Haya kama maajabu vile


Bubu Msemaovyo

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Messages
3,435
Likes
58
Points
145
Bubu Msemaovyo

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined May 9, 2007
3,435 58 145
Watanzania tumekuwa wepesi sana wa kuiga mambo mbali mbali toka sehemu nyingine aidha kwasababu tumeona katika picha au kusikia hebu soma hii taarifa huwezi kuamini kama imetokia Tanzania. Mbona mazuri ya huko tunakoiga mabaya hatuyaigi???

Aliyemchinja mdaawa wake kutinga Mahakama Kuu

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/12/17/habari33.php


na Anthony Komanya, ShinyangaMTU mmoja anayedaiwa kumchinja kwa panga na kuondoka na kichwa cha mdaawa wake hadi mahakamani, atafikishwa mbele ya Mahakama Kuu kujibu tuhuma za mauaji, imefahamika.
Akisoma maelezo ya awali, wakili wa upande wa mashitaka, Robert Mkoba, aliiambia Mahakama Kuu mjini Shinyanga kuwa mtuhumiwa Ndito Sukumawiki, alimkatakata na kumchinja kwa panga, akitenganisha kichwa na kiwiliwili mdaawa wake, aliyemshinda kwenye kesi ya madai ya nyumba ya thamani ya sh 60,000, Yusuf Charles.

Wakili Mkoba alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwa marehemu Machi 5, mwaka 2002 majira ya saa 5:00 usiku katika Kijiji cha Kimali wilayani Meatu, Mkoa wa Shinyanga.

Mkoba aliendelea kudai kuwa, baada ya kumkata kichwa, Sukumawiki, aliondoka na kichwa cha marehemu hadi kwenye Mahakama ya Mwanzo ya Kimali, ambako aliendelea kufanya vitendo vya kinyama.

Akiwa mahakamani huko, alisema mshitakiwa alipaka milango, madirisha na sakafu kwa damu inayosadikiwa kuwa ya marehemu, kwa kuandika herufi 'n.d.s' hapa na pale mahakamani humo.

Ilidaiwa kuwa, akiwa anaendelea na vitendo hivyo vya kinyama, mshitakiwa alikurupushwa na mlinzi wa mahakama hiyo na kutoroka hadi alipokamatwa siku nyingi baadaye.

Ilidaiwa kuwa katika maelezo ya ungamo la awali mbele ya mlinzi wa amani wa Mahakama ya Mwanzo Kimali, mshitakiwa alikiri kufanya mauaji hayo ya kinyama.

Hata hivyo, wakati akisomewa maelezo ya awali, mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo mbele ya Jaji Alice Chinguwile na hivyo kesi yake kupangwa kusikilizwa katika kikao kijacho.
 
Mnhenwa Ndege

Mnhenwa Ndege

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2007
Messages
243
Likes
12
Points
35
Mnhenwa Ndege

Mnhenwa Ndege

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2007
243 12 35
jamani mbona kesi imechukuwa muda mrefu wakati the facts are clear yani tangia 2002 mpaka 2007!!!!!!!!
 
Bundewe

Bundewe

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
401
Likes
1
Points
35
Bundewe

Bundewe

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
401 1 35
Hii kweli inatisha! Yaani 60,000 zamtoa mwenzio roho??
 

Forum statistics

Threads 1,238,887
Members 476,223
Posts 29,335,613