Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,210
- 113,500
- Thread starter
- #241
Wapi pana ufichaji wa takwimu? Tanzania?Kwenye hizo data za John Hopkins umejiridhisha kujua nchi ngapi katika zote zimekuwa na ujasiri wa kuhuisha takwimu zao kwa wakati?
Niangalipo sasa hivi kwenye link ya hiyo hospitali, duniani kote kume ripotiwa vifo vipya Mexico, Bolivia, S. Korea na Australia tu.
Vipi kama au ni kama kwetu wengine nao jalada la Corona wamekwisha funga?
Au takwimu zako unazokokotoa assumption kubwa ni kuwa nchi isipotoa takwimu basi waathirika au vifo huko hamna?
Nani asiyejua kuwa pana ufichaji mkubwa wa takwimu. Hili si la mzee baba peke yake. Mbona hata huko tunakosoma hawajafa watu au wamekufa 5 tu ni dalili za utambuzi duni, magumashi au nia ovu ya kuficha takwimu tu?
View attachment 1513368
Suala la takwimu lina utata sehemu nyingi tu.
Kuanzia China, Marekani, Tanzania, na kwingineko.
Uingereza majuzi wamesitisha kutoa takwimu kwa sababu ya huo utata.
Takwimu za Marekani nazo zinatia shaka sana.
Za China ndo kabisa...
Bottomline, Tanzania haijaathirika kivile.
Hata Marekani nahisi takwimu zao zimejaa siasa kwa sababu huu ni mwaka wa uchaguzi na baadhi ya watu hawampendi Trump na hivyo kutumia takwimu mbaya ili kumfanya apoteze wafuasi wake.
Corona Marekani itaisha tarehe 3 Novemba, win or lose...