Hawa wazungu nchini wanatoa wapi hii jeuri?

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
345
100
Kumekuwa na unyanyasaji wa wananchi katika ardhi yao huku viongozi wakifumbia macho mambo haya.
Jana ITV nimeona wananchi wakifukuzwa kwenye mashamba yao walipozaliwa wakiambiwa wampishe mwekezaji, hivi mimi mTanzania naweza kwenda Africa ya kusini, au Ulaya na kufukuza watu sehemu yao kisa nimekwenda kuwekeza? Wafanyakazi kwenye makampuni ya wazungu wananyanyasika, wengi permit ni fake, uhamiaji wanakwenda kuchukua rushwa siku hadi siku, nini kifanyike ili wananchi tunufaike na matunda ya nchi yetu?
Mheshimiwa rais Magufuli, kuna sehemu unahujumiwa na watendaji wako, wahamiaji ni wengi sana wasio na vibali na tunawajua na tupo tayari kutoa ushirikiano
Mh Mwigulu Nchemba, tunahitaji muongozo wako kuhusu hili
Tufike mahali tukomeshe ukoloni mamboleo
 
Tatizo ni umasikini wetu na kua na viongozi wasiokua na hofu ya mungu/Maadili.
 
Ubaguzi sio mzuri dada….acha hizo
 
Hii kauli kuwa rais anahujumiwa huwa siielewi kabisa ila wakifanya kazi nzuri anayesifiwa ni rais, watanzania acheni unafiki let's call spade a spade not big spoon!
 
Samahani da Kitty Galore !!
Umeandika kwa jazba na hasira zako... Ujue Nchi hii inaendeshwa kwa sheria na katiba ndiyo dira ya Serikali....!!
Hakuna mtu anakuja na fukuza kinyamela au Mtu afanye kazi nchini bila ruhusa maalumu(permits,nknk) Labda hao wanaovuka mipaka kutoka nchi jirani!!

Halafu siyo kila mzungu ni mgenii humu nchini ..ujue wapo wazungu waliyopo kabla hata ya kupata Uhuru wa nchi !! na pia wazungu wengi walishika ngazi za juu na Uongozi/uWaziri.....
USISAHAU:- kuwa kuna kipindi maRais wa JMT waliienda kuwaomba hao wazungu (wawekezaji waje kuwekeza) warudi kufanya biashara hapa Tanzania.....

Soko huria.. kazana Ushindani ktk maisha hainaga Nchi yetu ooh sijui wazawaa.. !!
 
Sasa hapo mzungu ana kosa gani???????

Yeye ni mwekezaji kafuata taratibu zote za kisheria na kapatiwa ardhi ya kuwekeza ,unachomlaumu mzungu ni kitu gani

Nendeni kwa mkuu wa wilaya muelezeni ,huyo mzungu from no where hawezi kujiamulia lzm alifuata taratibu na akapatiwa

Mkuu wa wilaya atakuwa na majibu yenu

Permit fake ,ukipelekwa mahakamani ujibu hiyo tuhuma utatoa ushahidi au ndio kama yule jamaa aliyemzushia mwamunyange kawekewa sumu, kapandishwa kizimbani anatia huruma na kuomba huruma ya waTanzania..
 
Tupewe namna ya kuwakilisha kero zetu na serikali ifuatilie, sisi ndio tunaoishi nao na tunawajua
 
Mzungu ni nani? Mzungu ni binadamu aliefanikiwa katika mbinu za exploitative relationships. Hamna tofauti na mtu anaemlisha ng'ombe majani na pumba kisha anamkamu maziwa ya kutosha, waafrika ni kama ng'ombe wa maziwa kwa wazungu. Kama ng'ombe aliavyo kwa uchungu akinyimwa majani na huku amefungwa kamba shingoni anashindwa kwenda kujitafutia mwenyewe, ndivyo ilivyo kwa waafrika tukinyimwa misaada huku tunazuiwa kutengeneza uwezo wa kutumia rasilimali zetu wenyewe ili tuendelee. Tafakari, chukua hatua.
 
Leo nadhani mmesikia Rais akiongelea hili swala la migodi Shinyanga.
Tufike mahali tutangulize uzalendo kwanza.
Nasisitiza, wananchi tupewe namna ya kuwakilisha huu unyanyasaji, nasi tutoe ushirikiano
 
Tatizo ni umasikini wetu na kua na viongozi wasiokua na hofu ya mungu/Maadili.
Tatizo si umasikini wetu ila tunashindwa kulinda haki zetu, kama tungezisimamia na kuzilinda haki zetu kama mataifa mengine yafanyavyo huo upuuuzi usingetokea aslani!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom