Haya hapa matokeo ya darasa la saba 2019, Wanafunzi kumi bora kitaifa watoka kanda ya ziwa

khamis kilo

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,049
1,192
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambako mikoa ya kanda ya ziwa imeonekana kuongoza kwa kushika nafasi zote 10 bora kwa wavulana.

Katika matokeo hayo yaliotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya wavulana waliofanya vizuri zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Matokeo haya hapa https://results.necta.go.tz/results/2019/psle/psle.htm
 
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambako mikoa ya kanda ya ziwa imeonekana kuongoza kwa kushika nafasi zote 10 bora kwa wavulana.

Katika matokeo hayo yaliotangazwa leo Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya wavulana waliofanya vizuri zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.]

Shule 10 BORA zote zimetokea Kanda ya Ziwa, na hao WANAFUNZI ‘bora’ wametokea huko.... ila Kimkoa Dar es Salaam ndio KINARA ikifuatiwa na...... wala sio MIKOA kutoka Kanda ya Ziwa iliyoongoza.

Weka vizuri kumbukumbu zako.
 
Pamoja na matokeo chanya kanda ya ziwa haina hata Chuo Kikuu chenye Campus inayoeleweka.

Inaboa
 
Inawezekana samaki wa Ziwa victoria wana impact kwenye ubongo wanapotumiwa katika lishe!! ...vinginevyo hali ikiwa tofauti baada ya miaka saba ijayo, tutaelewa kuwa elimu ilitawaliwa na kujimwambafai.
 
Naona kanda ya ziwa ni mwendo wa kunimwambafai.
Nahisi Afisa Elimu mkoa, mkuu wa mkoa, nk wanataka kuteuliwa.
 
Wakitokea Kanda ile nyingine watu wanajifaragua humu ila wakitokea kwingine inakuwa siyo bure!!

Mwaka jana nako Kusini walifanya vizuri nadhani Advance basi wale jamaa wakajaza mate kwenye ile mijadala.

Aliyesema,Fahari ndiye mama wa ujinga hakukosea.
 
Inawezekana samaki wa Ziwa victoria wana impact kwenye ubongo wanapotumiwa katika lishe!! ...vinginevyo hali ikiwa tofauti baada ya miaka saba ijayo, tutaelewa kuwa elimu ilitawaliwa na kujimwambafai.
ni kweli kabisa samaki ni moja ya chakula kinachoongeza akili kwa utafiti wangu
 
Acheni masihara kanda ya ziwa ina wanafunzi vichwa nyie

Nimesoma shule tofauti ila kanda ya ziwa wanafunzi wa kule

Nimewavulia kofia,ina akili kama imetunga pepa na mwalimu
 
Back
Top Bottom