Hawa watu ni hatari kuliko hata magaidi wote duniani

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,589
2,000
Nimeshindwa kuelewa niweke neno gani ambalo linaweza kushabihiana na neno gaidi,maana Tanzania hatuna ugaidi ila nataka nikwambie tu kwamba watu wanaoteka au kutesa watu hapa Tanzania ni hatari kuliko hata makundi yote ya kigaidi hapa duniani.

Kwa sababu watu walimvamia Dr. Mvungi wakamshambulia hadi mzee akafa, hadi leo haijajulikana ni watu gani na nini sababu ya kufanya hayo.

Mwandishi wa habari na mbunge wa ubungo Saed Kubenea alishawahi kuvamiwa ofisini kwake na kumwagiwa tindikali usoni, hadi leo haijulikani waliofanya hayo wala sababu hazijulikani.

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kubanda alivamiwa na watu wasiojulikana akapigwa akaumizwa, hadi leo haijulikani ni nani walifanya hayo na kwa sababu zipi.

Aliyekuwa mwenyekiti wa madaktari alitekwa na kupelekwa msitu wa mabwepande,alipigwa nusu kufa hadi leo haijulikani nani alifanya hayo na kwa sababu zipi?

Bomu lilirushwa kwenye mkutano wa Chadema hadi leo haijulikani aliyefanya hayo wala sababu zake.

Na safari hii kapotea Ben saanane haijulikani alipo wala sababu ya kupotea,kwa mtirirko huo ni wazi kwamba hao wanaofanya matukio hayo ni watu hatari sana kuliko magaidi wote duniani.

Halafu wanajua kutunza siri sana,maana magaidi wakifanya tukio huwa wanasema,ila hawa hawasemi na hawakamatwi.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
Hivi ile kesi ya Saed Kubenea ya kuwasingizia masheikh wa Zanzibar wamelawitiwa imeishia wapi?
 
bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Umesahau na zile mahiti Saba walizozika katika shallow graves. Mungu mlinde Ben huko aliko.

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]
 
mekuoko

JF-Expert Member
Nov 15, 2012
324
250
Tunapita kipindi kigumu, Mungu tuhurumie na tuokoe na majanga ya kupangwa.
 
Noel france

JF-Expert Member
Oct 8, 2012
897
500
Nimeshindwa kuelewa niweke neno gani ambalo linaweza kushabihiana na neno gaidi,maana Tanzania hatuna ugaidi.ila nataka nikwambie tu kwamba watu wanaoteka au kutesa watu hapa Tanzania ni hatari kuliko hata makundi yote ya kigaidi hapa duniani.kwa sababu watu walimvamia Dr,Mvungi wakamshambulia hadi mzee akafa ,hadi leo haijajulikana ni watu gani na nini sababu ya kufanya hayo
Mwandishi wa habari na mbunge wa ubungo Saed Kubenea alishawahi kuvamiwa ofisini kwake na kumwagiwa tindikali usoni,hadi leo haijulikani waliofanya hayo wala sababu hazijulikani
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kubanda alivamiwa na watu wasiojulikana akapigwa akaumizwa,hadi leo haijulikani ni nani walifanya hayo na kwa sababu zipi
Aliyekuwa mwenyekiti wa madaktari alitekwa na kupelekwa msitu wa mabwepande,alipigwa nusu kufa hadi leo haijulikani nani alifanya hayo na kwa sababu zipi?
Bomu lilirushwa kwenye mkutano wa Chadema hadi leo haijulikani aliyefanya hayo wala sababu zake
Na safari hii kapotea Ben saanane haijulikani alipo wala sababu ya kupotea,kwa mtirirko huo ni wazi kwamba hao wanaofanya matukio hayo ni watu hatari sana kuliko magaidi wote duniani.harafu wanajua kutunza siri sana,maana magaidi wakifanya tukio huwa wanasema,ila hawa hawasemi.na hawakamatwi.
juvenile umetumwa na nani kuongea yote aya? uogopi?
 
wambagusta

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
2,333
2,000
Uwezi jua na atuwezi jua labda hats hao unahona wewe wanaonewa labda nao wanahusika kwa namna furan hili wananchi tuhamini hivyo kama unavyo amini wewe
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,644
2,000
Nimeshindwa kuelewa niweke neno gani ambalo linaweza kushabihiana na neno gaidi,maana Tanzania hatuna ugaidi.ila nataka nikwambie tu kwamba watu wanaoteka au kutesa watu hapa Tanzania ni hatari kuliko hata makundi yote ya kigaidi hapa duniani.kwa sababu watu walimvamia Dr,Mvungi wakamshambulia hadi mzee akafa ,hadi leo haijajulikana ni watu gani na nini sababu ya kufanya hayo
Mwandishi wa habari na mbunge wa ubungo Saed Kubenea alishawahi kuvamiwa ofisini kwake na kumwagiwa tindikali usoni,hadi leo haijulikani waliofanya hayo wala sababu hazijulikani
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kubanda alivamiwa na watu wasiojulikana akapigwa akaumizwa,hadi leo haijulikani ni nani walifanya hayo na kwa sababu zipi
Aliyekuwa mwenyekiti wa madaktari alitekwa na kupelekwa msitu wa mabwepande,alipigwa nusu kufa hadi leo haijulikani nani alifanya hayo na kwa sababu zipi?
Bomu lilirushwa kwenye mkutano wa Chadema hadi leo haijulikani aliyefanya hayo wala sababu zake
Na safari hii kapotea Ben saanane haijulikani alipo wala sababu ya kupotea,kwa mtirirko huo ni wazi kwamba hao wanaofanya matukio hayo ni watu hatari sana kuliko magaidi wote duniani.harafu
wanajua kutunza siri sana,maana magaidi wakifanya tukio huwa wanasema,ila hawa hawasemi.na hawakamatwi.
Hapo kwenye blue muulize ule mkanda wa soweto alio sema anao uko wapi?
pia muulize alipo Ben saanane
 
Ruttashobolwa

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
47,644
2,000
Alafu unaambiwa nchi ya amani na upendo .........

Juzi si umesikia walimteka wakili msomi mapanga ya kichwa kakatwa katwa.............

Hawa watu ni hatari sana bora hata anayejilipua ukafa naye kuliko kuachwa kilema......
alisema ametekwa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom