The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Hawa watoto wa wameweza kunusurika na mazingira hatarishi ya msitu mkubwa wa Amazon kwa siku 40 bila chakula wala malazi yoyote hadi walipopatikana leo kutoka kwenye kikosi cha waokoaji.
Watoto hao 4 walipotea mwanzoni mwa mwezi wa 5 baada ya ndege waliyokua wakisafiria kupata hitilafu ya injini na kuanguka kwenye msitu wa Amazon na kuua watu 3, rubani 2 na mama yao na hao watoto.
Baada ya jeshi la uokozi kufika eneo la tukio la ajali ya ndege wakakuta miili 3 lakini hakuna watoto, mtoto mkubwa ambae ni binti ana miaka 13 na mdogo kabisa ana mwaka 1.
Watoto hao ni jamii ya watu wa asili ya msitu wa Amazon. Hii ndio sababu inayosemekana kuchangia watoto hao kuweza kuishi siku 40 msituni kutokana na kujua mbinu za asili ya kuishi, survival skills toka wakiwa wadogo.
Watoto hao wamepatikana wakiwa wazima ila wenye afya iliyodhoofu hasa mkubwa wa miaka 13 ambae inadaiwa alikua akiwapa wadogo zake chakula chote wanachokipata wale kwanza kisha yeye anakula kitakachobaki.
Tukumbuke. Amazon imejaa nyoka wakubwa na wakali kama Anaconda, Chui wakali wanaoitwa Jaguar na mamba wakali pamoja na wale samaki wanaopiga shoti za umeme ukiingia kwenye himaya yao.
Je ikitokea ukajikuta kwenye mazingira magumu kama hayo can you survive?