Hawa watu kwanini hawajaanza kuhojiwa?

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,111
2,000
Toka mheshimiwa rais apokee report ya pili ya mchanga wa dhahabu ni zaidi ya wiki imepita.

Baada ya kupokea report hiyo mheshimiwa Rais hakumung'unya maneno , alisema anakubaliana na mapendekezo yote ya Kamati na akaelekeza mamraka zote za serikali kila moja katika nafasi yake zishiriki katika kuyafanyia kazi mapendekezo hayo.

Hakuishia hapo, akaelekeza vyombo vya dola viwahoji wote waliotajwa katika report hiyo.

Ikumbukwe,wakati akipokea report ya kwanza katika hotuba yake alitoa maelezo ambayo yalimaanisha waziri wa nishat na madini hastahiri kuendelea kushikiria nafasi hiyo na masaa machache baadae Siku hiyo hiyo alimfuta kazi.

Waliotajwa katika report ile wanajulikana kwa majina na mmoja wao (karamagi) amekaririwa na vyombo vya habari akisema yuko tayari kutoa ushirikiano.

Sasa sielewi ni kwa nini hawajaanza kuhojiwa , na cha ajabu Ikulu,waziri wa sheria na katiba na waziri wa mambo ya ndani ghafla wamejikita kwenye hoja za watu ambao tunajua hawatahojiwa achilia mbali kwamba hawakutajwa kwenye report.

Hivi hata kumuita mmoja wao tu na kumwambia mnafikiria kumuhoji imekuwa shida?
 
Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
18,664
2,000
Hivi unasubiri mtu ahojiwe kweli? Ahojiwe nini wakati mabosi waliowaagiza wameambiwa waachwe wapumzike? Kwa kifupi hapa hakuna kesi.

Watanzania wanafanywa wapumbavu sana aisee na hii serikali.
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,284
2,000
Porojo tu zile hakuna wa kuhojiwa wala kuguswa.

Nchi imejaa wasanii kila kona.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,980
2,000
Toka mheshimiwa rais apokee report ya pili ya mchanga wa dhahabu ni zaidi ya wiki imepita.

Baada ya kupokea report hiyo mheshimiwa Rais hakumung'unya maneno , alisema anakubaliana na mapendekezo yote ya Kamati na akaelekeza mamraka zote za serikali kila moja katika nafasi yake zishiriki katika kuyafanyia kazi mapendekezo hayo.

Hakuishia hapo, akaelekeza vyombo vya dola viwahoji wote waliotajwa katika report hiyo.

Ikumbukwe,wakati akipokea report ya kwanza katika hotuba yake alitoa maelezo ambayo yalimaanisha waziri wa nishat na madini hastahiri kuendelea kushikiria nafasi hiyo na masaa machache baadae Siku hiyo hiyo alimfuta kazi.

Waliotajwa katika report ile wanajulikana kwa majina na mmoja wao (karamagi) amekaririwa na vyombo vya habari akisema yuko tayari kutoa ushirikiano.

Sasa sielewi ni kwa nini hawajaanza kuhojiwa , na cha ajabu Ikulu,waziri wa sheria na katiba na waziri wa mambo ya ndani ghafla wamejikita kwenye hoja za watu ambao tunajua hawatahojiwa achilia mbali kwamba hawakutajwa kwenye report.

Hivi hata kumuita mmoja wao tu na kumwambia mnafikiria kumuhoji imekuwa shida?
Unaposema hawa Watu halafu unaishia tu kumtaja mmoja wapo Karamagi na kutotutajia hao wengine unataka tukueleweje Mkuu?
 
Babuu Rogger

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
1,517
2,000
Kwa hiyo hela iliyotumika kuanzisha mahakama ya mafisadi imeenda hivi hivi kama ela ya katiba mpya ilivyopukutika!!!!?? ama kweli hii ndio tz ya alieturoga ameshakufa....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom