Field Marshall ES
JF-Expert Member
- Apr 27, 2006
- 12,624
- 1,233
JUST THINKING!
Pole pole inaanza kuonekana kuwa Wa-China, wanaweza kuwa ndio jawabu la waa-Afrika katika kupambana na ufisadi wa The West, katika kujikomboa kiuchumi. Biashara kati ya China na Afrika, imeongezeka kwa kasi kubwa toka mwaka 2001 hadi leo kufikia DOLA BILLIONI 40, kulinganisha na DOLA BILLIONI 15-20, katika mwaka wa 1999. China inafuata nyayo za waliowatangulia katika biashara hizo na Afrika, yaani kwanza Waarabu na baadaye The West, ambao waliweza kujenga Empire zao huko Ulaya kwa kutumia jasho na damu la Waa-Afrika, na baadaye kupigana nasi katika kugombea uhuru wetu, ambao baadaye walitupatia kwa njia za ujanja ambazo zimetuacha wa-Afrika kukwama kiuchumi, ambapo kazi yetu imeendelea kuwauzia the West vifaa muhimu kwa ajili ya maendeleo yao kwa bei ndogo, na kubaki soko kubwa la the West katika kuuza vifaa vyao vibovu au (Cheap manufactured goods).
Lakini Wachina wanaonekana kutupatia Waafrika, biashara na uchumi katika njia mpya ambazo ni staright business yaani za uwazi bila ujanja, na bila kuingilia siasa za ndani ya nchi zetu, ingawaje swali ni kwamba je ni kweli na wao hawana nia mbaya kama the West, waliokuja na Biblia wakatuacha tumeshikilia hizo Biblia zao mikononi mwetu, wakati wao wakigawana ardhi yetu? Ni swali linalowasumbua wasomi wengi wa nchi za Afrika sasa hivi.
Lakini kuna wanaosema kuwa wa-Afrika wanaweza kunufaika kwa kufuata busara za Wa-China ambao katika miaka ya karibuni tu wameweza kuwaondoa wananchi Billioni moja huko China, kutoka kwenye umasikini wa kutupwa, na kuji-Transform kutoka kwenye Agrarian backwater mpaka sasa hivi kuwa the world's fastest-growing economy! kufanikiwa huko kwa wa-china kumetokana na kuwa na viongozi imara katika siasa, ambao waliwapa viongozi wao wa uchumi uhuru wa kuamua maamuzi ya uchumi bila ya kuingiliwa na wanasiasa, kitu ambacho waa-Afrika tunaonekana kuwa kigumu sana kwetu kwa wanasiasa kuwaachia maamuzi mazito ya uchumi, viongozi wetu wa uchumi kina Kigoda na Mramba, ambao nafasi ya kwanza kwao ni kupeleka hela zote za bajeti katika majmbo yao ya uchaguzi!
Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha kuwa hata Wa-china nao wana shida moja kubwa na Afrika, nayo ni kuchukua Raw Material tofauti yao ni kwamba hawatuingilii siasa zetu au kuja na maneno ya kuja kufuta corruption, lakini pia historia inaonyesha kwamba njia zote za kujaribu kugeuza utajiri ili uwasaidie Wa-Afrika wenyewe, zimeshindikana na hasa ukiangalia nchi kama Nigeria, ambayo ina utajiri mkubwa wa mafuta.
Ukiweli ni kwamba Waa-Afrika, tunapaswa kuamua wenyewe kwani mambo yote yako mezani na uamuzi ni wetu either kuendelea kuwafuata World Bank, na IMF ambao umetuua kabisa kiuchumi na uzoefu wa wa-china, ambao ndio umewakomboa kiuchumi, uamuzi ni wetu!