Hawa wafanyabiashara sio ndio Serikali hii iliwaita wapiga dili, wezi, wakwepa kodi? Na yale makusanyo yaliyozidi walitoa wapi? Uchumi si unakua?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Serikali haitakiwi kusaka mchawi usiku na mchana juu ya hali ya uchumi wetu,suluhisho lipo kwenye maandishi ya Sera na mipango ya Serikali suala ni utekelezaji tu.

1.Unakutana na Viongozi wa Chama na Serikali,unawauliza nini kinawafanya msitekeleze mkakati wa kutengeneneza matajiri wa ndani ili washike njia kuu za uchumi na hata tuwe na mkakati wa kuwa na matajiri ambao watatawala uchumi wa Afrika?unajibiwa hao ni wezi tu!😳

2.Unakutana na kiongozi wa Serikali ama Chama unamwambia ,Imarisheni sekta binafsi msiache zianguke kwa maana Sayansi ya uchumi imethibitisha bila sekta binafsi huwezi endesha nchi,wanakujibu hao sekta binafsi ni wizi tu.

3.Unakutana na Kiongozi wa Serikali ama Chama unamwambia uchumi hauendeshwi kwa kuwapiga kodi kubwa watu,unawaambia nadhari za uchumi hazisemi uendeshaji wa uchumi ni kodi,kodi,kodi.Wanakujibu wewe mpinzani,umetumwa kukwamisha maendeleo.

4.Unakutana nao na unawaambia,Nje huko watu wanafunga biashara na wengine wanahamisha mitaji yao kwa sababu ya sera zenu za kodi na mazingira yasiyo rafiki ya kufanya biashara,Unajibiwa,hao walikuwa wapiga dili hao wacha waende.

Maoni yangu baada ya mkutano wa jana.
1.Bila sekta binafsi imara hatuwezi yaona maendeleo tunayoyatamani.

2.Bila utekelezaji wa PPP,Serikali itabeba mzigo wa kuendesha nchi ambao haitaweza kufika nao mwisho,itaishia njiani.
 
Watu wengi sana wamesha athirika na Kauli za Mkuu wa Kaya ,hasa ukizingatia na Mfumo mmbovu wa Nchi wa kugeuza Kauli ya Mtu mmoja kuwa ndio Sheria.Mpaka ufike wakati wa Uchaguzi tutakuwa tume shuhudia mengi sana na ya ajabu ajabu.Ni mwendo wa kula Matapishi tu..
 
Wameshagundua wajinga wengi.
 
Hata Fastjet kapigwa vita na watu wakatetea!!

TTCL inabebwa watu wanashangilia!

TBA inapewa tender karibu zote za serikali na watu wanashangilia!!

Anaesimamia haya akibadili gia angani,watu wanashangilia!!!

Na haya ndio Maajabu ya Wananchi wa Tanzania ..
 
Hata Fastjet kapigwa vita na watu wakatetea!!

TTCL inabebwa watu wanashangilia!

TBA inapewa tender karibu zote za serikali na watu wanashangilia!!

Anaesimamia haya akibadili gia angani,watu wanashangilia!!!
Nchi imekua ya hovyo sana hii.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom