Hawa Wasanii wetu wa Muziki vipi?

Apr 4, 2011
39
9
Kuna wimbo wa umefanywa na wasanii mbalimbali wa hapa nyumbani Tanzania ktk kuazimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ingawa wenyewe wanadai miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Jambo linalonisikitisha ktk wimbo huo ukisikiliza kuanzia mwamzo mpaka mwisho hakuna kitu wanachozungumzia zaidi ya AMANI tu.
Kitu ninachojiuliza hivi hawa wasanii wetu hawana jambo lengine ambalo wangeweza kuzungumzia kuhusu miaka hii 50 ya uhuru zaidi ya AMANI tu!
 
Wimbo wenyewe mbaya, kila mtu ameimba mashairi anayojisikia hivyo hauna maana yoyote. Wimbo maalum kama huu inabidi utungwe na mtunzi mahili kisha kila msanii apewe kipande chake, tofauti na walivyofanya wengi wao hawajui kuandika mashairi yenye mashiko badala yake unapata makelele tu.
 
Yaani siupendi ule wimbo,pengine kuliko nyimbo zote nilizowahi kusikiliza,.........pppppuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuf
 
Ni kama vile wametumwa kuhubiri agenda flani dhaifu inayotumiwa na chama fulani kilichokongoroka. Vilaza hawa ovyoo!
 
Kuna wimbo wa umefanywa na wasanii mbalimbali wa hapa nyumbani Tanzania ktk kuazimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ingawa wenyewe wanadai miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Jambo linalonisikitisha ktk wimbo huo ukisikiliza kuanzia mwamzo mpaka mwisho hakuna kitu wanachozungumzia zaidi ya AMANI tu.
Kitu ninachojiuliza hivi hawa wasanii wetu hawana jambo lengine ambalo wangeweza kuzungumzia kuhusu miaka hii 50 ya uhuru zaidi ya AMANI tu!
Hakuna amani bila haki.
 
Sasa wewe ulitaka wasifie nini?,epa au richmond?! Halafu kaa ukijua kuwa ule sio wimbo wa serekali wa kusherehekea miaka 50 ya uhuru ule ni wimbo uliombwa na wasanii mbalimbali kusheherekea miaka 50 ya uhuru na wao au waandishi wa wimbo huo wakaona ndani ya miaka hamsini kitu cha kujivunia angalau ni amani hivyo wakaona waimbe zaidi kuhusu amani ndani ya wimbo huo. Sasa wewe wakerwa na nini? Mbona nawe uko huru si ujikusanye na wenzako mnaouchukia huo wimbo ili mtoe wa kwenu mtakaouimba vile mnavyotaka tani yenu! Acheni tabia ya kudharau yanayofanywa na wenzenu nyie yenu makubwa na mazuri mliyoyafanya yako wapi? Kama inakukera ukiisikia tu au ukianza kuiona badilisha station halafu uone kama maisha yataendelea au vipi!
 
I didnt make out what they were singing, labda nikiusikiliza kwa mara ya pili which I dought.
 
Sasa wewe ulitaka wasifie nini?,epa au richmond?! Halafu kaa ukijua kuwa ule sio wimbo wa serekali wa kusherehekea miaka 50 ya uhuru ule ni wimbo uliombwa na wasanii mbalimbali kusheherekea miaka 50 ya uhuru na wao au waandishi wa wimbo huo wakaona ndani ya miaka hamsini kitu cha kujivunia angalau ni amani hivyo wakaona
PUMBAVU ZAO HAWAMUONI BONTA au ROMA
kazi kukalilishwa tu amani bila haki
wapi na wapi? upupu mtupu!
 
Ulitegemea kusikia nini kwenye huo wimbi zaidi ya kelele?hakuna ujumbe wala walichomaanisha,kila mtu ameimba ili mladi single itoke baaasi.
 
mimi nayashangaa masanii ya bongo siyo yale ya muv wala ya kuimba kama kuigiza basi mapenz kama kuimba bac ni mapenzi au viduku yakimba AMAN YAMEKALISHWA au YAMEPEWA KIMEZA MATE kesho yanarudi kwenye njaa! mengine ndo yale yale yalokuwa yanazunguka na JK kwenye campeni. pongezi kwa BONTA, ROMA, YAKI. MENGINE YANAIMBA KUSIFU POMBE NA BANG PUMBAVU SHENZI NYIE SHAME ON YOU!
 
sijui kwanini nina bahati mbaya sana na huo wimb,kila nikiwasha tv lazima nikutane nao..kila msanii anaongelea amani tu,hamna cha kuongelea miaka 50 jamani?
 
Wimbo wenyewe umekaa kidisco disco, haya ndiyo matokeo ya kuwapa kazi watoto wasiojua lolote, bora Wangepewa Msondo ngoma. ama watu kama Banza Stone na Muhidin Ngurumo, lakini hawa wavuta Bangi unadhani kitatokea nini !!?
 
Ule kwangu mm ni sawa na UCHAFU, TAKATAKA, KOHOZI, MAVI, MAJI TAKA, yani unaniKERA mimi basi tu, yani wakishapewa MAKOMBO na hao MAFISADI wana KURUPUKA tu, hao ni VIBARAKA.
 
yan wamesahau yote kuhusu haki zao za kisanii na kuhusu mapato yao katika kazi zao za kisanii.

angalia sasa wanavyowanufaisha akina ruge,riz1 na akina january. malipo kidogo bado unaimba aman ya wapi sasa.

nimeshangaa sana humo ndani kumuona fidq, ay na fa nao wanahubiri amani as.s.ho..les.

iyo kazi wangewaachia hao watoto akina bele9. nashangaa dogo janja nae kasahau shida za masela pale ngarenaro,ungalmited.
 
Wimbo wenyewe mbaya, kila mtu ameimba mashairi anayojisikia hivyo hauna maana yoyote. Wimbo maalum kama huu inabidi utungwe na mtunzi mahili kisha kila msanii apewe kipande chake, tofauti na walivyofanya wengi wao hawajui kuandika mashairi yenye mashiko badala yake unapata makelele tu.

Mahiri.
 
Back
Top Bottom