Hawa Watangazaji Wawili wa Star Tv Wanatumia neno Hili Vibaya!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Ni Bernard James na Sauda Mwilima wote watangazaji wa Star Tv. Bernard James wakati mwingine anatangaza michezo na Sauda siku zote ni kipindi cha Bongo Beats. Wote wawili wanapenda sana kutumia neno 'kuweza' na wanalitumia kwa namna ambayo si sahihi (Nionavyo mimi)

Kwa mfano, Bernard James akitangaza mchezo wa mpira wa miguu utamsikia akisema: " Taifa Stars iliweza kufungwa mabao 4 na Ivory Coast. Neno hili la 'kuweza' anapenda sana kulitumia.Naye Sauda Mwilima kwenye wasifu wa mwana hip-hop aliyezikwa hivi karibuni alisema: " Mwanamuziki Langa aliweza kuugua na kupelekwa Muhimbili kwa matibabu. Huko basi, mambo yalishindikana na akaweza kufariki"

Je, wataalamu wangu wa lugha, hayo ni matumizi sahihi ya neno 'kuweza'?
Naomba msaada.
 
Mkuu badala ya ya tujadili twiga alipandishwaje kwenye ndege, unataka tujadili hayo kweli? Kwa maslai ya nani?
 
Mzee tupo kwenye majonzi mazito ya kufiwa ndugu zetu kule Arusha, mambo ya kuweza waachie wazee wa Lumumba.
 
Mzee tupo kwenye majonzi mazito ya kufiwa ndugu zetu kule Arusha, mambo ya kuweza waachie wazee wa Lumumba.
Bahimba. Wazee wa lumumba hawatumiii sana neno la ' kuweza' Neno lao kuu ni 'mchakato'
 
Last edited by a moderator:
Kwa maslahi ya kukuza lugha yetu "KISWAHILI"...kwa hyo kila siku tujadili tembo wanavopanda pipa..heeeee:eek::confused::p:p:p
Ni kweli biee. Jukwaa hili ni la lugha. Mambo ya kusafirisha twiga na kupiga watu mabomu yana mahali pake.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu badala ya ya tujadili twiga alipandishwaje kwenye ndege, unataka tujadili hayo kweli? Kwa maslai ya nani?
KakaJambazi, ya twiga kupandishwa kwenye ndege yana mahala pake.Hapa tujadili matumizi ya lugha yetu kwa maslahi ya urithi wetu wa lugha.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu badala ya ya tujadili twiga alipandishwaje kwenye ndege, unataka tujadili hayo kweli? Kwa maslai ya nani?

Mtoa mada yuko sahihi,mada ina mifano mizuri tu kuhusu matumizi ya lugha,.Ni namna gani Twiga kapandishwa kwenye ndege ni muhimu kujadili ila hapa sio mahali pake,twaweza kujadili hilo kule Tech, Gadgets & Science Forum ,Jamii Intelligence na kungineko.
 
Hilo neno linatumika visivyo. Na nakushauri mtoa mada uwarekebishe wengine wanaobananga lugha kwenye maoni yao. Kwa mfano kuna mmoja hapo ameandika komenti. Lumumba maneno yanayotumika ni MCHAKATO, CHANGAMOTO.
 
Ki msingi hawako sahahi kutumia 'kuweza' katika kushindwa(kufeli)-neno hili hutumika zaidi katika matokeo chanya
 
Back
Top Bottom