Hawa watu sasa wamekubali kuwa Corona imeisha?

Membe kajipaka vitakasa mikono pia alinawa mikono baada ya kutoka pale na kwenda kutafuna tangawizi kunywa maji ya limau Asprin kwa wingi, corona ipo nyingi hapo jijini Dsm lakini kwa kuwa watu wameamua kufanya siri hawataki kusema ndugu zao wamekufa kwa covid 19 bali husingizia ni magonjwa mengine ya kawaida tu, wengi hawataki ijulikane wana mgonjwa wa corona kwao wakihofia kutengwa na jamii zilizowazunguka, hilo jiji la Dsm lina watu zaidi ya milion 5 na wengi huishi uswahilini kwenye misongamano mkubwa ambapo hufa wengi lakini wanafanya siri huku wewe na CCM mkiendelea kuwahadaa watanzania kuwa corona imekwisha Tanzania.
Utaficha Kifo kweli? Mi mtaani kwetu tangu convid 19 iingie ni juzi tu ndio tumezika mtu mmoja tena mbibi ambaye hata hakufa kwa covid zaidi ya uzee
 
Nakubaliana nawe mkuu..suala corona linafikirisha japo tahadhari ni muhimu kama alivyosema Mh. Rais
 
Kweli. Ninawafahamu angalau watu 11 walioipata na kupona baada ya kujidunga mixer za tangawizi, kitunguu swaumu, kitunguu maji, pilipili kichaa na limao. Hii kitu imetuspare waafrica. Wazungu hata flu tu huwaua sana
Wanaopona ni wengi mno kuliko wanaokufa.

Na wanaoipata bila hata kuugua wala kujua wanayo, nao ni wengi mno.

Hivyo, Corona si hatari kivile.
 
Wanaopona ni wengi mno kuliko wanaokufa.

Na wanaoipata bila hata kuugua wala kujua wanayo, nao ni wengi mno.

Hivyo, Corona si hatari kivile.

Nilisema tukipima nchi nzima kwa mara moja, zaidi ya asilimia 90 huenda wakawa nayo au wameshawahi kuwa nayo.

Tulitandikwa hofu kila kona mitandaoni, TV, radio, wachambuzi yaani tafrani, sikulala siku tatu najua huenda hili dude ni kama Ebola ili nianze kuandika urithi..sijakaa sawa mke wa Bill Gates akasema na hii bado, mizoga ya maiti itatapakaa hakuna pa kusogeza mguu wala nafasi ya kutema mate.

Nikasikililizia weee. Hofu ikatamalaki. Nikasema nchi imekwisha, hamad kutahamaki watu wanapona tu na wengine wanapona juu kwa juu.

Natofautiana na JPM kwenye baadhi ya mambo ila kwa jinsi alivyoshughulika na hili janga nipo upande wake. Wananchi wakapunguza hofu, shule zikafunguliwa, biashara zinaendelea.

Yeye alisisitiza hili janga tutafute namna ya kuishi nalo.
 
Jasusi mbobezi aliwahi kusema Tanzania itatengwa na jumuiya za kimataifa kwa vile tu imechukua hatua tofauti na jumuiya za mataifa mengine katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona
Huyu ni kati ya watu waliotaka vifo kama inzi. Ngoja tuanze kampeni turejeshe tweets zake
 
We vipi
Corona kutokuwepo sasa haimaanishi kipindi kile haikuwepo..
Halafu acheni kufanya kama Afrika nzima Magufuli peke ake hakuweka lockdown..
Nitajie nchi nyingine zaidi ya Kenya,Uganda,Rwanda,South Africa na Nigeria zilizokuwa na lockdown.
Ghana
 
Huwa napenda mtu ajenge hoja inayosimama yenyewe. Ulichosema hapa sioni kama umejenga hoja yoyote. Ni kama kusema 1) A 2) B 3) C. 4) Therfore, H.
 
Jana Russia iliondoa raia wake nchini, us,uk nk wameishaondoa watu wao. Sisi tuendelee kuimba na kumtukuza huyo yesu mpya ila ukweli bado ugonjwa upo na watu wanakufa sana ila haitangazwi. Maisha ni mali yako binafsi unaweza kuwachezea kamali kama utaona inafaa
 
We vipi
Corona kutokuwepo sasa haimaanishi kipindi kile haikuwepo..
Halafu acheni kufanya kama Afrika nzima Magufuli peke ake hakuweka lockdown..
Nitajie nchi nyingine zaidi ya Kenya,Uganda,Rwanda,South Africa na Nigeria zilizokuwa na lockdown.

Naunga hoja, ubarikiwe sana
 
Yeye alisisitiza hili janga tutafute namna ya kuishi nalo.
Baam!! Sawa kabisa.

Kwa kimombo tunaiita ‘adaptation’. Yaani kubadilika kuendana na mazingira yaliyopo.

Mfano, kuzingatia usafi kwa umakini wa hali ya juu. Ukiwa hujisikii vizuri, kaa nyumbani usikilizie kuliko kutoka na kwenda kujichanganya na watu maana waweza kueneza maambukizi, kutokukumbatiana, na kadhalika.

Ajali zinazotokana na magari ni nyingi sana duniani kote. Lakini sijawahi kusikia popote pale duniani watu wakisema tuache kuyatumia magari.

Kinachotokea ni kwamba, tunabadilika.
Tunaendesha kwa umakini zaidi, teknolojia ya usalama wa magari nayo inaboreshwa, tunaweka matuta barabarani, tunatunga sheria na adhabu kali dhidi ya madereva walivyo, tunakumbushana kupitia awareness campaigns kama Wiki ya Usalama Barabarani, na kadhalika na maisha yanaendelea.

Pamoja na yote ajali bado zinatokea na lakini hatuachi kuyatumia magari.

Dhana hiyo hiyo ndo itumike na kwenye magonjwa.
 
Daktari mmoja wa WHO alisema haafiki kutokutoa taarifa za maambukizi ila anamsifu JPM kwa kuwa na msimamo. Akasema lockdown kwa nchi zetu haiwezi leta tija.

Akamalizia yeye anapenda sana mtu anayesimamia maamuzi yake na kutokuyumbishwa, akaenda mbali zaidi kwamba hata kama anachosimamia hakipo sahihi ila kwake ni ule msimamo wa mtu ana uheshim sana kuliko mtu anaebadilikabadilika.
Hawa mabeberu sasa ndio wanamkubali JPM hata uingereza wamesitisha kutangaza takwimu za covid wanasema vipimo havina uhakika kiko wapi sasa akinya kuku sawa lakini akinya bata ooohhh kaharisha
 
Mashirika ya Ndege ya kimataifa bado yanaitenga Tanzania ni Ndege chache za kimataifa zinakuja hapo Dsm, nyinyi mnasema corona haipo lakini ofisi za Balozi wana taarifa za kwenye jamii kote wanajua corona ipo kwa wingi.
Jana balozi wa Italy hapa Tanzania tulimuona kwenye TV Dar akihutubia hana hiyo barakoa
 
  • Thanks
Reactions: len
Daktari mmoja wa WHO alisema haafiki kutokutoa taarifa za maambukizi ila anamsifu JPM kwa kuwa na msimamo. Akasema lockdown kwa nchi zetu haiwezi leta tija.

Akamalizia yeye anapenda sana mtu anayesimamia maamuzi yake na kutokuyumbishwa, akaenda mbali zaidi kwamba hata kama anachosimamia hakipo sahihi ila kwake ni ule msimamo wa mtu ana uheshim sana kuliko mtu anaebadilikabadilika.
Ungetuwekea tujisomee/tusikie wenyewe aliyosema huyo Daktari.

Kwa hivi ulivyofanya hapa ni kutulisha matango tu na kumfanya huyo Daktari aonekane kama juha fulani kwa kusema maneno kama hayo.
 
53 Reactions
Reply
Back
Top Bottom