Hawatibiwi hospitali zetu,hawasomeshi shule zetu, hawajui machungu ya kukosa umeme, je watatusaidia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawatibiwi hospitali zetu,hawasomeshi shule zetu, hawajui machungu ya kukosa umeme, je watatusaidia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Mar 14, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Uingereza kuna waziri wa elimu alilazimishwa kujiuzuru baada ya kugundulika kuwa watoto wake wote walikuwa wanasoma shule za binafsi huku yeye akiliambia taifa kuwa hali ya elimu kwenye shule za umma ilikuwa ni nzuri kuliko wapinzani walivyokuwa wanadai.

  Kwa wenzetu ukiwa mtumishi wa umma (hasa wakisiasa kama waziri) na ukakwepa kutumia huduma wanazotumia wananchi wengine ni tiketi inayokuondolea uhalali wa kuendelea kushika huo wadhifa, hapa kwetu ukipata uwaziri unasahau shida kwa kupata huduma kwenye hospitali za binafsi (nje ya nchi), kusomesha watoto wako kwenye shule za binafsi zinatoa huduma bora (au hata nje ya nchi), n.k,.nk.

  Taifa likiwa limegubikwa na mizengwe isiyoisha kwenye sekta ya nishati viongozi wetu hawajui hata hali ilivyo pale mtu unapokosa umeme (wao hawana mgao wa umeme na wana majenerata pale unapokatika), kwa maana hiyo hawana hata haraka ya kuona kuwa changamoto ya kukosa umeme inapatiwa ufumbuzi wa haraka na wa kudumu wao wanachoangalia ni namna gani watajaza mifuko yao kwa kuingia mikataba ya kilaghai.

  Je tutafika?
   
 2. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tutafikaje wakati hujasema nini kifanyike? Kusomesha watoto nje ya nchi siyo shida, kuwa na jenereta nyumabi siyo shida kinachihitajika ni uadilifu. Mimi nafahamu mawaziri kibao ambao watoto wao wanasoma hapa nchi akiwemo mtoto wa waziri wa Elimu anayesoma Mzumbe hata watoto wa rais wengi wamesoma hapa nchini kwa ngazi zote. Sidhani kama kutokuwa na jenereta nyumbani, kutokusomesha watoto nje ya nchi ndiyo kipimo cha kiongozi kuwa muadilifu au kutokuwa fisadi au kujua matatizo wa wananchi. Matatizo yetu hapa nchini yanaletwa na wanasiasa wote bila kujali chama, mwenye uwezo na asiye na uwezo kila kitu wanafanya unprofessional ni maslahi ya chama na maslahi yangu basi.
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mabulangati lazima huwe mkweli, hoja iliyotolewa hapa ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo mtindo wakupiga siasa katika utoaji huduma muimu; chukua hili suala la elimu, ukitathmini kauli na vitendo vya viongozi wetu unaona dhahiri kuwa wanalenga katika kuwapotosha watu wa kawaida ya kuwa kupata elimu ya sekondari ni sawa nakupanda vyumba. Ndiyo maana wanadiriki kuandikisha shule za sekondari zenye mwalimu mmoja ambaye wakati huo huo ni mwalimu mkuu. Ni kiongozi gani anaweza kusomesha mtoto wake kwenye shule hizo? Katika kuendeleza ulaghai wao walifuta mtihani wa kidato cha pili ili kuwezesha wanafunzi walioko kwenye shule za sekondari kwa jina waweze kuendelea hadi kidato cha nne. Kila mtu alijua ya kuwa wengi wataanguka kwenye mtihani wa kidato hicho. Baada ya hilo kutokea bila aibu serikali inajifanya kushangaa na kunza kuteua tume kuchunguza jambo hilo.
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Ridhwani alisoma Uingereza kama sikosei. Khalifa amesoma Trust St. Patrick ya Arusha ambayo ada yake ni mamilioni kadhaa....
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wanaishi maisha ya ughaibuni kwa hiyo tukilalamikia huduma duni hawaelewi maana yake nini, wanaona kama tunaigiza vile. Kitu usichokijua ni usiku wa giza!
   
Loading...