kambiko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 354
- 304
Usifananishe Serikali Na Wakina Gwajima Au Tundulisu.Serikali ikitaka Watu wachanje Watachanja kwa Lazima .Ishu Ni Kwamba Mpk Sasa Hakuna Amri Yakulazimisha watu Kuchanja.Tanzania ni moja ya nchi ambayo ukidhani wananchi wake wengi wanachokisema ndicho watakitenda basi utakuwa unajidanganya na nafasi yako!
Historia nchini imeonyesha mara zote wanaodhani wana watu nyuma yao hujikuta peke yao!
Sio muda mrefu aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu alijikuta “peke yake” baada ya kuitisha maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020. Hii ilikuja baada ya kuamini huku akisaidiwa na Sheikh Ponda na “Askofu” Mwamakula kuwa kuna kundi kubwa la watu nyuma yake ambalo aliliapisha wakati wa kampeni ili lihakikishe kura haziibwi na kama zitaibwa litaandamana nchi nzima pale atakapoitisha maandamano.
Uchaguzi Mkuu ulifanyika na baada ya matokeo kuanza kutangazwa, Tundu Lissu aliyakataa na kuitisha maandamano nchi nzima akiamini lile kundi lililokula kiapo kutoka kwa Sheikh Ponda na “Askofu” Mwamakula litajitokeza. Alichokishuhudia hakuamini! Mengine ni historia!
Kwa kiwango kikubwa ni kundi hili hili la Watanzania kwa sasa ukilisikia linampinga Askofu Gwajima kuhusiana na mtazamo wake wa chanjo za korona unaweza kudhani linachokisema ndicho linachokitenda!
Mtu anapinga hoja za Askofu Gwajima kuhusiana na chanjo za korona lakini ukimwambia aende kuchanja anakuambia hawezi kuchanja kwa sababu zile zile anazozitoa Askofu Gwajima!
Serikali nayo imejikuta katika hali kama iliyomtokea Tundu Lissu baada ya kusikiliza kelele za watu ambao ilidhani watajitokeza kwa mamilioni kwenda kupata chanjo na matokeo yake mpaka sasa hata laki nne hawajajitokeza.
Serikali imeingia “gharama” ya kuingiza chanjo za watu milioni moja na nusu ikidhani ina watu nyuma yake na matokeo yake ni chanjo nyingi zinaenda kupita muda wa matumizi (expire date) bila kutumiwa hasa ikichukuliwa kuwa chanjo zinaharibika baada ya miezi minne.
Ukichunguza utagundua kwa sasa watu wanaoenda kupata chanjo nchini wanafanya hivyo kwa sababu wanataka kusafiri nje ya nchi kwa vile ni takwa la kisheria na sio kwa sababu ni muhimu katika afya zao.
Siwezi kushangaa hata wale wabunge waliokuwa wanamshambulia Askofu Gwajima bungeni kuhusiana na hoja zake za chanjo ya korona kuna baadhi wanaweza wakawa hawajapata chanjo ya korona kwa sababu zile zile za hoja za Gwajima!
Unafiki nchini umekuwa kama ni sehemu ya maisha!