Haya huchangia Mwanaume kuwa mchovu kitandani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya huchangia Mwanaume kuwa mchovu kitandani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Feb 27, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Kuna malalamiko mengi sana yamekuwa yakitolewa na wanawake na wengine kufikia kuvunja ndoa au mahusiano kwa sababu tu wanaume wao wameshuka kiwango au ham imeisha kabisa ya tendo.

  Lawama hizo wamekuwa wakiwatupia wanaume bila kuangalia uhalisia wake.

  Ukweli ni kuwa wanawake wenyewe ndo wamekua chanzo kikubwa cia tatizo hili.

  Sababu zifuatazo kwa ufaham wangu ndo zinasababisha:

  UCHAFU:
  Wanawake siku hizi wanashindwa kujifanyia usafi ipasavyo miili yao kitu kinachosababisha mwanaume kukereka na hamu kwisha.

  KAZI:
  Wanawake wa siku hizi inafahamika kuwa wanafanya kazi,mwanamke anarudi kazini na uchovu, stress, katukanwa na bosi wake, amepata loss, ametongozwa na boss na kutishiwa kufukuzwa kazi kama atamkataa, amesikia fununu za ridandasi n.k,mwanamke kama huyu hawezi kuwa na ndoa imara.

  KUTOKUWA MUWAZI:
  Hili ni tatizo kubwa, wanawake hawapo wazi kama hawajatosheka kitandani hivyo wanaenda kulalamika nje na pindi mume apatapo taarifa hunyong'onyea kwa sababu anajua watu wanajua mkewe hamtoshelezi.

  UFUJAJI:
  Mwanamke mfujaji mume wake lazima atakuwa na tatizo hili.

  LUGHA CHAFU:
  Lugha ni nguzo nyingine inayochangia tatizo hii, unakuta mume maumbile yake madogo, badala mwanamke kutumia lugha nzuri anatumia lugha za kashfa kitu kinachomfanya mume kupoteza kujiamini.

  USHIRIKIANO:
  Wakati wa tendo unakuta mwanaume anashughulika lakini mwanamke amelala kama hakuna kinachoendelea hali hii inakera sana!...

  Sababu ni nyingi sana ila nasema wanawake wabadilike wao ndio nguzo muhimu sana hapa. Sisemi wanaume hawana lawama wanazo hasa, ULEVI, UVUTAJI SIGARA na KUFANYA KAZI KUPINDUKIA humfanya awe mchovu kitandani, lakini mwanamke anaplay part kubwa kwenye tatizo hili! Ladies mpo hapo?

  NAWATAKIENI NDOA/MAHUSIANO IMARA!
   
 2. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  nangoja waje watatuambia.
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tuhuma za uchafu sina hakika nazo....

  Ila hayo mengine nayakubali......

  Mwanamume anaweza kuwasha gari ila mwenye jukumu la kuliendesha hadi mwisho wa safari ni mwanamke...Jukumu la mwanamume ni kuhakikisha halikwami kwenye matope!!

  I wish they knew!!

  Babu DC!!
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii maneno, inaweza leta tafrani hapa................
  Hebu ngojeni Wabeijing watie timu.
   
 5. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  za siku DC? mkuu umeamua kuunga tela kwenye vagi la Eiyer vs wadada? Wakianza kurusha makombora? Mkuu mimi najiweka pembeni!
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Usijali ukweli wataukubali tu!
   
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Babu DC,uchafu mimi ni shahidi,niliwahi kuwa na binti mchafu,nilikuwa natumia hekima sana kumweleza ili asijifikirie vibaya lakini hakuwa akinielewa,nashukuru Mungu kilichofanya tusitishe uhusiano ni jambo jingine kabisa!
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Umekutana na huyo binti mmoja tu ambaye alikuwa mchafu au katika sample yako, zaidi ya 90% walikuwa wachafu?

  Babu DC!!
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako bashaija,usihofu nimevaa helmet,na kila silaha kukabiliana nao!
   
 10. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ...oooh! Kumbe unyago ulikuwa muhimu kuliko "kitchen part" ee.
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  wamekimbiaa
   
 12. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  here we go again... kila couple ijifanyie tathmini yenyewe na kuchukua hatua
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Wakora waitu....Babu DC ni mzima kabisa,

  Babu ni fair kwa wajukuu wote...Ameona na kushiriki mengi sana toka enzi hizo za 1947...neno analotoa si lake pekee bali ni mkusanyiko wa uzoefu kutoka wa wazee wenzake kibao...bahati mbaya wengine walisharudisha kadi kwa Mwenye haki!!

  Wadada (pamoja na nyie vijana) lazima waelewe tu kwamba haya mambo ya MMU hayafanywi na mtu mmoja...bali timu ya watu 2 ambapo mmoja akifanya uzembe, kibarua kinakwamia njiani!!

  Babu DC!!
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Babu DC,asante kwa swali zuri,sio kweli kuwa wote niliokuwa nao wapo hivyo,ila nina marafiki nasoma visa mbalimbali na pia nakutana na wadada hawa kila siku,vitu kama kutoa harufu mdomoni na kwapani ni vitu vya kawaida,wanaume nao wanamatatizo hayo ila mwanamke na mwanaume ni tofauti!
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Watakuja tu usijali!
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Tathmini inaweza kufanyika lakini siku za karibuni, kila mtu amekuwa akimrushia mwenzake madongo na kulalamika!!

  Mie nawaeleza, kama kuna kitu kimeshindikana basi wote wamefeli mtihani kama yule binti wa kaka mkubwa!!

  Tukae chini na kujipanga upya...vinginevyo............!!!


  Babu DC!!
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  duh, ntamwachisha kazi mke wangu ili awe fit usiku.
  Ila kama unapenda kiuno panga boy si bora kuifunga kwenye mota ikazungushwa hadi basi.

  Anyway, kuna ka ukweli hapo.
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Yes!Vitu vingi vya leo ni vya hovyo!
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kitchen party hakuna kitu
  ni kutupa hela tu
  huwezi fundishwa tabia kwa saa 3

   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,667
  Trophy Points: 280
  Kongosho bana,kwa hiyo post yako hapo juu,jiandae kukwepa ngumi!
   
Loading...