Haya huyo wenu wa CIA mnayemuami kwamba ni mkweli, aletwe sakata la Tundu Lisu!

Pia CIA hushiriki kuunda vikundi vya Uasi hususani huko Uarabuni na sehemu zingine Duniani, CIA ni chombo hatari sana na hutumika kufanya biashara ya siraha za Marekani
Ndio uongo wenyewe huo, ndio kudanganya kwenyewe huko..

Kudanganya, kuzuga Dunia ndio kazi kubwa ya hicho chombo
 
Nadhani wewe ndio huelewi ya kwamba CIA ndio baba wa FBI ! Collections of all FBI findings are centrally processed by CIA especially when it comes to INTERNATIONAL Security matters for the US and its allies !
Si kweli mkuu, ni vyema ukawa umesoma na kujua majukumu ya vyombo hivyo viwili kikamilifu ndipo uandike hayo uliyoandika. Ebu google basi ujue vizuri mkuu.
 
Jibu lipo hapo juu, tofauti kati ya FBI na CIA ni kwamba FBI wanahusika ndani ya USA na CIA nje ya USA, hivyo kama mkiomba na USA akikubali kutuma watu atatuma CIA kwa maana CIA ndo sana Expertise na foreign countries FBI hawana, FBI wako trained kuhudumia ndani ya USA!
Sio kweli haya uliyoyasema Mkuu, CIA ni SHIRIKA LA KIJASUSI linalofanya kazi kwa maslahi ya Marekani..

MFANO Serikali ya Marekani hawakumpenda Raisi fulani, Labda tuseme Magu, CIA Watafanya uongo, uzushi, uchonganishi mpaka Raisi husika aondoke madarakani..

FBI hawa ni WAPELELEZI WA POLISI wanaweza kufanya kazi katika jimbo lolote la Marekani, Unaujua Marekani kila jimbo lina sheria zake lakini ni Polisi wa Muungano wanaweza kuingilia jimbo lolote..

Kwa vile FBI wamebobea kwenye uchunguzi wa kipolisi hawa jamaa wanaweza kuitwa na kufanya kazi nje ya Marekani..
 
Si kweli mkuu, ni vyema ukawa umesoma na kujua majukumu ya vyombo hivyo viwili kikamilifu ndipo uandike hayo uliyoandika. Ebu google basi ujue vizuri mkuu.
Endelea ku Google! Lakini nakushauri sana uangalie vipindi muhimu television za CNN, FOX NEWS , CBS, BBC, ALJAZEERA...Huko kuna senior correspondents and retired directors of the Bureau and the Agency wakitoa uchambuzi na maelezo ya kina ! Hasa panaptokea jambo duniani linalohusu intelligence!

Hear from the horse's mouth! You can even contribute in the discussions. Dont confine yourself to a narrow definition and functionality of those entities ! They are more than what Google portrays them ! Do you know Gen. McMaster for example? Usikariri ukidhani maisha yako Google tu ! Jiongeze...
 
Jitahidi ujue tofauti ya majukumu ya CIA na FBI, kwa nini hao unaowasikiliza unafikiri ndio wanatoa taarifa sahihi zaidi kuliko wanaoandika.
 
Mizungu ni mijizi pia
Ukiangalia ili mijizi ya Acacia ilivyotuibia na ikaendelea kuwa ngangari mpaka ilipoishiwa pumzi,siwaamini wazungu
 
Kwahiyo madudu ya mtu mmoja ndio uhitimishe CIA wapo kama huyo jamaa?

Fallacy of generalization.

Lumumba bongo zenu ni mashudu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndo Akili yako Ni mashudu kwa Maana umeshindwa kutambua hata nafsi iliyo tumiwa na pompeo. Ushaona Neno "WE" harafu bado unasema heti Kuna nafsi moja hapo Rudi English course ukapigwe msasa wa kingereza shudu wewe.
 
Mijitu ya CCM hovyo kabisa, na lichama lao useless Kama damu ya hedhi
Mkuu usiitukane kwa shombo hivyo damu ya hedhi. Hiyo ndo ilikufanya Hadi wewe ukawepo dunian na hiyo ndo imekufanya uitwe baba fulani.. harafu Leo kwa hasira za kijinga tu na Uchumia vyama ndo unakuja kuitukana damu ya hedhi kweli?.

Kuwa naheshima kwa wanawake akiwemo na mwanamke aliekuzaa pia.
 
Damu ya hedhi Ni useless, haitengenezi watoto
 
FBI hawahusiki na mambo ya nje ya USA, FBI ni home security, hivyo msaada wowote mtakaomba kama USA akikubali ni kazi ya CIA na siyo FBI!

Tunaongelea swala la kuchunguza CIA hawafanyi uchunguzi wowote wenyewe ni usalama wa taifa na kwa nje ya USA . Lakini hawana wataalamu wa uchunguzi. Kuna nchi nyingi zinaomba FBI msaada ni lazima waje kwa makubaliano. Naona wengi mnajichanganya.
 
Huyu Dada uwa anachemka sana mada zake.
Haya wahi Buku 7 na hivi juzi mlichangiwa pale Zanzibar.
 
FBI hawafanyi uchunguzi nje ya USA, FBI ni home security, hivyo kama mlitaka USA aje basi angetuma CIA na siyo FBI.

Tofauti kati ya CIA na FBI ndio hiyo, FBI ndani ya USA na CIA nje ya USA!
Mkuu inaelekea huelewi mambo. CIA ni kama usalama wa Taifa Tanzania. Wanafanya kazi zao underground.

FBI wanafanya kazi mpaka nje ya mipaka yao ... labda unachotaka kusema ni issues zinazohusiana na makosa ya sheria zao. Kawaulize akina Michel Platin na Sepp Blatter kama ile issue ya rushwa FIFA ilikuwa chini ya nani ...........!!?
 
Sio kweli haya uliyoyasema Mkuu, CIA ni SHIRIKA LA KIJASUSI linalofanya kazi kwa maslahi ya Marekani..

MFANO Serikali ya Marekani hawakumpenda Raisi fulani, Labda tuseme Magu, CIA Watafanya uongo, uzushi, uchonganishi mpaka Raisi husika aondoke madarakani..

FBI hawa ni WAPELELEZI WA POLISI wanaweza kufanya kazi katika jimbo lolote la Marekani, Unaujua Marekani kila jimbo lina sheria zake lakini ni Polisi wa Muungano wanaweza kuingilia jimbo lolote..

Kwa vile FBI wamebobea kwenye uchunguzi wa kipolisi hawa jamaa wanaweza kuitwa na kufanya kazi nje ya Marekani..
Wakati wa ugaidi ktk balozi za Marekani Nairobi na Dar es salaam 1998, FBI walikuja hapa Tanzania kufanya uchunguzi.
 
OK, sawa!
Kwanza tuwekane sawa; CIA hawafanyi kazi ya uchunguzi wa matukio ya kihalifu kama ya kushambuliwa kwa risasi kwa bwana Tundu Lissu
Chadema na wengineo wanataka CIA waletwe nchini kuchunguza waliomshambulia Tundu Lisu, wanasema Muzungu hadaganyi na kuita eti uchunguzi huru na hawana imani na watu wetu wa Tanzania, sasa huyo ni aliyekuwa Top Boss wa CIA Mike Pompeo akitupa mbili tatu zake kuhusu wanavyofanya kazi kama CIA, ...

I was the CIA director, we lied, we cheated, we stole, ... Mike Pompeo.

Barbosa,
Kwanza jambo moja inabidi lifahamike wazi kwamba CIA hawafanyi uchunguzi wa matukio ya kijinai kama ya kutekwa, mauaji, ubakaji au ujambazi, iwe huko kwao America,au nje ya America.
Wanaohusika na uchunguzi wa matukio ya kihalifu kama hayo huko America ni polisi ambao nao wakizidiwa wanaomba msaada kwa FBI ambayo ni taasisi bobezi kwa mambo hayo.
CIA ni taasisi ya kijasusi kama ilivyo MI6 ya Uingereza, au Mossad ya Israeli ,au FSB ya Russia,na au ilivyo Tiss hapa kwetu.
Kwa hiyo kama serikali ingeomba msaada wa kiuchunguzi wa matukio ya kijinai kutoka America, watakaokuja ni FBI, siyo CIA. Vivyo hivyo ikitokea serikali imeomba msaada wa kiuchunguzi toka Uingereza, watakao kuja kufanya kazi hiyo ni Scotland Yard, na siyo MI6.
Matokeo ya uchunguzi unaofanywa na taasisi hizi za aina ya Scotland yard na FBI au kama polisi wetu,ndiyo huo huja kutumika mahakamani. Na kwa vile matokeo ya kazi zao hizi za kiuchunguzi baadaye huja kutumika mahakamani, hivyo basi kazi nzima ya kiuchunguzi huwa ya kisayansi zaidi ili kupata ushahidi thabiti. Mathalan, kwa sasa kutokana na matumizi ya kiuchunguzi yanayohusisha vinasaba (DNA) yamerahisisha kuwakamata wahalifu wa ubakaji au hata wauaji na kutiwa hatiani bila ya shaka.
Ni kweli CIA na hata taasisi nyingine za kijasusi wanaweza kudanganya kama sehemu ya propaganda. Hata taasisi yetu ya kijasusi ya TISS inaweza kudanganya katika propaganda zake kwa maslahi ya nchi.
Lakini kama jeshi letu la polisi likasema sasa limeshindwa, na kwamba wakaomba msaada wa taasisi ya Scotland yard au FBI katika uchunguzi juu ya matukio ya kihalifu,au kama ulivyosema tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu ,taasisi hizo zikija hapa kufanya uchunguzi,zitafanya kazi kisayansi kwa sababu mwisho wa siku matokeo ya uchunguzi wao ndiyo yatakayotumika kwa ushahidi mahakamani.
Taasisi ya kiuchunguzi ikidanganya au kufanya propaganda, inashindaje kesi mahakamani? Hata kama CIA wangehusika na uchunguzi kama ulivyodhani mwanzo, unafikiri baada ya hapo wakisema wao wangekuwa na jukumu la kutueleza waliohusika tu na kisha sisi tukawakamata waliotajwa na kuwapeleka jela bila waliotajwa kujitetea mahakamani?
Sasa kama wanadanganya au kufanya propaganda katika uchunguzi wao, wanashindaje mahakamani?
Miaka ya 80 jengo la BOT,liliungua. Serikali baada ya muda kidogo tu ikaomba msaada wa Scotland Yard. Baada ya wiki 2 za uchunguzi,sababu ya moto ilijulikana.

Huko Kenya pia, baada ya kuuawa kwa Waziri wa mambo ya nje bwana Robert Ouko, serikali iliomba msaada wa Scotland yard,wakiongozwa na kachero John Troon. Wakiwa katikati ya uchunguzi, serikali ya Kenya iliwafukuza baada ya kugundua kuwa Nicholaus Biwott ambaye alikuwa mtendaji Ikulu na pia mpwa wa rais Moi, kwamba alionekana kuwa ni mmoja kati ya watu muhimu waliotakiwa kuhojiwa baada ya uchunguzi wa kimazingira, kuona, na kisayansi.
WACHUNGUZI WA NJE HAWAJI KUFANYA PROPAGANDA UKIWAHITAJI.
ILA UNA MOYO,MAANA ISIJE IKAONEKANA MUHALIFU AKAWA MWANAO.
 
Walichotuzidi wenzetu si tu akili, Bali ni u smart wao katika kuchakata mambo.

Unaweza hata hiyo kauli ya Pompeo inatolewa kimkakati Sana ila kwa kuwa hatupo smart tunaichukulia kirahisi kama Mtoa Mada anavyoainisha,
Kwamba Cia director anakiri ,waliiba, na kudanganya!! Na Mtoa Mada anakuja kuitoa huku kama reference ya bad conduct, bila hata kujiuliza waliiba nini na kudanganya nini,!!!

Pengine, Cia walidangaya maadui ili kufanikisha jambo la ki usalama? Au labda waliiba nyaraka zilizofanikisha jambo flani muhimu kwao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom