HAYA FISADI WATOTO Haoo...

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
49,282
19,617
Mtoto wa Mbunge Keenja afutiwa dhamana

Habari Zinazoshabihiana
• Baada ya bintiye kunyimwa dhamana...Keenja aingilia kati, yatolewa 27.03.2008 [Soma]
• 'Mtoto' wa Mbunge kizimbani akidaiwa kujaribu kuua 14.11.2007 [Soma]
• Kichaa aiba mtoto na kumnyonyesha 15.09.2007 [Soma]

Na Grace Michael

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemfutia dhamana mtoto wa Mbunge wa Ubungo, Bw. Charles Keenja, Bibi Eliaisa, baada ya kukiuka masharti ya dhamana aliyokuwa amepewa na mahakama.

Dhamana hiyo ilifutwa jana mahakamani hapo na Hakimu Mkazi, Bibi Benardetha Beda, baada ya mshitakiwa huyo kutoonekana mahakamani kwa kipindi kirefu bila ya Mahakama kuwa na taarifa yoyote.

Bibi Keenja anakabiliwa na kesi ya wizi wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 300, ambapo katika kesi hiyo, wapo pia washitakiwa wengine wawili ambao ni Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Tabora, Bw. Damas Ngoiya (47) na Bw. Josephat Leema (48), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Manyoni Auctioneer Limited.

Mshitakiwa huyo awali aliandika barua akiiomba mahakama imruhusu kwenda nje ya nchi kwa matibabu Septemba mwaka jana kwa miezi mitatu, lakini aliondoka kabla ya mahakama kutoa kibali hicho.

Muda alioomba ulikuwa unamalizika Desemba mwaka jana ingawa hakuonekana mahakamani hapo wakati kesi ilipokuwa ikitajwa, hivyo baada ya kuonekana jana, Mahakama ilimfutia dhamana na kurudishwa rumande mpaka MEI 15 mwaka huu kesi itakapotajwa.

Katika kesi hiyo, washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa katika muda ambao haukujulikana, wakiwa Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda makosa ya wizi wa vitu mbalimbali mali ya raia wa China, Bibi Li Jinglan vya thamani ya sh. 333,300,000.

Walidaiwa, kuwa Mei 9 mwaka jana Kinondoni, waliingia kwenye nyumba ya NHC ambayo mpangaji wake ni Bi. Jinglan wakiwa na nia ya kuiba.

Washitakiwa hao walidaiwa kuwa baada ya kuingia waliiba mabandari 74 ya nguo, kompyuta, dola za Marekani, hereni za dhahabu, kamera na vitu mbalimbali mali ya mpangaji huyo.


hawa naona wameamua kuiba waziwazi baba zao wakitumia makaratasi

MUNGU TUOKOE JAMANI TUSAMEHE DHAMBI ZETU MBONA HIVI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom