t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 6,367
- 14,752
Asante kwa maelezo mazuri,Kwanza tuwekane sawa; CIA hawafanyi kazi ya uchunguzi wa matukio ya kihalifu kama ya kushambuliwa kwa risasi kwa bwana Tundu Lissu
Barbosa,
Kwanza jambo moja inabidi lifahamike wazi kwamba CIA hawafanyi uchunguzi wa matukio ya kijinai kama ya kutekwa, mauaji, ubakaji au ujambazi, iwe huko kwao America,au nje ya America.
Wanaohusika na uchunguzi wa matukio ya kihalifu kama hayo huko America ni polisi ambao nao wakizidiwa wanaomba msaada kwa FBI ambayo ni taasisi bobezi kwa mambo hayo.
CIA ni taasisi ya kijasusi kama ilivyo MI6 ya Uingereza, au Mossad ya Israeli ,au FSB ya Russia,na au ilivyo Tiss hapa kwetu.
Kwa hiyo kama serikali ingeomba msaada wa kiuchunguzi wa matukio ya kijinai kutoka America, watakaokuja ni FBI, siyo CIA. Vivyo hivyo ikitokea serikali imeomba msaada wa kiuchunguzi toka Uingereza, watakao kuja kufanya kazi hiyo ni Scotland Yard, na siyo MI6.
Matokeo ya uchunguzi unaofanywa na taasisi hizi za aina ya Scotland yard na FBI au kama polisi wetu,ndiyo huo huja kutumika mahakamani. Na kwa vile matokeo ya kazi zao hizi za kiuchunguzi baadaye huja kutumika mahakamani, hivyo basi kazi nzima ya kiuchunguzi huwa ya kisayansi zaidi ili kupata ushahidi thabiti. Mathalan, kwa sasa kutokana na matumizi ya kiuchunguzi yanayohusisha vinasaba (DNA) yamerahisisha kuwakamata wahalifu wa ubakaji au hata wauaji na kutiwa hatiani bila ya shaka.
Ni kweli CIA na hata taasisi nyingine za kijasusi wanaweza kudanganya kama sehemu ya propaganda. Hata taasisi yetu ya kijasusi ya TISS inaweza kudanganya katika propaganda zake kwa maslahi ya nchi.
Lakini kama jeshi letu la polisi likasema sasa limeshindwa, na kwamba wakaomba msaada wa taasisi ya Scotland yard au FBI katika uchunguzi juu ya matukio ya kihalifu,au kama ulivyosema tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu ,taasisi hizo zikija hapa kufanya uchunguzi,zitafanya kazi kisayansi kwa sababu mwisho wa siku matokeo ya uchunguzi wao ndiyo yatakayotumika kwa ushahidi mahakamani.
Taasisi ya kiuchunguzi ikidanganya au kufanya propaganda, inashindaje kesi mahakamani? Hata kama CIA wangehusika na uchunguzi kama ulivyodhani mwanzo, unafikiri baada ya hapo wakisema wao wangekuwa na jukumu la kutueleza waliohusika tu na kisha sisi tukawakamata waliotajwa na kuwapeleka jela bila waliotajwa kujitetea mahakamani?
Sasa kama wanadanganya au kufanya propaganda katika uchunguzi wao, wanashindaje mahakamani?
Miaka ya 80 jengo la BOT,liliungua. Serikali baada ya muda kidogo tu ikaomba msaada wa Scotland Yard. Baada ya wiki 2 za uchunguzi,sababu ya moto ilijulikana.
Huko Kenya pia, baada ya kuuawa kwa Waziri wa mambo ya nje bwana Robert Ouko, serikali iliomba msaada wa Scotland yard,wakiongozwa na kachero John Troon. Wakiwa katikati ya uchunguzi, serikali ya Kenya iliwafukuza baada ya kugundua kuwa Nicholaus Biwott ambaye alikuwa mtendaji Ikulu na pia mpwa wa rais Moi, kwamba alionekana kuwa ni mmoja kati ya watu muhimu waliotakiwa kuhojiwa baada ya uchunguzi wa kimazingira, kuona, na kisayansi.
WACHUNGUZI WA NJE HAWAJI KUFANYA PROPAGANDA UKIWAHITAJI.
ILA UNA MOYO,MAANA ISIJE IKAONEKANA MUHALIFU AKAWA MWANAO.
Wenzetu linapokuja swala la investigation wapo vizuri Sana,
Nakumbuka bbc walimwelezea FBI director aliyekuja Kushughulika na shambulio la Nairobi, Alisema haikuwahi kuijua Kenya kiu jumla, na hata haikuwahi kusikia neno Nairobi,
Ila siku mbili baada ya jamaa KuingiaNairobi, tayari alikuwa amefanikisha kumkamata key suspect akiwa amelazwa hospitali Moja jijini hapo,
Na alikuwa, peke yake 'team solo'
Sent using Jamii Forums mobile app