Hawa Wendazake (Marehemu) haya maneno yetu huwa yanasaidia kweli?

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
1,694
3,981
"Roho yake iwekwe mahali pema peponi"

Kama unamuamini Mungu. Je haya maneno humsaidia Mwendazake (Marehemu)? Kama yanamsaidia basi kuna haja gani ya mtu kuhangaika kutenda mema ilhali ukifa wakawepo mapadre,wachungaji,maaskofu,masheikh,maimamu wengi wakakuombea basi ile hukmu yako yaghairishwa.

Unakuwa umeombewa ghofilo. (msamaha) je inawezekana kabisa mpaka mtu anakufa Mungu hajapanga au hajui pa kumweka mhusika? Hivyo akishakufa watu mkamwombea anawekwa mahali pema?

Kama ni hivyo nadhani wachache sana wataenda Motoni.labda wale ambao walikuwa majambazi au wauaji. Ila kama ni hizi dhambi zetu common za Uzinzi, Ulevi, Uongo, Husda, Uasherati, Wizi, Ufisadi, Uchoyo, Chuki na Mauaji ya Siri basi nadhani hizi watu wataenda tu mahali pema. Maana hawa huwa wanaombewa sana. Na hasa kama walikuwa na mkwanja ibada huwa zinakuwa ndefu na zenye pambo nying nyingi na sifa za Mwendazake.

Otherwise mimi naona huwa ni usanii tu. Mtu mpaka amekufa kama hakutubu sisi hatuwezi batilisha ukaazi wa Roho yake. Alipaswa awe mwema akiwa hai.
 
1. RIP
2. Apumzike kwa amani
3. Ilazwe pema peponi
4. Tangulia tunakufuata
5. Nenda!
6. Umemaliza mwendo
7. Mungu kakupenda zaida
8. Tutakutana
9. Kamsalimie fulani & fulani huko
10. Umetuachia machungu
11. Ungetuaga\Hatahukutuaga
 
Hapana ni hulka ya sisi binadamu kusalimiana,kutakiana heri,kupeana pole kwenye matatizo ,kupongezana ,kwahiyo kumtamkia mwendazake maneno kama apumzike kwa amani ni kitu kizuri na kinaleta hata kiamani cha juujuu,maisha ni safari na mwendazake ana haki zote za kutakiwa heri ya anapokwenda...ndio ubinadamu huo au utu.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom