Hawa wananchi wa Chato waliolima bangi kwenye ardhi waliyopewa na Rais wachukuliwe hatua stahiki

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Imeripotiwa na luninga ya ITV kuwa baadhi ya wananchi waliopewa ardhi na Rais Magufuli kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula wao wamepanda bangi.

Mkuu wa wilaya ya Chato na kamati yake ya ulinzi na usalama imewalazimu kuvamia mashamba hayo na kuwashurutisha wale waliolima bangi waing'oe na kuichoma moto mbele ya waandishi wa habari

Source ITV habari

My take; hawa waliolima bangi wachukuliwe hatua za kisheria kwa kutenda kinyume na agizo la Rais
 
Hao hawatakiwi kukamatwa ni wawekezaji wazawa wametangulia kuwekeza kabla wawekezaji wa kigeni hawajaruhusiwa kujakuwekeza.
 
hili zao lilishawekewa mikakati kuwa ni muhimu kwa malighafi, mbegu zake zinatengeneza mafuta ambayo ni malighafi muhimu madawa ya binadamu

majibu ya dokezo, taratibu zilisha tolewa taarifa bungeni naona huyu mkuu wa wilaya anatafuta kuondolewa kwe wazifa wake

hajui pato la taifa saivi lategemea hayao mazao
 
johnthebaptist,
It's funny how someone else's success brings pain
When you no longer involved, that person has it all
And you just stuck standing there
 
Na wakati mwingine bwana yule ndiye kawaamurui wailime... jaribu kufikiri

Na yule jamaa wa mjengoni anaye Sukuma hoja ya mmea kuna MTU anawakilisha... hii siyo buree

''Akili za kuambiwa changanya na zako..'' By Mkwere, mzee wa Msoga

*Soon naiona California, Canada na UK ndani ya Bongo's hasa ktk matumizi ya mmea

Legalise it...Peter Tosh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huenda ni maelekezo toka juu. Wanatakiwa walime ili uwanja wa ndege upate kazi. Ila waliyomvutisha inatosha jamani. Waache hivyo hivyo.
 
Bwashee jamaa wamewahi msimu, wanazo taarifa nyeti hao kwamba soon mzigo utakuwa hewani wameamua kuwahi sokoni..
 
"Kuwashurutisha wale waliolima bangi wain'goe na kuichoma moto"

Kwamba hiyo ndio adhabu waliyopewa?

Mbona yule mzungu waliemkamata Kilimanjaro hawakumshurutisha kuin'goa na kuichoma moto ile bangi yake?

Hao wakulima wa bangi Chato nao wapelekwe mahakamani kama wanavyopelekwa wengine wanaolima bangi maeneo tofauti Tanzania, pasiwepo na upendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh...!, mimi nashauri huyu DC aondolewe!, hao wananchi wanaonewa bure tuu, maeneo mengi Usukumani bangi inajiotea tuu yenyewe, na maadam Wasukuma wenyewe bangi haiwadhuru, na bangi ina active ingredients 4 muhimu kwa matumizi ya medical marijuana ambazo ni raw material ya kutengenezea CBC, viburudisho, na virembesho.

Ingredients hizo ni Tetrahydrocannabinol, cannabidiol, cannabinoids na
Tetrahydrocannabivarin hivyo kwa vile Tanzania bado hatuna viwanda vya products hizo, then badala ya kuing'oa, tupitishe ku legalize kilimo cha zao la bangi for export na kufanya usimamizi mzuri ili bangi hiyo isivutwe.

Mimi hili nilishauri siku nyingi nyuma ikiwa ni pamoja na kuhalalisha ile biashara yetu ile ya

https://www.jamiiforums.com/threads...nia-tuhalalishe-the-oldest-profession.437136/
P
 
Imeripotiwa na luninga ya ITV kuwa baadhi ya wananchi waliopewa ardhi na Rais Magufuli kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula wao wamepanda bangi.

Mkuu wa wilaya ya Chato na kamati yake ya ulinzi na usalama imewalazimu kuvamia mashamba hayo na kuwashurutisha wale waliolima bangi waing'oe na kuichoma moto mbele ya waandishi wa habari

Source ITV habari

My take; hawa waliolima bangi wachukuliwe hatua za kisheria kwa kutenda kinyume na agizo la Rais
Hapo njia nzuri nadhani wawekewe kiwanda cha kuchakata bangi na wapewe mafunzo ya kina ya namna ya kuliendeleza zao hilo na kuuza nje kihalali, iwaletee faida wakulima hao na taifa kwa ujumla.

Kuichoma moto hakuna faida yoyote ni kuteketeza rasilmali.

Bangi ni zao lenye manufaa mengi na faida kubwa ikiwa litapewa kipaumbele na kuwekewa mikakati ya kuliendeleza zao hilo kibiashara.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom