Hawa Watu Vipi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Wakati wadau mbali mbali wanalalamika kuhusu wageni kupewa ajira za chee katika idara mbali mbali ,kuna wengine inaonyesha hawashituki kuhusu malalamiko haya na ndio wanaendelea kuleta ndugu , jamaa na marafiki katika idara hizo hata kama anafanya kazi ya usafi wa vyombo si ndugu yake ?

Wiki iliyopita muda wa saa 5 hivi usiku nilikuwa napita mwenge pale , ghafla nikakumbana na jamaa mmoja ambaye kwa sasa tumekuwa marafiki wazuri , akanisimamisha akaniambia najua wewe ni mtu wa IT tulikutana katika duka Fulani si ndio ?

Nikamwambia ndio , akaniuliza unaonaje lile duka ? wale wote wachina , yule fundi wao ni kijana kutoka Uganda ,kasoro yule dada tu ndio mtanzania tena haelewi chochote kuhusu computer na vifaa vyake maana yake chochote kikitokea ni ngumu kumhoji huyu dada haelewi chochote .

Halafu kali kuliko zote huyu dada haelewi kichina yule kijana wa Uganda tu ndio anaelewa kichina kidogo , pamoja na hawa wachina wengine jamaa ananilalamikia vipi unaonaje pale ?

Nikamwambia mimi nikipita pale napenda kumtania yule kijana kuhusu LRA na joseph kony lakini siku moja nilimuuliza amejuana nao vipi hawa jamaa akaniambia yeye ametoka katika tawi lao lengine la Uganda .

Nikamuuliza kama anavbali vyovyote vya kufanya kazi Tanzania akasema hana , yeye amekuja tu hajui chochote hata hana marafiki Tanzania hii mwisho akaniambia huku Tanzania watu wengi sio waaminifu ndio maana wameamua kuja na wakwao .

Baada ya mazungumzo hayo , kijana akaniambia wakati Fulani aliwahi kwenda katika usaili mkoani arusha , alipomaliza kufanya usaili baadaye kidogo akapigiwa simu na mmoja wa wale wasaili kumwambia kwamba siku Fulani anatakiwa aje kuripoti kazini .

Siku hiyo ilipofika HR wa kampuni hiyo akampigia simu kumwambia ajira yake amesitishwa na anapewa mtu mwingine ambaye ni mwanamke huyu mwanamke alikuja nae katika usaili huo mwanamke mwenyewe ni kutoka nchi jirani ya Kenya huyu HR pia ni mkenya kwahiyo jamaa kikaota .

Machozi karibia yananitoka , yaani hata kama umefanyiwa usaili ukapitishwa inawezekana ajira yako ikasitishwa juu kwa juu kwa sababu ya huu undugunaizeshen kila mtu anajaribu kumwita jamaa yake wa karibu , ndugu jamaa na marafiki .

Ikanikumbusha sehemu Fulani niliwahi kufanya kazi , wakati niko pale kwa muda nikashangaa mtu mwingine analetwa kuja kufanya kazi nilipojaribu kuangalia wapi amefanyiwa interview sioni , tangazo la kazi lilibandikwa wapi sioni .

Mimi nikaendelea kuchapa kazi baadaye nikagundua yule kijana ni ndugu wa mwajiri wangu ufanyaji wake wa kazi nao unatia utata , zikitokea kazi yeye hataki kwenda mambo kama hayo hata kama akiwa katika ratiba kisa ndugu wa mwajiri .

Kutokana na mambo haya na mengi yaliyokuwa yanaendelea nikaamua kujiuzuru ili kuokoa fani yangu kutoka katika nafasi niliyokuwa nayo katika sehemu husika na kwenda kufanya kazi sehemu zingine ambazo kuna ushindani wa kweli .

Kwahiyo sasa mtu unaenda katika ajira huku unakumbana na mengi unafanya kazi na watu wasiokuwa na sifa husika na zisizotakiwa au uzoefu husika wa fani husika matokeo yake ni kuharibika kazi na wote muonekane kundi moja
 
Hii kitu sio ya kuongea polepole, Kwenye viwanda vya ndugu zetu Wahindi, kumejaa maajabu, wako wafanyakazi wa Kihindi wanaoingia Tz kama watalii na kupewa kazi kwenye hivi viwanda. Huwa hawaruhusiwi ktoka getini siku za wiki. Hutolewa jumapili na bus kuzungushwa town na kurudishwa factory. Kampuni huajiri mtu kuwafundisha swahili. Hii sio siri kwani Uhamiaji wanajua hili ila ni Dill za wakubwa best.

Kuna Idara nyingi zina ajiri watu ambao TZ wanawataalam wake. Huwezi kuniambia kampuni unahitaji HR toka ulaya. Pia sikubali kwamba Hatuna wataalamu wa fufanya sales Tz. Nakumbuka hata zile kazi za RP ilitakiwa mtaalamu akija awe na msaidizi MTZ ili baada ya muda mtaalamu achape mwendo Mtz ashike nafasi.. Vibali bado vinatolewa kwa mtu mmoja kwa mika kumi na kuendelea.Muda wote huo si tayari Mtz ana Phd?? Jamani Idara ya Kazi ONENI AIBU.

Kuna mwanasiasa mmoja wa hii NCHI alisema, siku moja kizazi kijacho kitalazimika kufukua viongozi walio ongoza hili Taifa kuchunguza kama Brain zao zili kuwa OK. Nalazimika kuamini hiyo siku itafika. Natamani ije LEO
 
Back
Top Bottom