Hawa Vijana Wa Kings Music Hakika Wameiva

Mkuu wanaimba kawaida sana hao jamaa '' halafu beats za nyimbo zao bado hazi toi ruksa ya wao kuweza kuliteka soko ..... ALI K anapaswa kubadilika
Basi sawa...
 
Mziki uliopo kwenye market ya sasa ni beats za latin America yenye mchanganyiko wa raga muffin ", kama uliisikia manyaku nyaku ya marioo " pia na beats za niger " . ... ndio maana mimi na wewe twaweza kuona nyimbo kama Aibu. Ya nandy" ikifanya vizuri " wet ya vanisa ikifanya vizuri " jibebe ya wcb ikifanya vizuri ".... Tatizo la ali k anaupenda sana mziki wenye mahadhi ya kongo " nimziki mzuri lakini kwa sasa hauna market kubwa africa
Basi sawa...
 
Kuimba sio kujua kuiremba sauti tu"... ni Melody kali yenye mchanganyiko wa sauti nzuri inayoamsha mpaka hisia uandishi " mzuri "unaogusa hisia pia ' na product nzuri toka kwa producer ... hapa kwenye product ndio kiungo nyeti haswaa " kwa sababu mpangilio wa vyombo vya music ukiwa mzuri huwa inamfanya msikilizaji achanganyikiwe ".... jaribu kusikiliza nyimbo ya lucky dube back to my roots mtaelewa nacho kiongea" Au kwa sasa jaribuni kusikiliza wimbo za patoranking " different na this kind love"..... kwa tz kuna ule wimbo wa harmonies Dm chick ..
 
Beat za Ali Kiba ni zile zile hazibadiliki alafu haziendani na mahitaji ya Sasa, video iko na ubora mzuri tatizo sauti za vijana wa KINGS MUSIC zimefanana na Ali Kiba mwenyewe kwaiyo kwa mtu aliye nje ya nchi anaweza akajua ni Kiba ndio kaimba mwanzo mwisho.

Tumshabikie mtu lakini tumwambie ukweli asije akaamini yupo sawa kumbe anapotea, Kwenye hiyo LEBO mtu mwenye utofauti ni Nedy Music Peke yake
 
Back
Top Bottom