Hawa wazee wa tigo wana kazi gani( polisi maendensha piki piki) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa wazee wa tigo wana kazi gani( polisi maendensha piki piki)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KAPECHA, Apr 24, 2009.

 1. K

  KAPECHA Member

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wadanganyika wenzangu

  Kwa mara ya kwanza napenda kujitokeza rasmi na kuweza kutoa maduku duku mengi huwezi kuamini kuwa kuna kampuni linaweza kuweka mpaka dhahabu zenye samani ya dola milioni tatu kwa ajili ya kuuza wakati makazi wa kipawa wanalala kwenye shule.

  Naomba sasa nianze na mada ya hapo juu nilikuwa nimesimama kando mwa barabara ya nyerere maeneo ya tazara mataa nikisubiri taa ziruhusu ili niweze kuendelea na safari yangu ya kwenda buguruni. upande wa pili kulikuwa kijana mwenye piki piki akisubiri taa kuwaka yeye alikuwa anaelekea mjini akitokea vingunguti na hakuvaa helmet. Mara nikaona askari polisi wawili waliokuwa kwenye piki piki wakimfuata yule kijana na kabra hawajamfikia hule kijana mwenye piki piki alipiga u turn fasta na kuondoka kwa kasi sana kuelekea vingunguti. Swali langu wadau ni
  1: hawa wazee wa tigo kazi zao ni zipi kupambana na uharifu au kufanya kazi za trafiki. kwani muda mwingi wamekuwa wakiutumia kupiga mabao dala dala, bajaji, taxi, piki piki na magari mengine na maswali yao utasikia una leseni, vipi mapato umelipa, mbona taa haziwaki? naomba wadau mnisaidie

  2: hebu niambie tangu hawa jamaa waanze hata siku moja hawajawahi kupambana na majambazi ana kwa ana zaidi yale magari tuliyoyazoea maarufu kama TZ R . ndio mara nyingi huwa yanahusika katika mapambano hivi wao huwa wanakuwa wapi.

  3: hivi kazi yao ni kupiga doria au kukaa sehemu zenye makutano na kusubiri taarifa za uharifu ili waweze kuwa tayari kwa mapambano mfano hai wizi wa total magomeni, duka la pesa kariakoo na matukio mengine mengi

  Kwa leo naomba niishie hapo

  Ni wenu sungura mjanga( kwa tafsiri ya neno kapecha kwa wangoni )

  TANZANIA YA WATANZANIA NA WATAKAO IBADILI TANZANIA NI WATANZANIA WENYEWE INA ANZA NA WEWE.
   
Loading...