Uchaguzi 2020 Hawa wakienda kupiga kura Oktoba 28, CCM hatuna chetu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,068
2,000
Kwa ngazi zote za Urais, Ubunge na Udiwani. Kama chama tawala kinachoomba ridhaa ya miaka mitano mingine, tukeshe tukiomba kuwa hawa wafuatao wasiende kupiga kura Oktoba 28 mwaka huu. Wakienda na wakipiga kura, CCM hatutakuwa na chetu. Watapiga kura za uchungu na kuukataa uchungu zaidi. Zitakuwa kura za kuponya mioyo yao kwakuwa watakuwa wametoa maumivu yao kupitia kukataa.

Hawa wakienda kupiga kura, CCM lazima ije na mbinu mbadala kuliko daladala. Wataikataa CCM na wagombea wake mchana peupe. Wataikataa CCM na wagombea wake kwa kutumia kadi zao za kupigia kura, kwenda kwao kupiga kura. CCM itakataliwa kwa maumivu yaliyotokana na matendo na maneno ya Serikali iliyoundwa nao. Nawataja wa uchache watu hao ambao kama CCM tunapaswa kukesha tukiomba wasiende kupiga kura.

Waliobomolewa nyumba na biashara zao bila kulipwa fidia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofukuzwa kazi kwa sakata la vyeti bila kupewa hata sumni pamoja na kufanya kazi kwa miongo kadhaa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliopatwa na majanga ya asili bila kupata msaada wa kiserikali pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofungiwa biashara na shughuli zao za kiuchumi kwa njia za kibabe pamoja na wategemezi wao.

Na wote ambao wameoisoma namba kwa namna moja au nyingine!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kagera, Tanzania)
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
25,180
2,000
Waliobomolewa nyumba na biashara zao bila kulipwa fidia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofukuzwa kazi kwa sakata la vyeti bila kupewa hata sumni pamoja na kufanya kazi kwa miongo kadhaa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliopatwa na majanga ya asili bila kupata msaada wa kiserikali pamoja na ndugu, jamaa na marafiki zao; waliofungiwa biashara na shughuli zao za kiuchumi kwa njia za kibabe pamoja na wategemezi wao.
Ndiyo maana namomba Lisu akazie sana watu hapo juu uliowataja, hawa kila mmoja angalau awavute watu 10 wa kumpigia kura Lisu, basi kama ulivyosema mchezo umekwisha!
 
xng hua

JF-Expert Member
Sep 24, 2016
2,062
2,000
We mzee kumbe unafanana sana matendo na nyumbu

Ok wapigakura ni ml28 je ukijumlisha hao wote unapata ngapi? ukitaka +na wafanyakazi wa serikali
wanachama wa ccm pekee wanatosha kumrudisha JPM madarakani
nyie endeleeni kupiga ramli tuu ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
6,655
2,000
We mzee kumbe unafanana sana matendo na nyumbu

Ok wapigakura ni ml28 je ukijumlisha hao wote unapata ngapi? ukitaka +na wafanyakazi wa serikali
wanachama wa ccm pekee wanatosha kumrudisha jpm madarakani
nyie endeleeni kupiga ramli tuu ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Wafanyakazi serikalini ni wachache sana..wanachama wa CCM ni wachache sana...kura za maoni za zamani wagombea wa CCM walikuwa wanapita mitaani na mikadi yao wanatoa hela kwa vijana wakawapigie kura...Sasa baaasiii
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
34,460

Ccm haina wanachama 3m hai nchi hii. Mke wangu ana kadi ya ccm ili kupata upendeleo wa mikopo ya vikoba, lakini hataki hata kuisikia.
 
xng hua

JF-Expert Member
Sep 24, 2016
2,062
2,000
Wafanyakazi serikalini ni wachache sana..wanachama wa CCM ni wachache sana...kura za maoni za zamani wagombea wa CCM walikuwa wanapita mitaani na mikadi yao wanatoa hela kwa vijana wakawapigie kura...Sasa baaasiii
Ccm inawanachama 8ml
 
jimama26

JF-Expert Member
Jul 30, 2013
1,950
2,000
Kuna kina sie wapenda haki. Sisi ndio tunamkimbizia huko kijijini kwakwe asubuhi mapema tarehe 28.10.2020. Aende akaangalie vizuri vitu alivyojiwekezea Chato akiwa jobless.

Hapa ni Lissu tu.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
34,460
2,000
iyo ml3 ni chadema
Ccm inao 8ml

Maisha yako, nchi hii haina wazee milioni 8. Ukiona kijana ana kadi ya ccm ni aidha ni mfaidika wa moja kwa moja na ccm, au kachukua kadi ilikufanikisha shughuli zake zinazohitaji upendeleo wa kiccm. Ila wanachama wa ukweli kwa maana ya itikadi ni wazee, na hakuna wazee milioni 8 nchi hii. Ww sema mpaka sasa ccm imeuza kadi zaidi ya 8m, maana kadi ni shilingi 500, lakini sio wanachama hai.
 
acha kudhania!!
 
kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,871
2,000
We mzee kumbe unafanana sana matendo na nyumbu

Ok wapigakura ni ml28 je ukijumlisha hao wote unapata ngapi? ukitaka +na wafanyakazi wa serikali
wanachama wa ccm pekee wanatosha kumrudisha jpm madarakani
nyie endeleeni kupiga ramli tuu ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Nani kakuambia wafanyakazi wa serikali (umma ) watampigia ccm kura? ndugu bora useme wengine ila siyo wafanyakazi wa umma hao hata Magu anajua hawamtaki kwa wingi wao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom