Haya Kwa Wale wanaoamini Mambo ya nyota angalia Mwaka 2011 je utakuwa na Bahati kwako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya Kwa Wale wanaoamini Mambo ya nyota angalia Mwaka 2011 je utakuwa na Bahati kwako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 31, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  2011 Horoscopes


  Ready to see if your Sun sign will shine in 2011?

  From your career path to your amorous adventures to just life in general, Astrology.com takes a good, long look at what the stars have in store for you this year! Click on your Sun sign below to get started with your 2011 Yearly Overview, and then check out the stellar insights into Your Career in 2011 and Your Romantic Life in 2011. Here’s to a cosmic time in the coming year!


   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe Aries March 21 Mpaka – April 19 Tabia zao ni hizi hapa

  NYOTA YA PUNDA AU KONDOO (ARIES)

  • Hii ni nyota ya kwanza katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21st March na tarehe 19 April ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Mars (Mariikh)
  • Siku yao ya bahati ni Jumanne
  • Namba yao ya bahati ni 9
  • Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu.
  • Asili yao ni Moto.
  NYOTA YA PUNDA AU KONDOO KATIKA MAPENZI NA MAHABA

  Kwa vile wao ni wenye nyota ya kwanza mara nyingi wenye nyota hii wanapenda kuwa mbele. Wanakuwa wakarimu na wenye pendo kwa wapenzi wao.
  Ni watu wenye kupenda kushirikiana na watu wengine, wanapenda mikusanyiko ya jamii

  na wacheshi. Ni watu wazuri kuwa nao karibu na mara nyingi wao wanakuwa ndio maisha na roho ya kundi wanalojihusisha nalo. Hivyo inatokana na tabia zao za asili za uchangamfu. Hata hivyo wakiudhiwa huwa ni viumbe wenye hasira kali.
  Wenye nyota hii ni wepesi sana kuvunjika moyo na hii inatokea wakati wapenzi wao wanapowaangusha au kuwadharau katika mapenzi ambayo wao wanayachukulia kwa uzito mkubwa.

  Pamoja na uchangamfu walio nao wenye nyota ya Punda wana moyo dhaifu usiovumilia matatizo na wanaweza kudhuriwa kirahisi katika mapenzi.
  Wanaingia katika mapenzi na kupenda kirahisi. Mara nyingi wanawafanya wapenzi wao

  ndio nguzo au kiegemezo na hapo ndipo matatizo yanapoanza.
  Wasipopata njia ya kutatua matatizo ya kimapenzi huwa wanachanganyikiwa na wanafadhaika sana hasa wanapogundua kwamba wapenzi wao ni binadamu kinyume na walivyofikira wao.

  Kwao wazo la kuwa waaminifu kwa mpenzi mmoja milele linapewa kipaumbele katika mambo ya mahaba, lakini wakiona mambo yanaenda kombo basi ni mwepesi sana kuondoka kwenda kutatufa mpenzi mpya sehemu nyingineyo.

  Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kuwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia

  katika mapenzi bila kufikiri wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.

  NYOTA YA PUNDA KATIKA FEDHA


  Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia nguvu au kulazimisha na siyo waoga. Mipango yao ya kifedha wanayoipanga inakuwa na ubora wa hali ya juu inayopendeza na inayowavutia watu wengine. Hii inatokana na uwezo wao, shauku na vipaji vya kiakili kuhusiana na masuala ya fedha.

  Hakuna sehemu yeyote ambayo mwenye nyota ya Punda atafanya shughuli yeyote bila watu kupendezwa na mipango yao. muda wote wako tayari kuchukua majukumu bila kujali chochote na mwisho wake mafaniko yanakuwa makubwa. Suala la kujiliza ni kuwa je
  wanaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu?

  Jibu ni hapana watu wa Punda wanatambulika kwa tabia yao ya ufuatiliaji wa mambo, bila kuchoka lakini tabia yao ya kiburi katika mambo madogo madogo ya kibiashara na kikazi wakati mwingine huhatarisha mradi au kazi zao zote.
  Wanapenda kutumia fedha kiholela bila kupata uhakika kwamba zitarudi au zipo. Hulka yao ya kuwa mbele na kupenda kuishi kiuaminifu huwafanya wakose kinga kwa wajanja wanao penda kuwatapeli.

  Kitu kimoja ni kwamba Mungu amewapa uwezo wa kufanya kazi vizuri wanapokuwa wao viongozi au wasimamizi. Wanakuwa na nia na moyo wa kufanya mambo mapya, lakini ajabu ni kwamba hawana subira wala mbinu za utawala hasa katika masuala ya fedha.
  Papara zao za kujua mambo zaidi mara nyingi husababisha utatanishi kwa watu wote wanaowazunguka na wanao wakilisha.

  Kimaisha wenye nyota ya Punda wanapenda sifa na kuonyesha matunda ya kazi zao au uwezo wao kifedha kwa kununua magari mazuri, nguo zenye thamani kubwa na vito vya thamani ili waonekane pamoja na ukarimu wao wakati mwingine hubadilika na kuwa wabinafsi na wachoyo.

  Kwa ujumla wenye nyota hii ni watu wenye ari na uwezo wa kuanzisha mambo na wanapenda kupata maendeleo ya kimaisha na kuwa na miradi mipya. “NATAKA” ndio neno lao kubwa. Wanahitaji sana fedha, uwezo na uvutio ni wakati mchache sana huangalia maslahi ya watu wengine. Huwa wanakabiliwa na tatizo la kuchagua fedha au mamlaka, hata hivyo mapenzi yao ya kuwa na uwezo huwa yanashinda.
  {mospagebreak}

  NYOTA YA PUNDA (AFYA ZAO)


  Wenye nyota hii ni watu wenye nguvu na afya nzuri. Wakati wote wao wanakuwa hawana subira ya kungoja kufanya shughuli zinazowahusu. Ni watu ambao hawapendi kabisa kuugua au kupata maradhi. Mara nyingi wanakuwa na uwezo wa ajabu wa kupona maradhi yanyaosumbua.

  Kwa vile nyota hii ya Punda inatwala kichwa maradhi yao mengi yanahusiana na kuumwa kichwa na homa za mara kwa mara ambazo hupotea kama zilivyokuja.
  Tatizo lao kubwa la kiafya ni la “Adrenalini” (Hii ni Homoni inayotoka ndani ya mwili wakati mtu anaposhtushwa au kukasirika, ambayo inafanya moyo upige haraka na kuutayarisha mwili kupambana na khatari). Watu hawa wanafanya kazi bila kuchoka na inatakiwa nguvu zao zielekezwe sehemu inayohusika, ikitokea vinginevyo huwa wanakosa raha na kuwa na wasiwasi.

  Wasiwasi huo unasababisha “Adrenalini” kumwagika kwa wingi wanakuwa wepesi kuudhika na kukasirishwa na kuwa na Hamaki au ghadhabu za haraka ambazo huwaletea matatizo ya mzunguko wa damu katika Ubongo na macho.

  Watu wa Punda wanahitaji kufahamu kwamba wao hawana kinga hivyo mapumziko ni muhimu kwao. Wanatakiwa wapendelee kutembea kwa miguu au wajihusishe na michezo ili kuondoa mzigo wa uchokozi, hakami na hasira walionao.
  Utaratibu maalum wa kula chakula vile vile ni muhimu, na wenye nyota hii wanashauriwa

  kukiepusha na kahawa na sukari nyeupe ambao inaongeza mfadhaiko katka mfumo wa neva na tezi za “Adrenalini”. Ni wachache sana wenye nyota hii ambao wana matatizo ya uzito kwa sababu wanajishughuoisha sana na shughuli mbalimabli.

  Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokata tamaa huwa wanaathirika, na tbaia yao ya haraka haraka inawafanya wawe katika vita na miili yao wenyewe. Matokeo yake ni kuathirika kiafya. Wanatakiwa wajifunze tabia ya nyota ya Mizani ya ushirikiano. Tabia hii pamoja na kwamba itawapunguza kasi zoa katika utendaji lakini itawasaidia kudhibiti matatizo yao ya kiafya.

  NYOTA YA PUNDA (MAISHA YAO)


  Punda wanapenda sana kujihusisha na masuala ya kuwafanya waishi vizuri kama binaadamu wengine. Wanapenda sana vitu vyenye msisimko vya pekee na utaona hivyo katika nyumba zao.

  Kuweka makazi ya kudumu kwa mtu wa Punda ni moja ya mitihani mikubwa ambayo ana lazima atekeleze lakini kwa watu wengine jambo hili wanalichukulia kama mojawapo ya mambo mengi ya kimaisha ambayo wakipata fedha anataka watekeleze.

  Moja ya hulka za Punda ni kuthibiti namna nyumba zao zinavyoendeshwa. Hivyo inamaanisha kwamba wanahitaji kupata mwenzi mwaminifu ambaye atatekeleza yote atakayoagizwa kuyafanya hapo nyumbani. Vinginevyo tabia zao za kutokupumzika na tamaa ya kufanya mambo mapya itawafanya wapoteze hamu ya maisha yao ya nyumbani.

  Wanapokuwa tayari wameweka mizizi yao wanakuwa waaminifu kwa familia zao. Hata hivyo kuna hatari kwamba wasipoweza kupata wanachokitaka hapo nyumbani wanaweza kusimama na kuondoka.

  Hawawezi kuficha hisia zao kwa yeyote wanayemualika katika nyumba zao ukikosa atakuambia na hawategemei hata walioalikwa nao kuficha hisia zao vile vile.
  Kutokana na shauku na hamu kubwa ya kuthitisha maisha yao, ni vizuri Punda wakawa waangalifu, wasiwe wajeuri au wakandamizaji katika nyumba zao.
  Ni watu wanaozipenda familia zao na mara nyingi wanatumia nyumba zao kama sehemu ya kufanyia kazi badala ya mapumziko.
  {mospagebreak}

  NYOTA YA PUNDA (LIKIZO NA SAFARI)


  Nyota ya Punda ni nyota yenye asili ya moto, maana yake ni watu wenye ari na nguvu zisizo na mipaka, na mara nyingi wanatatufa vitu vinavyowafurahisha. Wanapenda sana kusafiri aidha katika biashara au kwa kujifurahisha.

  Wenye nyota hii wana tabia ya kujenga uhusiano mkubwa katika tabia fulani. Hii inapotokea wanapenda kutumia muda wao mwingi katika mazingira hayo ili wayaelewe vizuri. Wanajua kabisa sehemu au mji ambao watajisikia wako nyumbani.

  Muda mwingi huwa wanapenda mazingira mapya na hii inawafanya kupata uzoefu mkubwa mara nyingi wanakuwa ni waalimu wazuri sana. Ukweli wa mambo ni kwamba walimu wengi wa shule wanaowaongoza wanafunzi katika safari za nje ni wenye nyota ya Punda.

  Punda ni wasafiri majasiri na wanapenda vyombo vinavyokwenda kasi. Kwao ni bora kusafiri kwa ndege kuliko kupanda basi linaloenda polepole. Huwa wanapenda kusafiri daraja la kwanza kama wakikosa kabisa basi watasafiri daraja la pili.
  Ukiwa katika likizo pamoja na mwenye nyota hii unaweza ukaudhika kwa sababu wao mara nyingi wanatafuta mambo mapya na wanakuwa hawatulii sehemu moja kwa kutegemea ujasiri wao.

  Kwa ujumla kwa vile wenye nyota ya Punda ni watu wasiokuwa na subira kwa rafiki zao wa duniani hawapendi kungoja watu wakubaliane na mipango yao ya safari ambayo wanaweza kubadilisha bila taarifa. Kwa sababu hiyo mara nyingi wanasafiri peke yao, au wanaweza kujitenga mbali na walio karibu nao. Hivyo watu wa Punda wanashauriwa kuwa na subira ya kuwangoja wenzi wao katika likizo au safari zao.

  NYOTA YA PUNDA (TABIA ZAO)


  Tabia ya wenye nyota ya Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisi na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hivyo ndio mambo wanayotaka kusikia.
  Ni watu wasiokuwa na surbira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Wenye nyota hii ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu. Wao
  wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”.

  Pamoja na kwamba wanakuwa wa kwanza kukamata mambo ya msingi ya jambo lolote wao wanakuwa wa mwisho kuliacha na ni wafuatiliaji wazuri.
  Kwa upande mwingine watu hawa wewe wape njia ya kutatua tatizo au ya kufanya

  jambo jipya, utashangaa jinsi watakavyolichambua na kulitekeleza jambo lenyewe.
  Jambo la kushangaza kwa wenye nyota hii ni kwamba tatizo lao kubwa linakuwa kusitasita au kuchelewesha jambo. Pamoja na kwamba wao wanapenda mambo ya haraka lakini yakiwa hayawavutii basi huwa hawana haraka nayo.

  Vile vile wanaweza kuwa butu. Mara nyingine hufanya makosa makusudi au kuwachokoza wafanyakazi wenzao kuonyesha ubinafsi wao ili wafanikiwe.
  Kwa ujumla wenye nyota hii ni watu ambao wanajipendelea. Ni watu ambao “MIMI KWANZA” ndio tabia yao wanapenda waonekane kwamba wao ndio wanajua zaidi na tabia hiyo inawasaidia, ukweli wa mambo ni kwamba wenye nyota ya punda kila walitakalo wanalipata.
  {mospagebreak}

  TABIA YA PUNDA (KATIKA NGONO)


  Wanapokuwa chumbani, tatizo kubwa la wenye nyota hii ni ubinafsi. Watu wa Punda huwa wanapenda kujishughulisha sana na mambo ya ngono na wanategemea kwamba wapenzi wao nao wajihusishe kikamilifu katika tendo hilo. Wakiona kwamba wapenzi wao

  hawako makini wakati wa ngono basi hujihisi kwamba hawapendwi na hawatakiwi.
  Wenye nyota hii ni watu wenye bashashi na wacheshi na hiyo inawafanya wawe ni watu wenye hisia kali na haraka, hivyo inakuwa vigumu kwao kufanya mambo kwa mpangilioi na pole pole. Hivyo inawafanya wasiweze kuwachezea wapenzi wao kabla ya ngono.

  Hisia zao kubwa ni kufanya tendo la ndoa na ni wakati huo huo bila kungoja.
  Kutokana na ubinafsi huwa wanasahau kabisa hisia za wapenzi wao. Kwa kweli ni watu ambao wanajipendelea sana katika tendo la ndoa na hiyo huwa inawaletea matatizo katika uhusiano wao wa kimapenzi.

  Wakati wanapochagua mpenzi Punda wanashauriwa wahakikishe kabisa wanapata wapenzi ambao wana ashiki au nyege za haraka haraka kama wao.
  Katika kipindi cha kubembeleza pendo (kutongoza) watu wa Punda wanatakiwa waonyehse tabia ya asili ya ukarimu na mahaba ili wapendeke na vile vile wajaribu kuachana na tabia yao ya asili ya hisia kali na ukali.
  Wanaume wa nyota hii wanapenda sana kujiona kwamba wao ni mabingwa na mashujaa katika ngono.

  Kwa ujumla watu wa nyota hii ni wenye kuhitaji sana ngono. Ni watu ambao hawataki kukataliwa. Wanaume wa nyota hii wana ashiki na hamasa za kufanya ngono kuliko kupenda na wanaliangalia hilo wanapotafufa wapenzi kwa wanawake nao wana hamu kubwa ya kufanya tendo la ndoa.
  Hakika wenye nyota hii wanaweza kuwa wapenzi wazuri.

  NYOTA YA PUNDA (KAZI ZAO)


  Wote wake kwa waume waliozaliwa katika nyota hii wana kipaji cha asili cha uongozi na wasiwasi wa kushindwa katika utekelezaji.
  Kwao kitu cha pili au wao wenyewe kuwa namba mbili. Wanawake katika hali ya ushindani ambapo wanaweza kutekeleza kazi zao katika spidi au haraka wanayoitaka ambayo mara

  nyingi inakuwa mara mbili ya spidi ya kawaida, kila kitu kitakuwa sawa.
  Wenye nyota hii huwa wanafanya vizuri shughuli zao za kazi au taaluma, mradi shughuli hizo ziwe zinazoleta athari. Hawapendi kuburuzwa wala kuishi bila kupata ushindani ni kawaida mara nyingi katika kazi zao hutokea migongano kati yao na wale wenye mamlaka

  juu yao. Wanapenda sana kupambana na hali ya ushindani wa kikazi na mara nyingi huwa wakiasisi shughuli mpya au kutoa mawazo mapya. Vile vile wanapenda sana ushindani wa kutafuata kitu kilichopotea.
  Watu wa Punda ni watu ambao wanaweza kuhisi jambo lolote, ni watu wanaopenda kutumia nguvu katika kazi na wakifanya kazi yoyote wanaifanya kwa moyo mmoja.

  Wakiwa katika kazi, hupenda kufanya kazi peke yao au katika kazi hiyo wawe ni wasimamizi.
  Kwa ujumla kwa vile watu wa Punda wanafanikiwa katika ushindani wanafurahi sana wanapofanya kazi ambazo zenye vipingamizi na ambazo utekelezaji wake unahitaji akili nyingi na nguvu.
  Watu wa aina hii wakishindwa kutekeleza majukumu yao huwa wanavunjika moyo vibaya sana. Wanapenda sana kufanya kazi katika mazingira ambayo yanahitaji muda maalum kutekeleza mambo fulani.
  {mospagebreak}

  NYOTA YA PUNDA (FAMILIA ZAO)


  Wazazi wenye nyota ya Punda wanakuwa wakarimu sana kwa watotowacheshi watafanya kila njia kuwahimiza wawe huru na watawaruhusu wafanye majaribio mbali mbali ya kimaisha na kuwahimiza kuchukua majukumu makubwa kwa gharama yeyote. vile vile watawahimiza watoto wao wawe na tabia ya ushindani badala ya kuwafundisha michezo.

  Wazazi wenye nyota hii watawapa watoto wao nafasi kujisimamia wenyewe katika mambo yao. tatizo lao moja ni kuwa hawapendi watoto ambao ni ving’ang’anizi na wanaohofia usalama wao.

  Watoto ambao ni waangalifu waoge na wanaofanya mambo kwa kufikiria wanakuwa hawaendani sana na wazazi wenye nyota ya Punda kwa sababu Punda hawapendi watoto wenye haya, waoga na wepesi kutishwa.

  Wazazi wa nyota hii wanaweza kuwa wakali, wasiokuwa na mbinu na wenye kauli za ukali ambazo zinaweza kuudhi mtoto yeyote mwenye moyo mdogo. Tabia hii mara nyingi inasababisha migongano kati ya mzazi na mtoto na kutokuelewena kunakuwa kukubwa.
  Wazazi wa Punda wanashauriwa kujilinda katika kuwashinikiza watoto wao kwa nguvu na haraka na kuwaruhusu watoto hao wakue na wafanye vitu katika njia za kawaida.

  Kwa ujumla wazazi wa Punda ni wenye msukumo lakini wanajivunia sana watoto wao ni wazazi wenye makaka na wanapenda sana utani kwa vile hata wao mioyo yao ni ya kitoto. Mzazi wa kike anapenda ushindani hasa katika mausuala ya maisha na kuishi lakini hata yeye anapenda utani hasa anapokuwa nyumbani.

  NYOTA YA PUNDA (MAUMBO YAO)


  Wenye nyota ya Punda ni wenye uso mrefu mpana paji lao la uso hutanuka likiambatana na fuvu lililokaa vizuri. Macho yao ni makali na yenye kuonyesha uzima na uhai na yaliyotumbukia kwa ndani.
  Nyusi zao ni nyeusi zenye kuonekana wazi au zilizo dhahiri kama zimepakwa wanja. Pua

  zao ni za bapa na midomo yao ni mipana.
  Unapozungumza na wenye nyota hii naye atakusimamia wima mbele yako na kukuangalia moja kwa moja kwenye macho yako.

  Tabia yao hiyo inawafanya waonekane wao ni wenye tabia za kigomvi au ushauri lakini ukiangalia kwa undani utagundua kwamba ni wakweli na wanaoweza kuaminiwa.
  Hata hivyo kipindi cha kukusimamia wima inakuwa kifupi hasa anapokuona mpuuzi.
  Kimaumbile ni watu wepesi na mwendo wao ni wa madaha. Miili yao kidogo imeinamia mbele ya misuli yao inaonekana imekakamaa, hiyo ni kwa sababu ya kujishughulisha sana bila kupumzika.

  Sifa za wanaume wa Punda ni kwamba wako makini na wenye msimamo. Ni wembamba na miili yao ni yenye misuli iliyojikunja kunja.
  Wanawake nao ni wembamba na maumbile yao siyo ya kupendeza sana, mikono yao na miguu yao ni yenye nguvu. Matamanio yao na uwezo wao huwa inawafanya wawe wanawake wenye tabia za kiume.

  Kwa ujumla alama ya Kondoo ni pembe zake na mambo yote yanayohusiana na pembe hizo. Wenye nyota hii wanapenda kupambana na maisha. Kimaumbile athari zao huonekana mara moja. Kama vile kujiamini, namna wanavyosalimia watu na vicheko vyao. Vitendo vyao hivyo vinakujulisha kwamba huyu ni Punda.
  {mospagebreak}

  NYOTA YA PUNDA (VYAKULA VYAO)


  Kama ilivyo katika tabia zao wenye nyota ya Punda vile vile wanapenda vyakula vya haraka haraka.
  Ukweli ni kwamba mawazo yao mara nyingi yanakuwa katika maisha kuliko chakula pamoja na kwamba wanakuwa na hamu na uwezo mkubwa wa kula. Wanapenda chakula kizuri lakini kiwe cha haraka na rahisi kutayarisha.

  Wanapenda sana kufanya karamu tafrija ambazo wana kipaji kikubwa cha kuzitayarisha na wanazifurahia. Katika karamu hizo vyakula vyao vinakuwa vya haraka ambavyo vinagawiwa wima wima bila kucheleweshwa.
  Wakati wanapokuwa hawafanyi karamu au tafrija wanapenda chakula chochote

  kinachotayarishwa upensi na ambacho kinaweza kulika huko wanatembea, kama vile asusa na vyakula vyepesi kama biskuti, chipsi n.k.
  Wanapenda ladha iwe nyepesi na viwe na pili pili na viungo vingi. wanapenda sana vyakula vinavyopooza au kutuliza njaa kama viazi, tambi na maziwa.

  Huwa wanapenda sana ladha za uchachu kama limao limao au ndimu ndimu au mbilimbili vile vile wanapenda sana mkate na Jibini au vyakula vilivyo kaangwa kama nyama.
  Wanatakiwa wawe waangalifu katika kula mafuta hasa vyakula vya kipuuzi puuzi ambavyo vinaweza kuwaletea madhara.
  Kwa ujumla wenye nyota hii wanapenda sana tafrija, na vyakula wanapenda viwe vile vinavyotayarishwa mbele ya wageni na viwe vilivyokaangwa na vyenye ladha nzuri. Vyakula hivyo viwe ni vyepesi kutayarisha visivyopoteza muda.

  NYOTA YA PUNDA (VIPAJI VYAO)

  Wenye nyota hii wanapenda sana kupambana na maisha na wanakuwa na mambo mengi sana vichwani mwao kiasi kwamba wakati mwingine wanasahau vipaji vyao vya asili.
  Tabia hiyo waliyo nayo haiwapi muda wa kufanya mambo mengine kama ya ubunifu. Kwa

  asili, wao ni watu wabunifu na wakati mwingine wanapata wasiwasi katika ubunifu wao.
  Kuna wakati wenye nyota hii wanashindwa kutofautisha kati ya vipaji vyao na matakwa yao. ambayo yanakuwa makubwa na yenye shinikizo. Watapata msaada katika hili iwapo watafanya jitihada za maksudi za kuwasiliana na busara zao za asili kuwa kupata

  mapumziko na kufanya taamuli (Meditation).
  Kipaji cha wenye nyota hii kinahusiana na kichwa ambacho ndio nyota yao inapotawala hivyo “Frenologia” (Ujuzi wa tabia ya mtu kwa umbo la kichwa chake iko chini ya nyota hii.

  Kwa kuongezea wenye nyota hii wana kipaji cha kutafsiri ndoto na kipaji cha kusikia sauti ndani ya kichwa.
  Kwa ujumla watu wa Punda wanapenda njia ya utabiri ambazo zinatoa matokeo ya haraka kama vile kutumia karata , dhumna, au dadu (dice).
  Taamuli (meditation) ni jina au mbinu nzuri kwa wenye nyota hii kuongeza kipaji chao. Ikiwa watafanya taamuli kwa dakika ishirini wakati wa usiku au kitu cha kwanza wanapoamka asubuhi, akili na miili yao itatuliza. Hivyo itawafanya wawe na uwezo wa kutumia nguvu zao za kimwili na kiakili pamoja na kuendeleza au kukuza vipaji vyao.
  {mospagebreak}

  NYOTA YA PUNDA (BAHATI ZAO)


  Watu wa nyota hii wana tabia ya kitoto ya kuamini kwamba mazuri yatatokea kwa amri ya Mungu. Kwa hiyo inawawia vigumu kufikiria uwezekano wa kushindwa katika jambo lolote.
  Wakiwa ni waliozaliwa katika nyota yenye kuasisi mambo, wengi wao hudharau kutopata matumaini katika jambo moja na kurukia jambo lingine.

  Kwa sababu shauku yao ni ya kuambukiza mara nyingi hufanikiwa kuwashawishi wengine wakubali kuongozwa nao hata kama kuna khatari.
  Mara nyingi hawana muda wa kutoa mashitaka wala kuwaza makosa yaliyofanyika mwanzoni, wao wanaamini kwamba wakati wote mafankii yapo na kwa vile wamezaliw ana roho ya ujasiri wa kupenda vituko wako tayari wakati wowote kuyaweka maisha yao katika hatari ili wafanikiwe.

  Tabia yao ya kutojali na misukumo au mihemko ya ghafla inawafanya wawe na sifa zilizokithiri za kubahatisha mambo.
  Hakimu kwa bahati, hii kwao inakuw asiyo tatizo kwa sababu hawafanya kitu kimoja kwa muda mrefu, ghafla huwa wanarukia katika jambo lingine.

  Watu wa Punda wana moyo wa ujasiri wa ushindani na wanafanya vizuri iwapo katika hali hiyo kutakuwa na uadui hasa mtu na mtu.
  Katika michezo ya karata ua kupimana nguvu au kuwekeana dau watu wa Punda wana pata bahati sana.

  Kwa ujumla watu wa nyota hii wanapenda kubahatika na wanachukia sana kukosa pamoja na kwamba faida zoa wanazopata zinalingana na hasara zinazowafika.

  NYOTA YA PUNDA (URAFIKI)

  Wenye nyota ya Punda ni wachangamfu, wanaosema kweli na wenye uwazi katika urafiki wao. Kama walivyo katika kila kitu kwenye maisha yao.
  Ni wazuri katika kuanzisha urafiki, wakati mwingine wanakuwa wawazi sana katika mazungumzo yao na vitendo vyao kiasi kwamba huwaogopesha baadhi ya marafiki.
  Kwa upande mwingine wao wanapendwa kwa sababu ya uaminifu wao na kusema kweli.

  Watu wa Punda wanathamini sana uhuru wao na wanapenda kufanya vitu katika njia zao wanachukia sana kufugika au kuogopa watu kwa hiyo urafiki sio kitu muhimu kwa wenye nyota hii . wakati mwingine huwa wanajisikia furaha wanapokuwa katika kundi la watu wanaopenda vituko na mambo ya ajabu.

  Watu wa Punda wako katika kundi moja na wale wenye nyota zenye asili ya moto na tabia zao zinafanana. Mfano wale wenye nyota ya Mshale wanakuwa marafiki wao wazuri ambao wanachangia tabia ya kupenda vituko.
  Hata hivyo huwa hawapendi au hawaoni umuhimu wa kuwa na rafiki mwenye nyota ya

  Mapacha. Kwa wenye nyota ya Ndoo kwa vile wanathamini uhuru wao basi wao wanaweza kuelewana nao.
  Watu wenye nyota zenye asili ya udongo Mbuzi, Ng’ombe na Mashuke wanakuwa marafiki wazuri wa Punda kwa Sababu wanamsaidia kutekeleza mipango yake kivitendo, pamoja na

  kwamba madhari na akili za hao Ngo’ombe, Mbuzi na Mashuke kupunguza nguvu ya urafiki wa kudumu.
  {mospagebreak}

  Kwa ujumla wote wenye nyota zenye asili ya moto mara kwa mara wanakuwa na tofauti na wenye nyota ya Punda hasa katika masuala ya ushindani mfano ni nyota ya simba na Punda wote huwa wananeemeka kutokana na uadui usioepukika katika urafiki wao, kama ikiwa katika kazi au nyumbani au kwenye starehe au wanapokuwa pamoja katika michezo.

  NYOTA YA PUNDA (MITINDO)


  Mitindo ya Punda ni yenye kuchangamka na nguo zisizo na madoido. Wanapenda wawe wanavaa kulingana na wakati. Mavazi yao huwa yanaambatana na mabegi, saa nzuri au mikufu na vito vyenye kupendeza.

  Hata hivyo watu wa Punda hawapendi kupanga kununua au kushona nguo. Wanapendeza sana wakiwa katika mavazi ambayo ni mepesi kuliko nguo zile zilizosanifiwa na zenye madaha.

  Suti zilizotafauti yaani suruali na koti tofauti, zikiambatana na buti pamoja na skafu na glavu ndio mavazi hasa na nyota ya Punda. Mavazi hayo yanaendana hasa na tabia yao ya ujasiri na mambo ya ajabu.

  Wengi wenye nyota hii huwa wanapenda kuvaa suti za michezo ambazo pia zinaendana na namna yao ya maisha.
  Wanapoamua kuvaa nguo, waume kwa wake wanakuwa wavaaji wazuri. Wanapenda nguo zilizoshonwa vizuri na zinazoeleweka.

  Rangi zao zinakuwa Nyekundu na Njano na mara nyingi hupendelea nguo zisizo na nakshi.
  Wanapenda mitindo thabiti na vitambaa ambavyo ni vyepesi kuvitunza. Wanawake wanapenda sana mikufu ya dhahabu na hereni za kuning’inia.
  Kwa ujumla watu wa punda wanapenda kuvaa kulingana na mitindo na wanapenda nguo ambazo zinawafanya watu wakiwaona washituke wakiamua kuvaa nguo maalum basi mavazi hayo yataambatana na vitu vya ziada kama mikufu. Pete, saa visivyo ghali. Hiyo huwainawafanya waonekane na wakati katika mavazi ya aina yeyote.

  NYOTA YA PUNDA (TASWIRA YA UMBO)


  Inapofikia hali ya kuweka miili katika hali bora wenye nyota hii wana bahati kubwa kutokana na hali halisi ya maisha yao ya kujishughulisha. Kwa kuongezea labda wawe wanapenda kula lakini kama ilivyoanishwa na nyota yao ni watu ambao hawapendi sana vyakula vinavyoweza kuwaletea unene.

  Hata hivyo wanafurahia chakula na wanapenda vyakula vyepesi. Kama ikiwa Kalori zinazoingia mwilini zinazidi zinazotoka basi uzito wao huongezeka.
  Inapofikia hali ya kupunguza uzito wenye nyota hii wanakuwa hawana subira, wanapenda mlo ambao utapunguza uzito wao upesi na katika muda mfupi inavyowezekana ikiwa ni pamoja na kujiadhibu wenyewe kwa kujimyima chakula kwa muda mfupi wakiwa na imani yakupata matokeo.

  Kwa wenye nyota hii muda wa siku chache au hata wiki moja ni muda tosha wa kujinyima chakula ili kupunguza unene.
  Baada ya hapo ni juu yao kuwa na ratiba maalum ya ulaji wao ikiambatana na mazoezi ya kila siku, kama kuongelea, kukimbia, au kutembea kwa nguvu kwa muda mrefu wenye nyota hii wanahitaji mazoezi ya kila siku ili waweze kupunguza uzito. Vinginevyo itawawia vigumu baadaye.
  {mospagebreak}

  Kwa ujumla wenye nyota hii huwa wanapata uzito mkubwa kwa sababu huwa wanajishughulisha sana kula milo ya kawaida ikiambatana na vitu vitamu vilivyojaa Kalori wanapokuwa wamechoka.
  Wanashauriwa kutumia muda wao kula tu milo ya kawaida hiyo itawasaidia kuondoa au kupunguza unene na kuboresha afya zao.

  NYOTA YA PUNDA (USHINDANI NA UADUI)


  Wenye nyota hii wanapenda sana ushindani na kuonyesha madaraka na uwezo wao, kwa sababu hii wanachukiwa na watu wengi. Wanapenda sana wawe wa kwanza na watatumia mbinu zozote ili wafanikiwe.

  Punda wako wazi na waaminifu katika malengo yao ni watu wenye kusema ukweli na haamini visingizio, ulaghai wala kuficha siri.
  Wanapenda kufanya mipango yao moja kwa moja na mtu yeyote akiingilia huwa unazuka ugomvi. Ikitokea hivi watu wa Punda huwaeleza wagomvi wao bila kuficha kinachoendelea.

  Kutokana na ukweli na uwazi wao wenye nyota hii huwaudhi sana watu wengine kwa maneno yao na vitendo vyao.
  Ni tabia yao kutojali hisia za watu na wala hawana muda wa kufikiri, maneno wanayosema au vitendo vyao vitawaathiri vipi wenzao.

  Mara nyingi watu wa Punda, hushinda vita vyao kutokana na uwezo wao na nguvu zao za ukatili lakini ikitokea pakatakiwa kujieleza au kutoa hoja au diplomasia huwa wanashindwa kujieleza.

  Wakiwa katika siasa hali ya uadui huibuka kutoka kila upande, wao huneemeka sana Kisiasa kutokana na upinzani na uadui mkali uliopo duniani ambao wao hufurahia.
  Kwa ujumla watu wa Punda ni washindani katika sehehmu zote, ni madereva wanaopenda kwenda kasi hivyo wanapenda mashindnao ya magari. Mara nyingi watu wa nyota hii wanapenda michezo yenye ushindani au kutumia nguvu ikiwa kama jambo la kupitisha muda au kazi yake, na hii inawapa changamoto katika kuendeleza ushindani wao wa Asili.

  NYOTA YA PUNDA (MANUNUZI)


  Kama tulivyoona tangu mwanzo wenye nyota hii wanapenda ushindani, kushughulika na vitendo na hawapendi kabisa kufuata utaratibu kwa hivyo kununua vitu ni mojawapo wa mambo wanayoyapenda sana.
  Vile vile wanapenda kupungua na kupanda kwa manunuzi au msisimko wa kwenda dukani

  katika mitaa inayopendeza au katika nchi za nje.
  Wenye nyota hii wanapokwenda kufanya ununuzi hufanya juhudi ya kuamka mapema ili wawakwepe watu, na manunuzi yao wanayafanya haraka haraka.
  Huwa wanakwenda kutoka duka moja hadi jingine wakizunguka kiuerevu kufanya manunuzi.

  Wanapenda kununua vitu vya wiki nzima na orodha yao lazima vitakuwepo vyakula vya kupikwa kwa haraka au vya kuliwa papo kwa papo kama nyama za kopo au Samaki wa Kopo. Mara nyingi hawana muda wa kupika na hawapendi kutumia muda wao mwingi jikoni.

  Kwa hiyo kitu ambacho hawa watu wa Punda wanapenda kununua. Jibu ni kwamba wanunue chochote ambacho kitaharakisha mwendo wa maisha yao.
  Mfano wanapenda magari yanayo kwenda kasi au vitu ambavyo wanaviota, kama ramani, glavu za kuendesha gari na viatu.

  Kwa ujumla watu wa Punda huwa hawapendi kwenda dukani kila siku lakini wanaona raha ikiwa kwa kufanya hivyo watapata ushindani.
  Wanapenda kushindana na rafiki zao ili kuonyesha nani atanunua mwanzo na kitu kizuri au kubishana katika bei ya kitu fulani, hiyo inawafanya wajisikie raha sana.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe April 20 – May 20 Tabia zao ni hizi hapa

  Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12.Wenye nyota hii ni wale ambao wamezaliwa kati ya tarehe 20 April na May 20 ya mwaka wowote.

  • Sayari yao ni Venus (Zuhura).
  • Siku yao ya bahati ni Ijumaa.
  • Namba yao ya bahati ni 6.
  • Rangi yao ya bahati ni kijani.
  • Asili ya nyota yao ni Udongo.

  KIPAJI CHA NG'OMBE

  (BODY-CENTERED)
  Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa kilicho ndani ya mwili wao ambacho ni pamoja na kuelewa mambo kimbele, hesabu, kuponya kwa kutumia mikono na kwa kumwagia mtu maji.

  TABIA YA NG'OMBE:


  Wenye nyota hii ni watu wanaopenda kujishughulisha katika shughuli nyingi. Ni watu wakarimu na wanaopenda kusaidia watu, na wana tabia ya uvumilivu na subira katika jambo lolote wanalolifanya.
  Ni watu wenye malengo na wenye msimamo thabiti, wasiopenda kupindishwa na wana tabia ya ubishi na ukaidi hasa katika jambo lao wanalolitaka.

  TABIA YA NG'OMBE KATIKA MAPENZI:


  Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
  Pamoja na kwamba asili yao ni udongo, wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi

  makubwa kwa wapenzi wao.
  Uhakika wa mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.

  Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao.
  Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.

  Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi kubadilishwa.
  {mospagebreak}

  MATATIZO YA KIAFYA:


  Nyota hii inatawala shingo, koo, koromeo, kidevu na sehemu ya chini ya taya.
  Kwa asili wenye nyota hii ni watu wabishi na wenye kufanya mambo kwa upole na wagumu kubadilika.

  Wanapenda sana vyakula vitamu na vyenye mafuta na huwezi kuwabadilisha katika hilo na wengi wao wanakuwa wanene kupita kiasi na inakuwa ni vigumu sana kuwashawishi kuamka na kufanya mazoezi ya mwili.

  Tatizo lingine ni kufanya kazi kupita kiasi ambalo linawafanya wapate matatizo ya mvutano na misuli hasa katika sehemu zilizotajwa. wenye nyota hii wanatakiwa wajihadhari na mpangilio wao wa chakula na wafanye mazoezi kwa wingi.

  KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'OMBE:


  Wenye nyota hii wana falsafa ifuatayo kulingana na kazi; "panda mbegu iote, mti uote halafu ule matunda". Ni watu ambao wanafuata mpangilio wa kikazi na wanaopenda kujituma na kujishughulisha. Wengi wenye nyota hii ni wafanyakazi wazuri na wanapenda

  wapewe muda kujenga vipaji na utaalamu wao wa kazi.
  Kazi zao zinakuwa kazi za muziki, kazi zinazohusiana na chakula, hoteli, migahawa, kazi za ujenzi, kazi za mashamba, kazi za uhasibu, na kazi za sanaa hasa uchoraji au uchongaji vinyago.

  FAMILIA ZA NG'OMBE:


  Wazazi wa familia za Ng'ombe ni watu wenye msimamo, wakutegemewa na wanaothamini familia zao, na wako tayari kugombana na mtu yeyote kwa ajili ya watoto wao.
  Ni wazazi wanaopenda kufuata mambo ya kizamani au ya asili hasa katika masuala ya nidhamu. wanapenda sana kuheshimiwa na watoto wao na huwashawishi au kuwashauri wawe huru.

  Ni wazazi wanaotegemea watoto wao wafuate nyayo zao hasa katika biashara au kazi wanazozifanya, hivyo watoto wa wazazi Ng'ombe wanakuwa na muda mdogo wa kufikiria mambo mapya.

  Ni wazazi ambao hufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wao hawakosi wanachokitaka na wanapenda watoto wao wawe na elimu nzuri. Hata hivyo ni wazazi ambao wanategemea watoto wao wafuate wanavyotaka wao vinginevyo inakuwa matatizo.

  MADINI YA NG'OMBE:


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa ALMASI au EMARALD.
  Mawe haya yanawafanya wenye nyota ya ng'ombe wawe katika hali yao ya kike kike (Feminine) vili vile thamani ya mawe haya ni uthibitisho wa nyota hii katika fedha.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI:


  (NG'OMBE NA N'GE):

  Tabia ya uaminifu na ukweli waliokuwa nao wenye nyota ya ng'ombe inakuwa ni faraja kubwa kwa nyota ya Nge ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi na kudhania maovu, kutuhumu na kushuku.

  VYAKULA VYA NG'OMBE:


  Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao; Tofaa (apple), (oysters), viazi mbatata (potatoes), na dover sole.

  NCHI ZA NG'OMBE:


  Ili kupata mafanikio ya kinyota, kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; baadhi ya nchi hizo ni USSR (Urusi), Ireland, St louis,na Lucerne (Switzerland).

  RANGI ZA NGOMBE:


  Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za kijani au rangi za pinki au rangi ya bluu ambayo haijakoza katika nyumba zao au sehemu zao ya biashara ili kuleta mvuto wa kinyota.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe May21-June21 Tabia zao ni hizi hapa
  NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)

  • Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei na 20 Juni ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Mercury (Attarid).
  • Siku yao ya bahati ni Jumatano.
  • Namba yao ya bahati ni 5.
  • Rangi yao ya bahati ni njano na bluu isiyoiva.
  • Asili ya nyota yao ni upepo.
  KIPAJI CHA MAPACHA: (TELEPATHIC):

  Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo.

  TABIA ZA MAPACHA:


  Watu wenye nyota hii ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza na wanaweza sana kushawishi watu.
  Ni watu ambao wanapenda sana mabadiliko na tofauti na wanapenda sana kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki. Wanapenda kusafiri sana.

  TABIA YA MAPACHA KATIKA MAPENZI:


  Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
  Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.

  Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.

  Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
  Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.

  Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
  {mospagebreak}
  MATATIZO YA KIAFYA:

  Nyota hii inatawala mabega, mikono, viganja na sehemu ya juu ya mbavu.
  Tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii. Wanafikia mpaka hali ya kuisahau miili yao na mara nyingi

  wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.
  Matatizo yanayotokana na nyota hii ni mgonjwa kukosa pumzi (bronchitis), pumu (asthma), matatizo ya kifua, mafua, flu, ajali za mara kwa mara kwenye mikono na mabega.

  KAZI ZA WENYE NYOTA YA MAPACHA:


  Kwa vile wenye nyota hii asili yao ni upepo na wao ni wenye kuzaliwa kwenye mawasiliano na uhusiano, wanapenda sana uhuru na uwazi katika kazi zao.
  Wanapenda sana kazi ambazo zinawashughulisha na kufanya akili zao zisipumzike lakini

  siyo jambo hilo hilo kwa muda mrefu. Kuwa na mawasiliano na watu wengi kwa wakati mmoja ndio jambo linalopendwa na wenye nyota hii. Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa radio na televisheni.

  Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.
  Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au kazi za biashara lakini zinazohusiana na safari za nje.

  FAMILIA ZA MAPACHA:


  Watu wa nyota ya Mapacha ni waliochangamka na wenye hiari na wazazi wa Mapacha huingia katika msisimko wa watoto wao kwa raha.
  Ni wazazi wenye furaha muda wote katika kutekeleza shughuli zao za nyumbani pamoja na kupenda kucheza na watoto wao na wana mipango mizuri na wanajua wapi wakiwapeleka watoto watafurahi.

  wenye nyota hii wanathamini sana elimu na hawawezi kuishi bila mawasiliano na habari, hivyo huwa wanapenda kuwanunulia watoto wao vitabu vingi.
  Tatizo linalotokea iwapo mtoto ataonyesha kwamba hapendi kusoma na watajaribu kila

  njia kumuweka katika njia wanayoitaka wao. Wakishindwa wanaacha.
  Wazazi wa Mapacha hawawezi kuelezea jambo na hawana uvumilivu wa kun'gan'gania kwa mtoto asiyeelewa mambo.

  MADINI YA MAPACHA:


  Wenye nyota ya Mapacha wanatakiwa wavae madini ya Agata au kito chochote chenye rangi ya njano. Kito hicho inasemekana kinamuwezesha mvaaji awe na uwezo wa mawasiliano na ufahamu.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI:


  (MAPACHA NA MSHALE)

  Tabia ya Mapacha ya kupenda kufahamu na kuelewa mambo hutulizwa na tabia ya Mshale ambao ni wasomi na wenye kuelewa mambo mengi.

  VYAKULA VYA MAPACHA:


  Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao. Vyakula vyenyewe ni kuku, rasiberi, karoti na uduvi.

  NCHI ZA MAPACHA:


  Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).

  RANGI ZA MAPACHA:


  Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ikipakwa ndani ya nyumba.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe June 22- Mpaka July 22 Tabia zao ni hizi hapa

  NYOTA YA KAA (CANCER)

  Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12.

  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Juni na tarehe 20 July ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni mwezi (moon).
  • Siku yao ya bahati ni Jumatatu.
  • Namba yao ya bahati ni 2 na 7.
  • Rangi yao ya bahati ni Nyeupe.
  • Asili ya nyota yao ni Maji.

  KIPAJI CHA KAA (SENSITIVE):


  Wenye nyota hii wana kipaji cha hisia ya kugundua mambo yanayotendeka ikiwa ni pamoja na kubashiri mambo, kumwelewa mtu kwa undani na kujua jambo ambalo mtu anataka kulifanya au jambo litakalotendeka hasa kwenye watu wengi.

  TABIA ZA KAA


  Watu wenye Nyota hii ni wenye tabia ya hisia nzito ni wapole na wenye huruma. Wakiwa na dhamira ya ulezi na kuwaangalia watu wengine na hiyo inaonekana waziwazi katika nyumba zao na familia zao.

  Hata hivyo upande mwingine ni watu ambao wana gubu na wakali ne wenye kupenda kujishughulisha na wanajiamini.
  ni watu ambao wanaweza kubadilika lakini wenye msimamo na itikadi na wanaweza kuwa ni wenye wivu mkali na wenye kudhibiti.

  TABIA YA KAA KATIKA MAPENZI :


  Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa wenye nyota hii pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanapenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.

  Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu na wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.

  Wenye Nyota hii bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo basi huwa hawana raha.
  Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
  Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.

  MATATIZO YA KIAFYA:


  Nyota hii inatawala njia kuu ya chakula kuelekea tumboni, mbavu, mfupa wa kidari, tumbo la uzazi, utumbo mdogo na utumbo au sehemu zote za kusagia chakula.
  Vile vile inatawala bandana na matiti.

  Tatizo lao kubwa la maradhi yao linatokana na ukimya wao wanapoudhiwa. Inapotokea hivyo wao hushindwa kusema na huumia kimya kimya.
  Maradhi yao makubwa yanakuwa maradhi yanayosababishwa na gesi , au vidonda vya tumbo au kiungulia au maradhi yanayotokana na mwili kuwa mnene au umbo kubwa.
  {mospagebreak}

  ZA WENYE NYOTA YA KAA:


  Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi ambazo zitawafanya wao wawe walezi wa wale wanaowatumikia ili kukidhi mahitaji ya nyota yao.
  Wanatakiwa wafanye kazi za utabibu kama vile Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini

  kama vile mabaharia, kazi za huduma ya chakula kama hoteli, migahawa, kazi za kuhudumia watoto kama katika shule za chekechea, kazi za benki au kazi za maneja utumishi au kazi za kuandika.

  FAMILIA ZA KAA:


  Wenye nyota hii ni wazazi asilia, na wazazi wakiume mara nyingi huonekana wakiwasaidia wake zao kulea watoto.
  Wanafanya kwa bidii kuhakikisha familia zao zinapata kila kitu kinachohitajika.

  Mzazi wakike ana hisia kiuzazi kuliko mume na kwa mtoto kwa mtoto anyependa kuwa huru kuna muda hujihisi kwamba mama yake anambana.
  Wazazi wa nyota hii wana tabia ya kuangalia mambo yaliopita nyuma hivyo hupenda mambo yasibadilike milele.

  Hali ya Wazazi hao ya kubadilika badilika huwapa wakati mgumu watoto hasa wale wenye hisia ndogo ambao huhisi wanasukumwa sana na hutaka kujikomboa ili waondokane na baa hilo.
  Wazazi wenye nyota hii hupenda sana watoto wao wafanye wanzozitaka wao kinyume na matakwa ya watoto wao .

  MADINI YA KAA:


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae madini ya moonstone au jiwe lolote lenye rangi ya maziwa.
  madini haya yana uwezo wa kuongeza hisia na kufanya wawe na ari ya kuwatumikia na kuwakinga wenzao.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI:


  Tabia ya Mbuzi ya ubahili na kutopenda anasa hulainishwa na tabia ya Kaa ya upendo, huba na huruma ambayo humfanya mbuzi atulie na atumie kile alichonacho .

  VYAKULA VYA KAA:

  Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vyakula vinavyotawaliwa na nyota yao.
  Vyakula vyenyewe ni kama Mapeas, kaa au vyakula vya baharini, na mboga kama kabichi na saladi (lettuce).

  NCHI ZA KAA:


  Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika miji au nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.
  Miji hiyo ni New York (Marekani) na Venice (Ugiriki) au nchi za New Zealand na Scotland.

  RANGI ZA KAA:


  Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe July 23- Mpaka august 22 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA SIMBA (LEO)

  • Hii ni nyota ya tano katika mlolongo wa nyota kumi na mbili.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21Julai na 21 Agosti.
  • Sayari yao ni Jua (Sun).
  • Siku yao ya bahati ni Jumapili.
  • Namba yao ya bahati ni 1 na 4.
  • Rangi yao ya bahati ni Njano au rangi ya Dhahabu.
  • Asili ya nyota yao ni moto.
  KIPAJI CHA SIMBA (INSPIRED):

  Wenye nyota hii wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.
  Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi.

  TABIA ZA SIMBA:


  Watu wenye nyota hii ya Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Ni watu wanaopenda kutumia na wanataka waonekane na wanuwezo wa kuvumbua mambo amabyo watu wengine hawajui na wanapenda sana heshima.
  ni wakarimu lakini ni wajeuri na wanapenda kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.

  TABIA YA SIMBA KATIKA MAPENZI:


  Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.
  Furaha haina mpaka katika mapenzi ya simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito

  hutokeza dhahiri wanapompenda mtu.
  Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.

  Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.

  Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.

  Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.

  MATATIZO YA KIAFYA:


  Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.
  Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.
  Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo.

  Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.
  Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.
  {mospagebreak}

  KAZI ZA WENYE NYOTA YA SIMBA:


  Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.

  Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.

  Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.
  Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.

  FAMILIA ZA SIMBA:


  Kwa asili Simba ni Mfalme na mamlaka yake yamezungukwa na hisia za kifalme. Wazazi wa simba huwa wana mila ya kuwapangia watoto wao namna watakavyoishi kwa sababu wanajivunia sana familia zao.

  Wazazi wa Simba wanajiona kwamba wana nafasi kubwa katika dunia ambayo inawataka wajionyeshe kwa watu ubora. Pamoja na kwamba wenye nyota hii hupenda kuzunguka na watoto wao (na wao wenyewe wakati mwingine wana tabia ya utoto) hawakubali

  kupoteza heshima zao wakati wanafanya hivyo.
  Wenye nyota hii ni wachangamfu, wenye moyo wa kupenda na wanapenda raha, pamoja na ukali wao wanaweza kuwa wepesi kwa watoto wao.

  Watu wa simba kwa uhakika wanaona raha kuwa wazazi lakini wanatakiwa wawe makini kutowaharibu watoto wao kwa zawadi nyingi na maisha ya raha.
  Simba wana uhakika na nafasi yao katika jamii kwamba wao ni viongozi hivyo watoto wao huwa wanapenda kujionyesha na wanategemea wawe wanaonekana kwa watu muda wote.
  MADINI YA SIMBA:

  (AMBER); Jiwe hili lenye rangi ya njano iliyochanganyika na kahawia linasemekana lina uwezo wa kumpa ukakamavu na ari ya uongozi kwa anayelivaa, vilevile linamwepusha mvaaji na maradhi ya kichwa.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (SIMBA NA NDOO):

  Tabia ya Simba ya kutopenda kudhibitiwa au kudhibiti watu inakuwa ni faraja kubwa kwa wenye nyota ya ndoo ambao wanapenda uhuru na kufanya mambo yao bila kuingiliwa.

  VYAKULA VYA SIMBA:


  Wenye nyota ya simba wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao.
  Vyakula hivyo ni machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo.

  NCHI ZA SIMBA:


  Watu wa nyota ya simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.
  Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia)

  RANGI ZA SIMBA:


  Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe August 23- Mpaka September 22 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA MASHUKE (VIRGO)

  • Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale wote ambao wamezaliwa kati ya tarehe 23 Agosti na 22 Septemba ya mwaka wowote.
  • Siku yao ya bahati ni Jumatano.
  • Namba yao ya bahati ni 5.
  • Rangi zao ya bahati ni Njano na Bluu isiyoiva.
  • Asili yao ni Udongo.
  KIPAJI CHA MASHUKE:

  Wana kipaji cha kuhisi au kufikiri au kutambua tatizo au ugonjwa au kupata picha ya wazi akilini ya kutambua jambo lolote. Vilevile wana uwezo wa kuponya na wana uwezo wa kusoma michoro yeyote.

  TABIA YA MASHUKE:


  Watu wote wenye nyota ya Mashuke ni watu ambao wanapenda kusoma. Wana akili nzuri ambayo inatumika zaidi katika kupambanua njia ya asili ya mpangilio wa mambo.
  Kwa ujumla ni watu ambao wanapenda kufuata kanuni na kufanya mambo kwa usahihi kabisa.

  Ni watu waangalifu sana hasa katika mambo madogo madogo na wanapenda kushutumu hasa mambo yanapokwenda vibaya.
  Wanatabia ya kuchunguza mambo na kuhakikisha mpangilio unafuatwa kikamilifu. Ni wenye kujituma na kujishughulisha na wanapenda sana kufuata sheria au mpangilio maalum ulioainishwa.

  TABIA YA MASHUKE KATIKA MAPENZI:


  Pamoja na kwamba wanaonekana ni watu wenye aibu kwa undani na kujiamini, wenye nyota hii hupumzika na kunawiri wanapokuwa katika mapenzi.
  Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe.

  Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani. Ni vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na Mashuke.
  Inawawia vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa.

  Kinachowasaidia ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua.
  Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.

  Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi wake ili amshutumu.
  Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.
  {mospagebreak}

  MATATIZO YA KIAFYA:


  Nyota hii inatawala utumbo, sehemu ya uvunguni mwa utumbo na neva zote zilizo chini ya kitovu.
  Kutokana na asili hiyo wale wenye nyota hii huwa wanapata sana matatizo ya maradhi ya ugonjwa wa tumbo au tumbo la uzazi au matatizo ya kizazi.

  Magonjwa ya mwili kushindwa kusaga chakula tumboni au magonjwa ya kujikunja utumbo na maambukizo ya utumbo.

  KAZI ZA WENYE NYOTA YA MASHUKE:


  Ni watu ambao ni tegemezi na wenye bidii ya kazi na wana tabia ya kufanya kazi bila ya kuchoka. Wanapenda sana kazi zenye mpangilio na ambayo kila kitu kikiwa katika mpangilio maalum.

  Wanapenda kuwa huru katika kazi zao na wanapenda kujitosheleza katika kila wanachokifanya na wanapenda kufanya kazi bila ya kusimamiwa.
  Kazi zao ni zile zinazohusiana na uchapishaji, utangazaji, afya, udaktari, kazi za unesi, kazi za uongozi, elimu na kufundisha, biashara au kazi za ukatibu muhtasi.

  FAMILIA ZA MASHUKE:


  Wazazi wa nyota ya Mashuke ni watu ambao wanajali sana utaratibu wao ili wawe na maisha yaliyo na mpangilio na yenye uhakika. Kinyume na hivyo huwafanya wawe na wasiwasi.

  Wana tabia ya kuwapeleka watoto wao hospitali mara kwa mara wakiamini kwamba watoto wakipata dawa za kinga hawatopata maradhi na wanapenda sana kuweka madawa nyumbani kwa akiba.

  Pamoja na kwamba wazazi hawa wanapenda sana wawaelewe watoto wao, wanatatizwa sana na watoto ambao wanashindwa kusikiliza maneno yao.
  Kwa ujumla wazazi hawa huwa wanashindwa kujieleza kwa watoto wao kulingana na kile wanachokipenda kama vile katika michezo au masomo.

  MADINI YA MASHUKE


  (SARDONYX):
  Kito hiki kinatakiwa kichongwe sanamu yeyote ili kiashirie alama ya mwanake wa Mashuke. Wenye nyota hii wanapata nguvu ya kupendwa.
  Kito chenyewe kinasemekana kina nguvu za ajabu za kutibu maradhi sugu.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (MASHUKE NA SAMAKI):
  Tabia ya Samaki ya fikra na ndoto za mambo ya baadae inapata faraja kubwa kwa Mashuke ambao ni wenye busara na wanaopenda kutumika na kutekeleza yale wanayotakiwa kufanya wakati wowote.

  VYAKULA VYA MASHUKE:


  wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao; vyakula vyenyewe ni kuku, rasiberi, karoti na uduri.

  NCHI ZA MASHUKE:


  Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota ya Mashuke wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; nchi hizo ni Austria na Norway na miji hiyo ni Jerusalem na Paris.

  RANGI ZA MASHUKE:


  Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi Nyeupe au rangi ambazo siyo nzito au zenye kuonekana
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe September 23- Mpaka Octobere 22 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA MIZANI (LIBRA)

  • Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na 22 Oktoba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni VENUS (ZUHURA).
  • Siku yao ya Bahati ni Ijumaa.
  • Namba ya Bahati ni 6.
  • Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.
  KIPAJI CHA MIZANI

  (Extra Sensory Perception)
  Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.

  TABIA ZA MIZANI:


  Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.

  Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

  TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI


  Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.

  Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
  Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina

  matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
  Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana

  kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
  Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.

  TABIA YA MIZANI KATIKA FEDHA


  Watu wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kutokuwa na maamuzi katika masuala ya fedha. Lakini hiyo siyo sababu ya wewe kufikiri kwamba wao ni wajinga.
  Wanapofanya hivyo huwa wanapima au kufikiria kuona uwezekano wa fedha kutumika vizuri.

  Ni watu wenye mipango mizuri na mara nyingi kwa kutumia uzoefu na kipaji chao kidiplomasia na upole, huwa wanapata mafanikio katika biashara zao.
  Wana kipaji cha kuelewa watu wengine wanahitaji nini na wanatumia maneno matamu kuwashawishi wawape wanachokitaka na wanafanikiwa.

  Wanapenda sana vitu vizuri na vyenye thamani na wako tayari kutumia fedha yeyote kutekeleza malengo yao.
  Kwa ujumla ni watumiaji wazuri na wenye ubinafsi mkubwa.
  {mospagebreak}

  MAVAZI YA MIZANI


  Wenye nyota ya Mizani wanatakiwa wavae nguo yenye kupendeza zenye mapambo na zenye kuashira mahaba.
  Nguo ziwe za rangi ya Pinki au rangi ya udongo.


  Kitambaa kiwe cha kotoni chepesi na chenye picha picha, kisiwe kile ambacho hakikuchorwa kitu.
  Wavae sana mikanda na wapende kuvaa nakshi za maua pamoja na skafu au mitandio iliyoingia. Wanapendelea mavazi ya ushanga na mikufu.

  MATATIZO YA KIAFYA


  Nyota hii inatawala figo, sehemu ya utumbo mkubwa, kiuno, mpaka sehemu ya juu ya Makalio

  Sababu kubwa ya maradhi yao ni kwamba wanapenda sana kutafuta amani na suluhu hata wakiudhiwa au kukasirishwa. Matokeo yake wanavunjika moyo na kujinyima yale wanayoyapenda. Sana na hiyo inawafanya waudhike na wajisikie vibaya na inawasababishia maradhi.

  Magonjwa yao makubwa ni figo, kibofu cha mkojo, ugonjwa usioambukiza wa ngozi unaowasha na unapojikuna huvimba (Eczema),maradhi ya misuli ya kiuno na matoki.
  Tatizo lingine kubwa ni unene.Watu wa mizani wanapenda sana kula na hiyo inatokea sana wanapokuwa wameudhiwa. Wao wanaona ni bora zaidi kuondoa hasira zao kwa kula chakula.

  KAZI ZA WENYE NYOTA YA MIZANI


  Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia uwezo wao wa kuzaliwa na inawawia vigumu wakati mwingine kutafuta kazi wanazozipenda.
  Wanapenda kufanya kazi katika mazingira ya amani na yasiyo na usumbufu.
  Kazi zao hasa zinakuwa za uhusiano wa jamii ushauri wa ndoa, biashara ya sanaa, ushauri wa mambo ya urembo au mwanasheria.

  FAMILIA ZA MIZANI


  Wazazi wenye nyota ya mizani wanapenda sana unadhifu na wanapenda watoto wao wawe nadhifu na wenye mavazi mazuri.
  Wanapenda kutumia muda mwingi na fedha nyingi kuwafunza watoto wao tabia nzuri. Kwao ni muhimu sana mtoto akikubalika na kila mtu.
  Wanapenda amani katika nyumba zao na wana tabia ya kuwapangia watoto wao namna ya kuishi na kufanya vitu ambavyo wao wnyewe wameshindwa kuvifanya.

  MADINI YA MIZANI


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa LAPIS LAZULI. Mawe kama nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa kama kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (Punda na Mizani)

  Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

  VYAKULA VYA MIZANI:


  Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo ndio yanayotawaliwa na nyota yao,Tufaha (Apple), viazi Mviringo (Potatoes), Chaza (Oyster) na Nyama ya Njiwa.

  NCHI ZA KUISHI ZA MIZANI:


  Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii ya Mizani.
  Miji hiyo ni Copenhagen (Denmark) na Vienna (Austria) na nchi ni Canada na Japan.

  RANGI ZA MIZANI


  Wenye nyota hii wanapenda rangi zilizopakwa juu juu na laini hivyo wanashauriwa watumie rangi ya aina yeyote lakini iwe hafifu katika nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe Octobere 23- Mpaka November 21 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA NG'E (SCORPIO)

  • Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 October na 21 Novemba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni MARS (MARIIKH).
  • Siku yao ya Bahati ni Jumanne.
  • Namba yao ya bahati ni 9.
  • Rangi ya bahati ni Nyekundu isiyoiva au Maroon.
  • Asili yao ni MAJI.
  KIPAJI CHA NG'E (MYSTICAL)

  Wenye nyota hii wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji.

  TABIA ZA NG'E


  Wenye nyota ya Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni watu wenye uelewa mkubwa na ni majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.

  Ni wenye tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.

  Ni watu wenye tabia ya siri na wanapenda kufanya mambo yao kwa siri sana.Wenye nyota hii kama ilivyo alama yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.

  Ni watu wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
  Watu wa Nge vile vile wana tabia au wanaweza kujidhuru wao wenyewe.Mambo yanapowawia magumu.

  TABIA YA NG'E KATIKA MAPENZI


  Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.

  Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.

  Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.

  Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
  {mospagebreak}

  TABIA YA NG'E KATIKA FEDHA


  Hakuna kitu kinachoshindikana kwa wenye nyota hii, na chepesi zaidi ni namna ya kupata fedha. Wana uzoefu mkubwa wa kuhimili matatizo ya kifedha wanapoanguka, hata wakiwa matajiri na wakafilisika.

  Watu wa Nge wana bahati ya kuvumbua fedha au utajiri katika njia ambazo watu wengine si rahisi kugundua.

  Ni watu ambao sio rahisi kudanganyika wakiona mpango wowote wa kifedha. Mara nyingi ni kawaida yao kuchukua kitu au kufanya mradi ambao wengine wanauona wa kipuuzi na wakaugeuza kuwa wa thamani kubwa.

  Ni wakarimu sana wanapokuwa na fedha, na hawapendi kujidai kwa utajiri wao. Wako tayari wakati wowote kuwatumia watu wengine kutekeleza malengo yao.
  Kwa ujumla wao ni wataalamu wa kutafuta fedha katika njia ambazo watu wengi hawazifahamu.

  MAVAZI YA NG'E


  Wenye nyota ya Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong’ara, zenye kuonekana na maridadi,zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja.
  Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta.
  Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali.

  MATATIZO YA KIAFYA


  Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi(cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).

  Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono. Wakati mwingine hisia zao zinakuwa kubwa sana kiasi kwamba wao wenyewe wanajishuku vibaya.

  Inapotokea hivi wanahitajika kusafisha miili yao kwa fadhaa iliyowajaa kutokana na mfadhaiko wa hisia zao.

  Kwa ujumla ni watu wenye afya nzuri na wanapona haraka maradhi yanayowasumbua. Wenye nyota hii wana tabia ya aidha kula, kunywa au kuvuta kupita kiasi au wengine hawafanyi mambo hayo kabisa.

  Kwa vile nyota hii inatawala sehemu zinazoondoa uchafu wa mwili ni vizuri watu wa Nge wakawa waangalifu na mambo yanayochafua mwili wao.

  Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya kike na mabusha.
  {mospagebreak}

  KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'E.


  Nyota ya Nge ambayo alama yake ya asili ni Maji ni nyota mojawapo ya nyota zenye nguvu katika mambo ya kikazi.

  Ni watu wenye milipuko ya hisia wanapokuwa katika miradi yao ya kazi. Wanafanya shughuli zao kwa hisia kali na hamaki na wanategemea wapate majibu ya kuridhisha.
  Ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu

  wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni watu waerevu na wenye kung’amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.

  Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono.

  FAMILIA ZA NG'E


  Wazazi wenye nyota ya Nge ni watu ambao wanaonyesha utulivu wa hali ya juu. Kimaumbile huwa hawaonyeshi hisia walizokuwa nazo juu ya watoto wao, wanaweza wakawa na chuki kubwa lakini hawapendi kuiionyesha.

  Kwa ujumla wazazi hao wanapenda watoto na wanatumia muda mwingi na hisia zao kuwangalia na kuwadhibiti watoto wao.

  Pamoja na ukarimu wao ni wazazi wenye kupenda nidhamu na wanataka watoto wao wafuate maadili mema. Wazazi hao walivyokuwa wadogo wamepitia ujanja wote hivyo hawakubali watoto wao wawadanganye.

  Watoto watagundua kwamba wazazi wao ni watu wa kutisha na kuogopwa lakini uhusiano wao unakuwa ni mzuri. Wazazi wa kike wanakuwa na hisia kali kwa watoto wao kitendo ambacho kinawafanya watoto wawe katika shinikizo.

  MADINI YA NG'E


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa BERYL NA RED CORNELIUS. Mawe haya yenye rangi ya damu ya mzee (Maroon) na rangi Nyekundu yanaakisi au kuashiria asili ya Nge ya uhusiano wake wa asili na kitu chochote cha miujiza na uchawi.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (NG'E, NG’OMBE)

  Tabia ya Nge ya wasiwasi, wivu, hisia kali za kimapenzi na dhana mbaya kwa wapenzi wao hutulizwa na kuzimwa na nyota ya Ng’ombe ambao wana tabia ya utulivu, uaminifu, wasioyumba na wanaopenda kusikiliza wanayoambiwa.

  VYAKULA VYA NG'E


  Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

  NCHI ZA NG'E

  Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.
  Miji hiyo ni Liverpool(Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.

  RANGI YA NGE


  Wenye nyota hii wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon).
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe November 22- Mpaka December 21 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA MSHALE (SAGITTARIUS)

  • Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 22 November na 21 December ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni Jupiter (Qawsi).
  • Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
  • Namba yao ya Bahati ni 3.
  • Rangi yao ya Bahati ni Hudhurungi.
  • Asili yao ni MOTO.

  KIPAJI CHA MSHALE (Prophetic)


  Wenye nyota hii wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.

  TABIA ZA MSHALE


  Wenye nyota ya mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe kama wao.

  Hawapendi mambo nusunusu na ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.

  Ni watulivu na ni waaminifu na wanapenda uadilifu. Ni watu ambao hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa

  kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
  Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake mradi jambo hilo liwe la kweli.

  TABIA YA MSHALE KATIKA MAPENZI

  Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.

  Wenye nyota hii wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Ni watu wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.

  Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.

  Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.

  Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali na inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.
  {mospagebreak}

  TABIA YA MSHALE KATIKA FEDHA


  Alama ya nyota hii ni Mshale na mategemeo yao ya kifedha yanalenga mbali na juu sana.
  Wenye nyota hii fedha kwao ndio njia pekee ya kujikomboa na kupata uhuru hivyo wako tayari kufanya jambo lolote hata kama ni la hatari ili wapate fedha na wanapozipata huzitumia bila mpangilio.

  Mara nyingi huwa hawapendi kutafuta fedha zao katika njia za kawaida wanapenda sana kutumia njia tofauti na kubuni mbinu mbali mbali kutekeleza malengo yao.
  Ni watu ambao hawaoni haya kumtumia mtu mwenye pesa au uwezo ili watekeleze

  malengo yao. Kwa sababu hii wengi wao wanakuwa matapeli.
  Matatizo yao makubwa ni kwamba wao ni watumiaji wabaya na hawana mipango thabiti ya matumizi ya fedha na ni watu ambao wakitoa ahadi ya fedha hawatekelezi.

  MAVAZI YA MSHALE


  Wenye nyota ya Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha kama koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi kama maua au nakshi nakshi.

  Rangi ya nguo zao iwe ya Zambarau au rangi ya Hudhurungi iliyochangamka au rangi ya blue.
  Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda, na viatu viwe vya buti.Wanawake wapendelee kuvaa sketi.

  MATATIZO YA KIAFYA:


  Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.

  Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao.
  Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.

  Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini (Liver Disorder) kupooza kwa miguu (paralysis of limbs) na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.

  KAZI YA MSHALE


  Kupata au kukosa, kushinda au kupoteza, kuna uchangamfu wa asili kwa nyota hii na uzoefu katika hali yeyote.
  Ni watu waaminifu wanaopenda sana mafankio na wako tayari wakati wowote katika kazi.

  Kutokana na hili wanakuwa na bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.

  Wenye nyota ya Mshale ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Ni wenye kuwaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
  Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.
  {mospagebreak}

  FAMILIA ZA MSHALE


  Wazazi wenye nyota ya Mshale ni wenye kuwachangamsha sana watoto wao. Nyumba zao zinakuwa zinajaa vitabu na vifaa mbali mbali na wanawahimiza sana watoto wao wawe huru na majasiri.

  Wenye nyota hii wanapenda kuwatembeza watoto wao katika sehemu za elimu, kama vile, Makumbusho au sehemu za kihistoria.

  Elimu na masomo hupewa kipaumbele na mzazi mwenye nyota ya mshale ambaye mara nyingi huhakikisha mtoto wake anasoma. Wazazi hawa wanapata matatizo makubwa kuwadhibiti watoto wasiosikia kwa sababu wao wenyewe wanapenda uhuru kwa sababu hii huwa wanavumilia tabia mbaya za watoto wao hata watoto wakiwa wajeuri.

  MADINI YA MSHALE


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa SAPPHIRE. Mawe haya nyenye rangi ya bluu yana uwezo mkubwa wa kinyota wa kumletea mvaaji afya nzuri, nguvu na kinga vitu ambavyo wenye nyota hii wanavihitaji.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (Mshale na Mapacha)

  Tabia ya kufanya mambo haraka haraka au kukata tamaa na kupenda kuelewa mambo ya wenye nyota ya Mapacha inaingiliana vizuri na wenye nyota ya Mshale ambao ni wenye busara na subira na wasiokata tamaa.

  VYAKULA VYA MSHALE


  Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kunazi za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera.

  NCHI ZA MSHALE


  Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
  Nchi hizo ni USA na SPAIN na miji ni Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).

  RANGI ZA NYOTA


  Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni.

  Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe December 22- Mpaka January 19 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA MBUZI (CAPRICON)

  • Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 22 Dec na 19 Jan ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni SATURN (ZOHAL)
  • Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
  • Namba yao ya bahati ni 8.
  • Rangi yao ya bahati ni rangi ya Kijivu au Nyeusi.
  • Asili yao ni Udongo.
  KIPAJI CHA MBUZI(GRADUAL)

  Wenye nyota hii wana kipaji cha kuchambua mambo kidogo kidogo au kufuatilia kitu bila watu kujua na kupata ufumbuzi wa uhakika mwishoni.

  TABIA ZA MBUZI


  Wale wote waliozaliwa katika nyota hii ni watu ambao wanapenda kuwajibika, ni wenye bidii ya kazi, katika kazi yeyote watakayofanya hata kama ikiwa ni ya kipuuzi.
  Ni viumbe waaminifu sana na ni watu wastahamilivu na wenye kuweza kuvumilia matatizo yeyote.
  Kwa upande mwingine ni watu wenye tamaa kubwa ya kimaisha na kimaendeleo, na kwa sababu ya kutekeleza malengo yao basi huwa wanakuwa wabinafsi na wenye uroho na uchu.

  TABIA YA MBUZI KATIKA MAPENZI


  Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.
  Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.

  Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.

  Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.

  YA MBUZI KATIKA FEDHA


  Kwa watu wenye nyota hii fedha ni kitu muhimu sana katika maisha.
  Watu wa Mbuzi wanaamini kabisa kwamba fedha ndio zitawapa uwezo wa kuweza kupambana au kukabiliana na mazingira ya Dunia, hivyo basi suala lolote la fedha na mali wanalichukulia kwa uzito mkubwa sana.

  Inawachukua muda mrefu kutekeleza malengo yao ya kifedha lakini wakishazipata basi huwa hawatetereki tena. Wana uwezo wa kuhifadhi walichonacho.
  Ni watu wabahili sana na hata kama wakiwa na fedha nyingi utaona wanaishi maisha ya kawaida na wala huwezi kuwajua.

  Fedha zao zinatoka kwa sababu maalum ya dharura na wala siyo katika starehe au vinginevyo na hiyo ni kwa sababu hupenda kukumbuka walikotoka katika hali ya umasikini au ufukara.
  {mospagebreak}

  MAVAZI YA MBUZI


  Wenye nyota ya Mbuzi wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi.
  Nguo hizo ziwe za rangi ya kijivu au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.
  Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi.
  Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikononi.

  MATATIZO YA KIAFYA


  Nyota hii inatawala Mifupa, Magoti na Ngozi.
  Matatizo yao makubwa ya kiafya huwa yanasababishwa na muda mrefu ambao wanafanya kazi au kujishughulisha.

  Hii ni kwa sababu hawamwamini mtu mwingine afanye shughuli zao ambazo zina mipangilio ya muda mrefu, nguvu nyingi, na akili hutumika.
  Shughuli zao nyingi za mizunguko na kufikiria huwaletea maradhi kama Baridi Yabisi (rheumatism).

  Maradhi yao mengine makubwa ni ugonjwa wa ngozi, matatizo ya Magoti na maradhi ya mifupa.

  KAZI ZA MBUZI


  Wenye nyota ya Mbuzi kitu muhimu katika maisha yao ni kazi na maisha mazuri na yanayoeleweka ambayo yako katika mpangilio wanaoutaka wao.
  Ni watu ambao wanazingatia sana muda wa maisha na wana mpangilio maalum kwamba

  katika umri fulani awe amepata nini au awe na fedha kiasi gani.
  Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo.
  Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno.

  FAMILIA ZA MBUZI


  Wazazi wenye nyota ya Mbuzi ni watu ambao wamepangilia kabisa mipango ya watoto wao kabla hawajazaa.

  Ni wazazi ambao wanayachukulia kwa uzito mkubwa majukumu yao ya kulea na hawakubali kabisa watoto wao kufanya michezo michezo ya kipuuzi. Wanapenda kuwahimiza watoto wao kuwa na malengo ya maana.

  Wanapenda sana nidhamu katika familia zao.
  Mara nyingi wazazi wa kiume huwa hawapati muda kuwa na watoto wao kutokana na kazi nyingi walizonazo lakini kwa wazazi wa kike wanakuwa wanatumia akili ya hali ya juu katika kutatua matatizo au hisia za watoto wao.

  MADINI YA MBUZI


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinayoitwa Black Jet.
  Jiwe hili inaaminiwa lina uwezo wa kuongeza ujasiri na kumletea mvaaji mafanikio ya kibishara.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI (MBUZI NA KAA)

  Tabia ya Mbuzi ya ubahili na kutopenda anasa hulainishwa na tabia ya Kaa ya upendo, mapenzi na huruma.

  VYAKULA VYA MBUZI


  Wenye nyota ya Mbuzi wanashauriwa wapende kula vyakula au matunda yafuatayo. Ambayo ndio yanatawaliwa na nyota yao.
  Wapende sana vyakula vya Nazi na Nyama yeyote.
  Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba (Shellfish).

  NCHI ZA MBUZI


  Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa watu wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee miji au nchi zifuatazo ambayo inatawaliwa na nyota ya Mbuzi.
  Miji hiyo ni Brussels (Ubelgiji) na Oxford (Uingereza) au nchi za Mexico na India.

  RANGI ZA MBUZI


  Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe January 20- Mpaka February 18 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini


  NYOTA YA NDOO (AQUARIUS)

  • Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 20 January na 18 February.
  • Sayari yao ni SATURN (ZOHAL).
  • Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
  • Namba yao ya bahati ni 8.
  • Rangi yake ya bahati ni Nyeusi.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.

  KIPAJI CHA NDOO


  (Sudden Revelation)
  Wenye nyota hii wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote.

  TABIA ZA NDOO


  Wenye nyota ya Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.

  Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.
  Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa

  shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.
  Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.

  TABIA YA NDOO KATIKA MAPENZI.


  Wenye nyota ya Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.

  Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.

  Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.

  Ni watu ambao wenye kusema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.

  Katika ngono kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.

  Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.
  {mospagebreak}

  TABIA YA NDOO KATIKA FEDHA


  Wenye nyota ya Ndoo ni watu ambao wenye ndoto na mipango mingi ya kifedha ya baadae, na wakati mwingine wanajikuta kwamba mawazo yao ya kifedha yanakuwa hayaendani na wakati uliopo.

  Masuala ya kifedha kwao yanategemea sana aina ya kazi, ambayo mara nyingi inahusiana na mambo ya sanaa au sayansi, sehemu ambayo wao watajihisi wanatoa mchango wao kwa binaadamu.

  Wanapokuwa matajiri mara nyingi inatokana na ustadi au umahiri na wale siyo uwezo wao.

  Wenye nyota hii huwa wanapenda sana kupata fursa ya kufanya kazi sehemu tofauti na hawependi kufungika katika sehemu moja, kwao fedha ni chombo kinacholeta uhuru na wanaona vyema maisha yao yakamilike kuliko kuwa tajiri.

  Mara nyingi wanachukia kuonekana kwamba wao ni wabinafsi. Hata hivyo wanapenda vitu vizuri lakini kwa sababu ya ubahili huwa wanaona raha wanapoviona vitu hivyo kwa watu wengine katika makumbusho au nyumba ya sanaa kuliko kuwa navyo wenyewe.

  MAVAZI YA NDOO


  Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya Kijivu, au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.
  Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi. Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikono.

  MATATIZO YA KIAFYA.


  Nyota hii inatawala kifundo na ugoko. Wenye nyota hii wana mawazo mapana ya kufanya mabadiliko ya Dunia na hii inawasababisha wajisahau hasa katika afya zao na mara kwa mara hupata matatizo ya kuugua.

  Kutokana na ubishi wao mara nyingi wanakuwa wabishi kupokea ushauri kuhusiana na hali zao za kiafya.

  Matatizo yao makubwa yanasababisha na kuchoka kwa misuli kutokana na kazi nyingi na ni wagonjwa wabishi wasiopenda ushauri.

  Wanapofanya mazoezi wanashaurwa wasiwe na hasira kwani hiyo inawafanya wajiumize au wapate ajali ndog ndogo hasa sehemu za miguu, ugoko, vifundo na uvimbe katika sehemu hizo.
  Vile vile matatizo yao mengine ya kiafya ni mzunguko wa damu na mishipa ya miguu.

  KAZI ZA NDOO


  Hawa ni watu wenye akili nyingi na wenye malengo maalum katika shughuli fulani. Ni wawekezaji asili na wana uwezo wa kuwabadilisha watu tabia zao kutoka mbaya kuwa nzuri.

  Kwa uhakika mawazo yao saa zote yanafanya kazi. Ni watu ambao muda wote wanafikiri njia mpya na za uhakika za kutekeleza wajibu wao na kikazi.

  Kazi zao wanazifanya kwa upole na uhakika, pamoja na kwamba wanafanya kazi kwa bidii mara nyingi huwa wanaonekana hawajafanya kitu au sifa huenda kwa watu wengine.
  Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.

  Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.

  {mospagebreak}

  FAMILIA ZA NDOO


  Wazazi wa nyota hii ni wenye shauku na wasiotabirika na wanaopenda maendeleo ya watoto wao.
  Wazazi wa Ndoo wako wazi na wanaweza kuzungumza chochote na wototo wao lakini ni wagumu kubadili mawazo yao ambayo wakati mwingine yanakuwa ya ajabu.

  Huwa wanapenda kuwahimiza watoto wao wawe huru kujieleza lakini wao wenyewe hawapendi kushutumiwa. Kwa upande mwingine ni wazazi ambao hawana mbinu katika kushughulikia mambo yanayowahusu watoto.

  Ni wazazi wanaowapenda watoto wao na wao wanapendwa sana na watoto na mara nyingi huwa hawalalamikiwi.

  Ni muhimu kwa wazazi wa kiume wenye nyota hii kuwaelewa vizuri watoto wao vinginevyo tabia zao zinaweza zikasababisha migongano.
  Kwa wazazi wa kike wanashauriwa waache tabia yao ya kigeugeu au ukali tabia ambayo mara nyingi watoto huudhiwa nayo.

  MADINI YA NDOO


  Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa Aquamarine Madini hayo yenye kumeremeta yanaashiria hewa ambayo ndio asili ya nyota ya Ndoo.
  Jiwe hili linaashiria urafiki na inasemekana huondoa uchovu wa akili.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (NDOO NA SIMBA)

  Tabia ya kupenda kuwa huru na kujifanyia mambo bila kuingiliwa waliyokuwa nayo wenye nyota ya Ndoo, huwafariji wenye nyota ya Simba ambao nao hawapendi kuingiliwa katika mambo yao.

  VYAKULA VYA NDOO.


  Wenye nyota ya Ndoo wanashauriwa wepende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota zao.
  Wapende sana vyakula vya nazi na nyama aina zote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba.

  NCHI ZA NDOO


  Ili kupata mafaniko ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
  Nchi hizo ni Sweden na Zimbabwe na Miji ni Humburg (Ujerumani) na Leningrad (Urusi).

  RANGI ZA NDOO


  Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia kama Bluu au Kijivu.
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa Wale waliozaliwa Kutoka Tarehe February 19- Mpaka March 20 Tabia zao na nyota yao hii hapa chini

  NYOTA YA SAMAKI (PISCES)

  • Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 19 February na tarehe 20 Machi.
  • Sayari yao ni JUPITER (MUSHTARA)
  • Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
  • Namba yao ya Bahati ni 8.
  • Rangi yao ya Bahati ni Zambarau au Kahawia iliyochangamka.
  • Asili ya nyota yao ni Maji.

  VIPAJI VYA SAMAKI (VISIONARY)


  Wenye nyota hii wana kipaji cha kufikiria jambo na kuliunda na likawa vile walivyotaka wao.

  TABIA ZA SAMAKI


  Watu wenye nyota ya Samaki ni wenye huruma, wapole na wenye moyo mzuri na hawawezi kukubali kumuona binaadamu mwingine akipata taabu au uchungu. Kwa hakika ni watu ambao wana hisia kati kwa wengine ni watu ambao hawajipendelei na wako tayari

  wakati wowote kujitoa mhanga ili watu wanufaike, mapenzi yao au huruma kwa binadamu wengine hayana masharti yeyote.

  Nafsi zao zimegawanyika katika nafsi ndogo ndogo kama vile muathiriwa mwenye kujitoa mhanga, mwokozi, na mkombozi.

  Hayo yote yaliyotajwa wanaweza kuyatekeleza inapohitajiwa na ikiwa mwenye nyota hii akishatumbukia katika moja ya mambo hayo huwezi kumtoa.
  Kwa ujumla nafsi za wenye nyota ya Samaki siyo za kidunia, ni watu wabunifu na wenye

  ndoto za kufikiri mambo ya baadaye na katika maisha yao wanaona raha sana kuwa na mawazo ambayo yatawaepusha na ugumu wa maisha.
  Ikiwa wamekwama katika jambo lolote basi wataitafuta faraja au watajituliza kwa ulimwengu wao wa mawazo.

  TABIA YA SAMAKI KATIKA FEDHA


  Ni vigumu sana kukadiria tabia za wenye nyota hii katika fedha kwa sababau wote waliozaliwa katika nyota huwa wanachanganyikiwa kwa sababu huwa wanashindwa kutafautisha kati ya matumizi na thamani ya fedha.

  Hii ni kwa sababu wanashindwa au hawakubali vikwazo kati ya muda na nafasi au za kwako na zangu, kwao kila kitu ni sawa sawa.
  Pamoja na kwamba wana uroho wa pesa, uwezo na matamanio lakini wanajichukulia

  mambo kadri yanavyokuja. Kwao wakiwa na fedha sawa wakiwa hawana sawa vile vile kwao uwezo wa kubuni au kutunga taswira ni muhimu kuliko fedha.
  Mara nyingi huwa wanajishughulisha na masuala ya kutatua matatizo ya watu wengine kuliko masuala ya kifedha. Wakati wote wako tayari kupoteza fedha kuliko kuibiwa ndoto zao.

  TABIA YA SAMAKI KATIKA MAPENZI


  Wenye nyota ya Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
  Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.

  Ni watu wenye hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
  Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.

  Ni watu wenye kuyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.

  Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazohazipo katika dunia hii.
  Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapwnzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao

  yanakuwa makubwa na yaispotimia huwa wanavunjika moyo.

  {mospagebreak}

  MAVAZI YA SAMAKI


  Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wavae nguo za michezo kama vile fulana au za kiasili na zilizoongezwa madoido na vimbwanga vingi.
  Nguo zao ziwe za rangi ya Zambarau au Kahawia iliyochangamka na rangi ya bluu.

  Kitambaa kiwe cha sufu (tweed)
  Wanawake wapendelee sana kuvaa sketi, ikiambatana na mikanda na viatu vyao viwe vya bati.

  MATATIZO YA KIAFYA


  Nyota hii inatawala nyayo na vidole vya miguu.
  Matatizo yao ya kiafya yanakuja pale wanaposhindwa kutekeleza ndoto zao au mipangilio yao kimaisha au wanapokorofishana na wapenzi wao.
  Wanapoathirika na hayo yaliyotajwa hukimbilia kwenye ulevi na utumiaji vidonge uliokithiri.

  Tatizo lingine ni maradhi ya nyayo za miguu, uvimbe unaotokana na baridi kali hasa katika vidole vya miguu.

  KAZI ZA SAMAKI


  Kugunuda muelekeo wa kimaisha kwa wenye nyota hii wakati mwingine huwa ni matatizo.
  Tabia yao ya kushughulikia sana binaadamu wengine huwafanya wasiwe na muelekeo.
  Wenye nyota hii wanatakiwa wasifanye ubaguzi katika kazi.

  Wanatakiwa wafanye kazi ambazo zinazohusiana na kusaidia watu. Kipaji cha kutafsiri mambo huwasaidia vile vile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo.
  Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini (Navy) kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha (Counselling).

  FAMILIA ZA SAMAKI


  Wenye nyota hii ni wazazi wenye hisia, wanaopenda watoto wao na wanahuruma hasa watoto wanapowasikiliza.
  Pamoja na hayo wazazi wa Samaki wana matatizo ya kukubali kwamba watoto wanaweza

  kuwa tofauti na wao, hata mwishowe wanapokubaliana na hilo huwa wanawachukulia watoto wao kama wageni kuliko ndugu.

  Mtoto akiwa anapenda kusoma na mwenye kujituma au akiwa na tabia ya kutumia sana akili kuliko moyo huwa hapendwi na mzazi wa Samaki.
  Wazazi wenye nyota hii wana mipangilio mibovu ya nidhamu na muelekeo, hivyo watoto

  wakorofi huwa wanatumia mwanya huo kufanya mambo yao.
  Hiyo ina maana kwamba watoto wa wazazi wa Samaki wanaweza kuharibika au kutumiwa kutokana na udhaifu wa wazazi wao.

  {mospagebreak}

  (MADINI YA SAMAKI)


  Wenye nyota hii wanashauriwa wavae madini yanayoitwa.
  Madini haya yanasaidia kupunguza hisia na kumuepusha mvaaji na ulevi.

  UHUSIANO WA KIMAPENZI


  (SAMAKI NA MASHUKE)
  Tabia ya Samaki ya kuwa na mbinu na mawazo ya mambo ya baadaye huenda sambamba na tabia ya Mashuke ya utekelezaji na kujishughulisha bila kuchoka.

  VYAKULA VYA SAMAKI


  Wenye nyota ya Samaki wanashauriwa wapenda kula matunda au vyakula vifuatavyo.
  Matunda ya Kunazi, Nyama mwitu kama Swala,nyati na kadhalika.
  Vile vile wapendelee kula maboga.

  NCHI ZA SAMAKI


  Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao.
  Nchi hizo ni Tonga na Tanzania na miji ni Alexandria (Misri) na Seville (Ufaransa).

  RANGI ZA SAMAKI


  Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi ambayo haijakoza ya Bluu au Kijani au Urujuani (violet).


  NAWATAKIENI WANACHAMA WOTE NA WAPENZI WOTE WA JAMII FORUMS KHERI YA MWAKA MPYA 2011 HAPPY NEW YEAR 2011 :A S clock::hug: HII NDIO ZAWADI YANGU KWENU ASANTENI.
   
 14. D

  Derimto JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asante kaka hasa hapo kwenye kondoo
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Thanx mkuu
   
 16. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mungu akupe jitihada pia utuwekee na matukio ya 2011.
  Ila umeelezea in detailed . Kuhusu kila nyota kwa mwaka huu watakuaje sijaona!
  Ila kama kawaida mwenye ilm hua hatosheki...nimezidi kupata faida zaidi.
  Japo nimefafananisha na kitabu kilichotungwa Na Mtaalam Paker's ni mume na mkewe.
  Happy New Year 2011.
  Wataamini inapokua ni kweli.
   
 17. October

  October JF-Expert Member

  #17
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Vipi tena Mzizi !!
  Mbona unatuwekea mabandiko ya utabiri, Ushirikina na kuosha Bahati?
  Au umekua mfuasi wa elimu ya Shekhe Yahya siku hizi?

  [​IMG]

  Nimekua nikikuoona kwenye jukwaa la dini ukiwa mstari wa mbele kutetea dini nikadhani uko Serious na unachokiamini kumbe danganya toto.
  Vipi Mzizi imekuaje unaamua kuanza mwaka mpya kwa kukumbatia ushirikina na utabiri?
   
 18. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #18
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwani ushirikina ni nini maana yake?
  Pia Utabiri ni nini maana yake?
  October!
  Hivi ukienda kupimwa haja kubwa nayo ni ushirikina au utabiri?
  Tafauti ni nini kati ya kupimwa haja kubwa na hayo mengine?
   
 19. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #19
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  NYOTA YA MASHUKE (VIRGO) kaka hapa umenikuna wala hujakosea nakupa:whoo:Happy New year!
   
 20. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa member!
   
Loading...