Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,836
Katika kampeni nzima Chama cha Mapinduzi hakikuahidi mabadiliko yoyote makubwa aidha ya mfumo wa kisiasa, miundombinu ya utendaji au hata mabadiliko ya kuona haja ya kufanya mageuzi makubwa ya kiutendaji ili kujenga mazingira bora ya kisiasa, kiuchumi na kiuwajibikaji. Ukilinganisha na vyama vingine hasa Chadema CCM haikuahidi kubadili muundo wa taasisi zake n.k Iliahidi kuendelea na kile kiliichopo kwa sababu inakubalika na wananchi.
Baada ya uchaguzi watu wameshikilia pumzi zao wakisubiri kuona kama kuna mabadiliko yoyote na wanaamini litakapotangazwa baraza la mawaziri basi ndio ishara ya wapi tunakwenda itaonekana. Lakini nyuma ya hilo ni kuwa yumkini serikali ijayo itasimamia mabadiliko muhimu. Lakini hawakuahidi mabadiliko!
Kama ni kweli (na ninaamini ndivyo) watu wana msingi gani wa kusubiri kwa hamu hotuba ya Rais Bungeni au baraza la Mawaziri jipya? Hivi serikali ikirudi na sura mpya lakini mwelekeo ule ule itawashangaza? Je ikija serikali mpya na semina mpya ya Ngurdoto na ziara za kila wizara kuwapa maelekezo itawapa tumaini?
Labda watu wapunguze matarajio yao (lower expectations) wasije wakaumizwa sana kwa kuona kile wanachohofia ndicho kinatokea. Watu wawe tayari kukumbatia na kukubali serikali inayokuja kwa misingi ya kuwa ni mwendelezo tu wa serikali iliyopita na wasitarajie mabadiliko makubwa kwenye baraza la mawaziri wala kwenye utendaji wake. Yaani, kile kilichotokea miaka mitano iliyopita, ndicho kitatokea miaka mitano ijayo na kwa mfuatano huo huo ndicho kitatokea miaka mitano baada ya 2015 endapo watu wale wale watachaguliwa.
Kwa maneno mengine... DON'T EXPECT CHANGE, YOU WILL BE DISAPPOINTED. Tarajia kile kile na tuendelee kuombea na kudumisha amani, umoja, utulivu na ushirikiano kati ya walioshiba na wenye njaa!