Hawa wanasheria walioshika kuandikiwa charge ndio ushauri kuhusu mikataba na miswada?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kilichotokea kwenye kesi ya Mbowe kina impact Sana kwenye siasa na uchumi wetu. Aina ya mawakili wa serikali na Majaji tulionao na kwa namna wasivyo serious kunapaswa kutujuza kwamba lipo tatizo serikalini.

Juzi Mama aliwaelekeza waache kubambikia watu kesi, walipoelekezwa wakafuta zaidi ya kesi za watu Mia nne zilizofunguliwa kimakosa. Tukaona sawa tu

Leo wamemfanya Jaji aonekane kama kiti alichokalia Hana uwezo nacho Bali kapewa kimkakati. Hii ni fedhea kwa mahakama

Lakini kibaya ni pale unapobaini mawakili wamekosa umakini hata wakiandika hati za mashtaka. Lakini pia watu wanapiga kelele humu mitandaoni kwamba charge zimekosewa lakini hakuna aliyejipa muda wakushauri zibadilishwe Hadi wanakuja kuaibishwa mahakamani adharani. Lakini pia hata lugha waliyoandikia charge Awana uwezo wakuitumia mahakamani, means walicopy na kupaste.

Swali lakujiuliza, Hawa ndio huandaa mikataba? Hawa ndio huandaa miswada? Kama ndio Hawa, uwezo wakujadiliana wanao? Wanasoma? Taifa lipo salama mikononi mwa wasomi Hawa,?
 
Ndio hawahawa wanaoshiriki kuandaa miswada ya sheria za kipumbavu zinazopitiswa bungeni. Nchi hii tusipokaa kuangalia namna bora kutengeneza Taasisi imara zinazojitegemea tutaendelea kuwa masikini mpaka mwisho wa dunia hata kama tutakua na kina nyerere kwenye kila idara na ofisi ya serikali maana serikali ya Tanzania inategemea kila kitu CCM ndio iamue na CCM mtaji wao ni ujinga wa watanzania ukizingatia CCM imejaa wachumia matumbo wanaojifanya wazalendo
 
Hoja zao walikuwa wanawasilisha kwa "lugha ya taifa" wakati wale wengine walijenga hoja kwa "lugha rasmi ya kisheria". Hiyo ni mojawapo ya tofauti kubwa kwa pande mbili hizo kwenye shauri hili.
 
Sasa nimeamini maneno ya Prof Assad,kwamba asilimia 60 ya watumishi wa umma hawana uwezo wa kumudu kazi zao,ni mbumbumbu,vilaza,akili hakuna
 
Ukiona wamevaa masuti na mavyeo na majukumu makubwa ya TAIFA waliopachikana unaweza waza wanazo AKILI , kumbe HAKUNA.

MaCCM wote akili zao hazina akili.
 
Back
Top Bottom