Hawa wafuatiliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa wafuatiliwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Oct 20, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Wiki iliyopita nilialikwa katika mkutano mmoja wa bidhaa , kampuni moja kutoka India ilikuwa inatafuta watu wa kuweza kutangaza na kuuza bidhaa zao za aina mbali mbali kama vifaa vya mawasiliano na zingine za mambo ya afya afya .

  Ila bidhaa zote hizi unatakiwa kwanza uwe na anuani mtandano unapata anuani hiyo baada ya kununua kifaa kimoja au bidhaa ambazo bei yake ni kuanzia dola 500 inategemea na bidhaa yenyewe mambo kama hayo

  Hawa watu wana wawakilishi wao hapa Tanzania ambao ni wafanyakazi sehemu mbali mbali katika mikutano hii nao huwa wanakuja lakini kwa majina tofauti hawataki watambulike .

  Niliuliza swali hizo biashara wanazofanya zinatambulika vipi na serikali pamoja na ummah wa watanzania ? je serikali ina tambua kuhusu ujuo wao hapa nchini na biashara wanazotaka kufanya ? wakakimbilia kuvunja mkutano tukapewa magazeti ya biashara zao na namba za mikono ya wawakilishi wao hapa Tanzania .

  Hiyo haikunishitua sana wakati natoka nikapiga simu kwa mmoja wa wawakilishi kuuliza mfano nikinunua bidhaa zao si nimefanya biashara ? kodi nalipaje ? pia ninatambulikaje ? natoa risiti za aina gani kwa mteja wangu ?

  Na hivyo vifaa vya mawasiliano je tume ya mawasiliano inajua chochote kuhusu suala hili ? sasa hata wawakilishi wenyewe sio watu wa mawasiliano lakini wanauza vifaa hivi kama simu na bidhaa zingine za afya za binadamu na wenyewe hawana utaalamu wowote wa utabibu wala nini

  Wahusika waangalie maswala haya kwa umakini sana , nawaomba vijana au mtu wowote yule kama amealikwa katika mkutano wowote ule usioeleweka katika mahoteli na sehemu zingine basi atoe taarifa katika majukwaa ya mtandao ili watu hawa waweze kufuatiliwa na kudhibitiwa

  Utakuwa umeokoa watanzania wenzako ambao wangeweza kuingizwa mkenge au watanzania wenzako ambao wangeweza kununua bidhaa hizo za afya na kupata matatizo zaidi na serikali pia ambayo inakosa mapato yake stahili
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kwanini usiende Polisi au unataka nani afuatilie?
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Hilo swali wamuuliza Shy, au mwandishi wa hiyo habari?
  .
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Oct 21, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kopy nimeshatuma kwa wahusika wengi naamini watafuatilia vikundi hivi vya wafanyabiashara kazi yangu ni kutoa taarifa tu kwa watu wawe makini
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Shy, hii ni habari nzito ya kufuatilia kwa karibu. Ila hujaiweka wazi sana. Tupe details zaidi na wahusika wa hapa ambayo wanatumia majina fake wawapo katika shughuli za wachina hao.

  Pia ummediately ulipoona kuna utata ungepiga simu polisi defender linakuja pale kabla ya mkutano kutawanyika. Au ungechukua another step uwafuatile ufahamu ofisi zao zilipo Dar au hata hotel walioshukia.

  Kuna biashara nyingi haramu za bidhaa kwa Sasa toka India na China, hasa Electronics, madawa and medical equipments.
   
 6. M

  Mjasiliamali Member

  #6
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa kaka, ni kama bahari ukijisikia kuogelea we'chojoa tu! Hawa wahindi wamejazana kilakona na wamefungua bank yao lakini kule Mumbai Mtanzania anaweza kufungua bank Kirahisi kama hapa? Hiini nchi isiyo na wenyewe bwana!.... na hata pale kariakoo wapo wahindi na wasomali wame jaa kibao wanaishi kama molecule in air! lakini je makwao unaweza kufanya hivyo? ....Uhamiaji kuna matatizo, na jeshi zima lapolisi lina matatizo kwani sasa lime kuwa si lile la enzi za Mwalimu tena kwani hata nidhamu hakuna, na kama nidhamu hakuna, utendaji unakuwa mmbovu, mfano mimi nakumbuka wakati nikiwa mdogo, yaani mtu kutamka lugha chafu ni kitu cha ajabu sana, na katika usafiri,mfano utaona sikuhizi konda wa daladala anatukana polisi akiwa hapohapo katika gari lakini hata hashtushwi, lakini kipindi kile, askari ata acha safariyake na kukuchukua kituoni hivyo kulikuwa na nidhamu, hii ni kuonesha ule utendaji katika jeshi la Polisi, lakini leo ikiwa wana ona matusi nikitu chakawaida basi hayo mambo ya Uhamiaji wawata yaweza!
   
 7. M

  Mjasiliamali Member

  #7
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sivyo kaka HIzo defender zinakuja kwamikwara tu wataondoka nao kisha baada ya siku chache, watuhumiwa wata achiwa, hivyo, wahindi wapo na wana saidiana kutoa hongo. na ndio maana wana watesa dadazetu na kakazetu pindi wanapo fanya kazi kwao kwani wanajua watahonga tu!
   
 8. M

  Mjasiliamali Member

  #8
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MSAADA WA USHAURI, Serekali iandae vijana wenye uzalendo na wanaojua kuwa wanataka kwenda katika majeshi kwa kujitolea na SI' MAJESHI YAWE MAHALI PAKUKIMBILIA VIJANA WASIO NA AJIRA,
   
 9. M

  Mjasiliamali Member

  #9
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Narudia tena kaka hao polisi nichanzo kwani hizo bidhaa zipo kariakoo bado zina ingizwa na wakija watapata mshiko wao na kuondoka, hivyo kama nikweli wanataka watoe tamko rasmi kisheria kuweka siku za kumaliza hizo stoc' ambazo zisizo isha za vifaa, na malighafi bandia,ili waanze operation ya kuzi angamiza.
   
 10. M

  Mjasiliamali Member

  #10
  Oct 21, 2008
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MTAZAMO USHAURI....Serekali, lazima itambue kuwa kushindwa kwa viwanda hapanchini ndicho chanzo cha kuingizwa malighafi zisizo na viwango sahihi, na kutowapa wananchi elimu za uzalishaji mali zenye ubora wa kimataifa ndio una fanya hata kazindogondogo, zina ingiliwa na wageni, na kuto wapatia elimu inayo stahili katika jamii ndio kuna zusha tafarani, kwani,HATA MAPROFESOR'S wetu wanashindwa kutunga mitaala itakayo kidhi mahitaji ya ki'ulimwengu!...Mfano...Kuna wanafunzi wanao maliza elimuzao zajuu hata hawa hawajui ni nini chakufanya kwani hawajui kubuni miradi,wanacho jua ni kungoja kuajiriwa na wahindi na wazungu hivi serekali ina jua kuwa ina walea vibaya wanachi wake, kwa mtaji huu, hatuto jitegemea hata kidogo kwani tuta subiri kuajiriwa na wazungu mpaka mwisho, KUHUSU VETA wana jitahidi sana. Ila wana toa elimu isiyo weza kumuwezesha mzalishaji kuzalish kwa kiwango cha kimataifa hivyo.
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kabisa ndugu yangu,,,,
  Hawa jamaa zetu haswa wahindi, wana kiburi sana, na sijui wanapewa na nani hiki kiburi. Saa ingine nakubaliana na mawazo fulani kuwa njaa ndo inayotusababishia haya.
  Nina mifano miwili ya kweli kabisa
  1. Kuna jamaa yangu alikuwa akifanya biashara na Wahindi na wazungu fulani, baada ya biashara kuchnganya, mhindi na mzungu wakala njama ya kumdhulumu huyu mtanzania. Wakampigia kura ya kutokuwa na imani naye (according to article of memorandum nanavyosema). Wakamwandikia barua ya kumtoa kwenye kampuni. Jamaa akatafuta wakili akamweka. Wakili akaandaa kesi kama inavyotakiwa, lakini huku nyuma akaenda kwa wadaiwa (defendants) akawaambia nia ya kuwafungulia kesi ya madai walichompa ni kitu kidogo,,,, advocate akaanza danadana ni leo ,,, ni kesho mpaka sasa haijafunguliwa hiyo kesi,,,, hi ni jaa na ndo dharau zinatokea.
  2. nilikuwa office moja ya wahindi,,,, driver akachelewa kazini,,, analalamika kuwa ni mgonjwa,,,, mama wa kihindi akaja juu kama kifuu,,, akamchapa makofi bwana mdogo yule na kumwambia kuwa nyie waafrika ni wajinga sana hamna akili,,,, at the sametime I was going to hire a car from them,,, then all of sudden an indian girl calling we are fool africans. Iliniuma sana nikamshauri yule kijana aende police,,,, wapi bwana mhindi alipigiwa simu akasema atakuja baadae. Nilichukua namba za simu za yule kijana nikamwuliza ilikuwaje na kama nahitajika kutoa ushahidi, anasema kuwa alifukuzwa kazi siku ileile mbele ya askari polisi.
  Haya yote yananifanya niamini kuwa njaa zetu (sio wote) ndizo zinatufikisha hapa.
  Mhindi ama mzungu anapojua kutoa kitu kidogo ni hatari sana kwa nchi yetu.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nilishalisema hili na nalirudia tena.
  Wahindi ndio wachawi wetu kwa mambo ya ufisadi.
  Chanzo kikubwa cha ufisadi katika nchi hii na nchi nyingine nyingi wewe sikiliziakama si wao!
  Hapa hakuna case ya ufisadi inayochomoka bila ya kusikia imekuwa initiated na mhindi.
  Kila mahali wahindi ni shida nakwambia. Tena wanaushirika sana mmoja wao anapokamatwa wale walio na influence kwa viongozi wetu waliojaa njaa hawa ndio utoa rushwa.
  Mimi pia nina mifano wazi.
  Nilikuwa naendesha tax. Nikakodiwa na kijana wa kihindi kumpeleka mji fulani. Alikuwa ana mabinti wawili wa kihindi pia. Kumbe alikuwa nawatorosha. Tulipofika mji fulani kabla ya kufika mwisho wa safari yetu tukakamatwa na askari waliokuwa wameweka vizuizi kwa ajili hiyo.
  Tukapelekwa kituo cha polisi na kuwekwa ndani. Lakini punde akatokea mhindi mmoja wa mji ule akapata habari kuwa kuna wahindi wamekamatwa na akatutoa rumande na tukalala kwake baada ya kuzungumza vizuri na OCD.
  Kesho yake tukarudi polisi na wakaturudisha mjini kwetu kwa escort.
  Tulipofika mjini kwetu tu tulikuta wahindi wengi sana pale polisi, pia na jamaa zangu wakiomba tudhaminiwe. Mimi nikawekwa ndani na wale wahindi wakaachiwa kwenda kulala nyumbani. Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kwa nini mimi nisiachiliwe ila staff officer ambaye alikuwa kashikia bango kesi ile alisema mimi niendelee kubaki mahabusu.
  Mungu ibariki kesho yake niliachiliwa na kesi ikaondoka upande wangu.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,206
  Trophy Points: 280
  pole Shy, ulitakiwa kuhudhuria zaidi hiyo mikutano upate mwanga zaidi. Kwa kukusaidia hiyo ni biashara ya Bio Disc. Ni biashara kama GNLD na Forever Living, hazihitaji daktari kama kuuza hedex. Mambo ya kodi ndio sijui.

  Nikirudi kwenye hii Bio Disc inalinda afya yako kwa kutoa miale ya nishati ya uzima iitwayo Life Force inafanya kazi ya chakra balancing kwenye mwili wako hivyo kuzuia magonjwa na kukupa maisha marefu.

  Bio Disk moja inauzwa dola 600. Kati ya hizo dola 100 inarudi kwa aliyekushawishi kununua ndio maana utaona sio tuu unabembelezwa ununue bali pia-unatongozwa kwa viofer ofer vya mara lunch hoteli kubwa mara dinner ili mradi ufike bei.

  Hakuna haja ya kuwafuatilia watu hawa kwa sababu biashara yenyewe inafanyika kwenye internet.Tanzania haina sheria yoyote ya kudhibiti chochote kwenye mtandao ndio maana kila siku kuna malalamiko TRA na COTEKNA kuhusu bei poa za magari kwenye net. Kuna web site japan wanauza gari za mwaka 2000 kwa dola 300 tuu. Nimeagiza gari limefiika jamaa wamekataa sio 300 na internet haitambuliki!.
  Fuatilia kwa makini, fanya biashara utajirike. Polisi hawawezi TRA hawawezi kisa sheria hakuna!.
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,113
  Likes Received: 5,565
  Trophy Points: 280
  bora hao wanaiba kwa kuelimisha kuliko hao wahuni wa CCM walioingia serikalini na Pesa za EPA na sasa wanarushiwa mawe baada ya watu kuchoka!!!
   
Loading...