Hawa paka wanaofugwa siyo viumbe wa kuwaamini kabisa

badison

JF-Expert Member
May 29, 2015
1,450
2,702
Nilisha zungumza kuhusu hawa wanyama wafugwao kwamba, siyo viumbe halisi, hawana nafasi, in short ni GMO.

Sipendi paka mimi wala sitaki kukaa nyumba yoyote ya mtu anayefunga paka. Kwa kweli paka siwapendi, akikuangalia kama anakusoma hivi, ana macho flani ya kijizi.

Embu ona yalivyo jaa huku mtaani na yanalia usiku, yani ni usumbufu kila mahali. Hata dukani nikienda nikamkuta muuzaji na kuna paka hapo dukani, sinunui kitu hapo naondoka.

Hata wanga huwezi kuwatofautisha na paka. Kwani wanga wanapenda sana kutumia umbo la paka. Popote nionapo paka naondoka haraka huwezi jua ni paka kweli au paka mtu.

Yani hawa wanyama paka cha kushangaza hata baa yapo, sipendi baa zenye paka sana. Ni bora niondoke kwa kweli, siwezi kumpa paka hata mfupa. Ninamfukuza popote nikimuona. Kwakuwa najua haya mapaka yana akili timamu kabisa kama watu. Na pia paka hasahau mtu na pia ni myama mwenye kisasi sana. Ushauri wangu, kaa mbali na nyumba yenye paka.
Screenshot_2022-09-04-11-25-55-818_com.twitter.android.jpg
 
Mwanadamu hasa mwanaume ndiye Mtawala wa Dunia.

Sasa Kama Mwanaume unaogopa tuu Paka Kwa kweli inashangaza.

Paka ni kiumbe Kama viumbe wengine, ingawaje Attitude yake ndio wengi hawaipendi, attitude ya kujiona yeye ndiye Boss.

Hata hivyo Kwa wenye akili Hilo haliwasumbui.

Raha ya nyumba awepo paka, nje awepo Mbwa
PAKA sio kama VIUMBE wengine mkuu. Mkamate PAKA mrushe juu Sana akitua chini atakuwa kasimamia miguu yake yote minne.
 
Tabia za paka:
Paka upokea tabia zako na ndio hatakavo kuwa alivo.mfano ukienda nyumba za watu ukakuta paka alafu ukiona paka ana mambo ya ajabu ajabu,mazuri,mabaya basi tambua huyo paka tabia zake katoa kwa mfugaji wake na mfugaji wake ndio tabia zake.

Paka hana tabia ya kutozea watu labda wale anaokaa nao na kumpa maitaji.

paka anaweza kukutafakari na kujujua wewe ni mtu wa aina gani na uchukua mda sana na ikiwezekana hata kukujaribu kwa kukuchokoza,kuja miguuni mwako,kuomba urafiki na n.k.

paka kii imani inakadiliwa ndio anayeweza kuona kifo cha mwadamu ni mda gani sema japo kuongea wala ishara ngumu.

paka uwezo wake wa kuona ni mkubwa usiku kushinda wanyama wote yani yeye usiku ni kama mchana.

Paka ukimtupa porini hakiwa mdogo ukamuacha huko mpaka hakuwe basi ukirudi sio paka tena kashakuwa mnyama hatari anayeweza hata kukamata mbuzi .

Paka anapenda umwinyi sana ,starehee na maisha mazuri sana .
unaweza kushangaa hotelini hawa kahuki sababu ya mapocho pocho mazuri.

Paka anapenda familia inayomfuga
 
PAKA sio kama VIUMBE wengine mkuu. Mkamate PAKA mrushe juu Sana akitua chini atakuwa kasimamia miguu yake yote minne.
Haaahaaha akili za stone age hizi...ndio maana mkawa mnajifukiza eti kukinga covid na sasa hivi mnapigwa sindano tuu kama kawa ....chezea sayansi wewe. Paka ni mnyama kama wanyama wengine. hata hao akina cheeter, leopards, etc hao wote ni paka tuu.
 
Paka ni kiumbe kwenye uwezo wake wa kipekee, ukifanikiwa kutengeneza urafiki naye atakusaidia makubwa usiyoyajua na unayoyajua, yakuonekana na yasiyo ya kuonekana.
Kwa mfano tangu utotoni tumekuwa tukiaminishwa paka mweusi ni wabaya, lakini katika kuchimbua Elimu za wahenga nimekuja kugundua paka mweusi ni mlinzi dhidi ya maroho machafu, wachawi na pepo wabaya japo imekaa kiimani imani ila ndo hivyo mtu mwema usipomtumia kwa ulinzi wabaya watamtumia kwa uovu.
Hivyo ukiona mtu anafuga paka mweusi usimuone mwanga bali anajilinda dhidi ya wanga wasumbufu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom