fenestra rotunda
JF-Expert Member
- Jun 18, 2015
- 608
- 614
Nimekutana na baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wa mwaka wa tatu kozi ya uuguzi na ukunga mtaani kwetu hali iliyonifanya kuuliza kulikoni wapo majumbani ilhali chuo chao kilishafunguliwa.
Wanadai hata hao hawaelewi kwani waliambiwa wataripoti mbeya kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na sio Dodoma kwa kuwa hospitali ya Dodoma kuna msongamani wa wanafunzi hivyo wanashindwa kusoma kwa umakini.
Siku ja Jumatatu waliambiwa wanatakiwa kuripoti Mbeya siku ya Jumamosi ya tarehe 12 lakini mpaka sasa hawajaambiwa watafikia wapi, makazi yao, ratiba ya mafunzo kwa vitendo (clinical practice), usajili, kusaini boom N.k na siku yenyewe imekaribia.
Hata hivyo wamelalamika kuwa taarifa hiyo ilichelewa kuwafikia kwani ilikuja siku ya alhamis ya tarehe 3 huku baadhi wakiwa wameshatangulia Dodoma kwa ajili ya kuwa hi usajili ambao ulikuwa unaanza tarehe 5.