa mapambano dhidi mdudu huyu mchafu Corona.

Wacha twende moja kwa moja kwenye mada yetu, dada yangu ana watoto wake wa kiume mwenye miaka 15 (nataja umri ili huu ushauri uone kama umri ndio chanzo au la)

Sababu ya kuleta mada hii hapa ni hii, huyu mtoto amekuwa na tabia ya kupendelea kumwita mama yake Mama Amani (yeye jina lake ndio Amani) au wakati mwingine hata cheo chake cha kazini (Chief Accountant wa kampuni ******) au dadake Display Name au vyovyote tu atakavyojisikia aiki hiyo

Mama yake amekuwa na wasiwasi flani labda mtoto hampendi au heshima imepungua kwenye jinsi mtoto wake amekuwa akimwita, mimi nimemwambia ni kawaida maana nimeshuhudia watu wengi wakiwapa mama zao/baba zao majina flani hivi, dada ameonekana kama kaelewa ila ka wasiwasi nakaona kwa mbaali bado kapo.

Je, hili ni jambo la kuwa na wasiwasi nalo au tumuache dogo aendelee na maisha?
 
Sio mbaya ni utani mtoto yupo free na mama yake.

Mama yangu ananiita Dada, watu nyumbani wanamuita mama lucky, nikimpigia simu namuita mama lucky ambalo ni jina langu. Saa nyingine nikimpigia namuita Majina ya wadogo zangu, mama Lucy, au mama Levi, au mama lady, hawa wote ni wadogo zangu. Na anapenda sana
 
Afadhali kwa kweli. Nitamfikishia taarifa hizi 🙏🏿
 
Ni kawaida sana hiyo mkuu

Kuna jamaa yangu huwa wanaitana jina la master na baba yake mzazi

Hakuna kitu kizuri kama kumfanya baba/mama/mpezi/mkeo/mmeo rafiki yako

Mfano:Mimi naweza kumuita mama yangu jina lake la asili/kiasili anaitifa vizuri tu na naweza kumutania kirafiki vizuri tu.

Mama huwa anamiss uwepo wangu sana pindi niwapo mbali na upeo wa macho yake

Mwambie Mama kuitwa hayo majina asiwaze wala kukasilika cha muno heshima iwepo tu.
 
Sio mbaya ni utani mtoto yupo free na mama yake.

Mama yangu ananiita Dada, watu nyumbani wanamuita mama lucky, nikimpigia simu namuita mama lucky ambalo ni jina langu. Saa nyingine nikimpigia namuita Majina ya wadogo zangu, mama Lucy, au mama Levi, au mama lady, hawa wote ni wadogo zangu. Na anapenda sana
Mkuu hao wadogo zako wameolewa
 
Back
Top Bottom