juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,449
Nimeshindwa kuelewa niweke neno gani ambalo linaweza kushabihiana na neno gaidi,maana Tanzania hatuna ugaidi ila nataka nikwambie tu kwamba watu wanaoteka au kutesa watu hapa Tanzania ni hatari kuliko hata makundi yote ya kigaidi hapa duniani.
Kwa sababu watu walimvamia Dr. Mvungi wakamshambulia hadi mzee akafa, hadi leo haijajulikana ni watu gani na nini sababu ya kufanya hayo.
Mwandishi wa habari na mbunge wa ubungo Saed Kubenea alishawahi kuvamiwa ofisini kwake na kumwagiwa tindikali usoni, hadi leo haijulikani waliofanya hayo wala sababu hazijulikani.
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kubanda alivamiwa na watu wasiojulikana akapigwa akaumizwa, hadi leo haijulikani ni nani walifanya hayo na kwa sababu zipi.
Aliyekuwa mwenyekiti wa madaktari alitekwa na kupelekwa msitu wa mabwepande,alipigwa nusu kufa hadi leo haijulikani nani alifanya hayo na kwa sababu zipi?
Bomu lilirushwa kwenye mkutano wa Chadema hadi leo haijulikani aliyefanya hayo wala sababu zake.
Na safari hii kapotea Ben saanane haijulikani alipo wala sababu ya kupotea,kwa mtirirko huo ni wazi kwamba hao wanaofanya matukio hayo ni watu hatari sana kuliko magaidi wote duniani.
Halafu wanajua kutunza siri sana,maana magaidi wakifanya tukio huwa wanasema,ila hawa hawasemi na hawakamatwi.