Hawara amuua mwenye mume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawara amuua mwenye mume

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 29, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWANAMKE mkazi wa Ronsoti mjini Tarime mkoani Mara, Debora James (30), anatuhumiwa kumuua mwenzake, Teresia Nago, kwa kumchoma kisu katika mauaji yanayohusisha kugombea mwanamume.

  Kwa mujibu wa Polisi, Teresia aliuawa jana saa 4.30 asubuhi Bomani mjini Tarime, baada ya kuchomwa visu viwili tumboni na kifuani na mgomvi wake huyo.

  Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rorya/Tarime, Sebastian Zakaria, alisema Debora alikuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano na mume wa Teresia, John Nago ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

  Kaimu Kamanda alisema, wanawake hao wawili walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na vurugu wakigombea mwanamume huyo.

  Alisema, jana Teresia na Debora walikwenda kusuluhishwa na mzee wa Kanisa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja eneo la Bomani.

  Lakini wakiwa Bomani, kulitokea vurugu na Debora ambaye alikuwa na kisu alimshambulia Teresia kwa kumchoma kisu kifuani karibu na moyo na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo, baada ya kutokwa damu nyingi naye akajichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa lengo la kujimaliza.

  Kamanda Zakaria alisema Debora amelazwa katika hospitali ya wilaya mjini hapa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kujijeruhi.
   
 2. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  duh! pole zao. Na Mungu awarehemu. Inakuwaje haya matukio ya wapenzi kuuwana yanazidi ?
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  idadi ya wanawake wavuta bangi inaongezeka
   
 4. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siku hizi bangi imekuwa kama pipi kifua, naskia hata bungeni tunao wavutaji hodari wa hii kitu
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  nilidhani idadi ya wanaume wakware imeongezeka!ila na sie wanawake huwa tuna akili za kuku,why on earth wld u kill someone for lov,ama kujiua? kuna watu wamefiwa na wenzi wao ambao waliwaonesha upendo na kuwajali,seuze ambaye haoneshi hata kujali! he is nt worth even a blink of my eye,kha!
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Jamani nini kinachogombewa hasa, du ona sasa. Hii yote ni upungufu wa kufikiri.
   
 7. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  wakurya bwana, wanauana kwa ajili ya mkoyonga????
  Lakini kwao kuua ni ujiko
   
 8. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mh.. pole kwa wafiwa.
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  yaani we acha tu!
   
 10. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  ni wale wanaorap sana nini!? khaaa asa wakipga msuba mjengoni c kunasku watazchapa kav kav?
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  ase is true it seems hilo janadume lilishindwa kuchagua liache yupi?is not an issue to fight for someone as dishonest as this shem on him loool,af msibani atalia huyooo kama ndama
   
 12. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  pole bwana harusi sasa umewakosa wote . mmoja jela mwingine kaburini!umefaidi nini hapo na nafsi itakusuta mpaka mwisho wako
   
 13. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Bungeni tena!!!!Nani anapuliza wida tena pale mjengoni?
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  tena kule kuna mchanganyiko wa hatari sana...
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  maisha kweli yamebadilika, cku hizi unaenda kusuluhishwa na hawara wa mumeo, khaa...RIP mdada.
   
Loading...