Hawara wa John Edwards ahojiwa na CNN leo kuhusu kitabu alichoandika cha maisha yake ya u mistress

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,309
8,369
Nilishawahi sikia juu juu kuhusu kashfa iliyomuangusha John Edwards kisiasa huko Marekani. Leo nikiwa nimewasha TV yangu huku napiga kazi nimejikuta navutiwa kusikiliza mahojiano kati ya huyu hawara Riele Hunter na Piers Morgan wa CNN; ingawa sikuweza kufuatilia mahojiano yote kwa kuwa nilikuwa nina safari haya ndio niliyoyapata:

Kwanza kabisa huyu dada ametunga kitabu kuhusu maisha yake ya kuwa mistress wa mwanasiasa huyu mahiri (John Edwards) kitabu ambacho kimeonekana kuwaudhi wamarekani wengi; kwani anasema ameandika ili mwanae alomzaa na Edwards akikua asome. Lol. Nilikuwa nafuatilia Yahoo wengi wana campaign watu wasikinunue hicho kitabu ili kumkomesha yeye na publisher wake. Na hicho kitabu ndicho kimewavutia CNN kufanya nae mahojiano

Cha kushangaza kila swali alilokuwa anaulizwa na Morgan alikuwa anakwepa kujibu kama anaona soo wakati ni ndani ya yaliyoandikwa kitabuni; mara ooh umetafsiri out of context (sijuhi kiswahili chake) ila ni kama anamwambia mtangazaji inabidi asome zaidi si ku pick mistrari fulani fulani ili aweze kuelewa alikuwa anamaanisha nini.

Kali zaidi mtangazaji anamuuliza kwa nini kwenye kitabu ametumia maneno ya kejeli na mabaya kumuelezea (describing) mke wa Edwards ambaye kwa sasa ni marehemu (amekufa kwa kansa). Akamuuliza mlishawahi kukutana au ulikuwa unamjua? Eti tulikutana mara moja tu; ila Edwards alikuwa ananisimulia kuhusu mkewe.

Morgan: Kwa nini ulikuwa unaamini unachoambiwa na Edwards wakati ni obvious hakuna mwanaume atakaye msema mkewe vizuri kwa hawara.
Hunter: Sijuhi kama nilikuwa namwamini au la
Morgan: Kwa nini ulirecord mkanda wa ngono na Edwards mkiwa Uganda? Ulikuwa wa nini?
Hunter: Sijuhi (mkanda wenyewe umeshaliki hivyo)
Morgan: Kwa nini ulikuwa hautumii dawa za kuzuia mimba na unajua Edwards alikuwa mume wa mtu
Hunters: Sijuhi
Morgan: Mke wa Edwards angekuwa hai leo ungemuomba msamaha
Hunter: Yes
Morgani: Unajisikiaje kuharibu political career ya mwanasiasa ambaye wamarekani wengi walitegemea angekuwa Rais
Hunter: Sijutii uhusiano wangu na Edwards kwani nilimfanya awe na furaha maishani
Morgani: Umeandika kuwa wewe ni mzuri kwenye sex (not sure if these were exact words) unataka kutuambia Edwards alikuchukua kwa sababu ya sex na si love.
Hunter: Jibu alilotoa halikueleweka ni kama alitaka kukana alichoandika.

Kwa ufupi the lady is insane; maana hakuna hata swali moja alojibu kwa uwazi wakati ameamua kuandika kitabu cha uchafu wake

Haya na mahawara wa Tz; hasa mnaotembea na vigogo; mwenzenu amejigundulia ujasiriamali wa kuuza siri za mahusiano yao kwa njia ya kitabu. Wanaume mtakomajeeeee!!! Wema alishaanza kuonyesha nia ya kutoa list ya alotembea nao (kama ni kweli maana nilisoam udaku).
 
if you are somebody famous
women get a life by sleeping with you...

she is now a qualified author because of sleeping with the guy
 
Me too. Lol.

Tena kwenye hicho kitabu huyu hawara anasema Edwards alikuwa na vimada wengi tu, yeye alikuwa just one of them. Sijuhi kwa nini Edwards aliamua kumwambia wazi kuwa hayuko peke yake. Alichowazidi kete wenzie ni kuamua kuzaa.

Nachosikitika ni kuwa na roho ya tamaa ya pesa kiasi cha kuanika uchafu wake adharani in the name of their daughter; mtoto amekosa nini mpaka amdhalilishe hivyo.


I thought white men don't cheat...
 
Huyu dada yuko funny; ameulizwa kama anajua maana ya Ndoa; anasema alishawahi kuolewa na amedumu kwenye ndoa yake for 9 years kabla hawajaachana na mumewe.

Kaulizwa why waliachana?

Anasema infidelity. Sasa sikusikia akifafanua nani alimchiti nani.
 
Kweli ameshakuwa maarufu. Japokuwa watu wana hasira nae na wanasema wagomee kitabu ili asipate ela maana inaonyesha anapenda ela sana; nina hakika hicho kitabu kitauzwa saaana;

Mimi mwenyewe naweza kukinunua si kwa kuwa amenifurahisha ila ni kitu cha hajabu na nataka kujua alichoandika.

if you are somebody famous
women get a life by sleeping with you...

she is now a qualified author because of sleeping with the guy
 
Back
Top Bottom