Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Mtoa post unaonekana kabisa wewe ni mdini lakini hata dini yenyewe huna ujuzi nayo, katika hao wote uliowaorodhesha hapo juu hakuna aliyehukumiwa na huyo mungu kwasababu ya kumdhihaki.

Labda nikukumbeshe kitu kimoja, kifo sio adhabu kwa maana huyo mungu mwenyewe kupitia maandiko yake kasema kuwa kila mtu kapangiwa siku yake ya kufa.

Sasa ikitokea leo mimi namdhihaki alafu anihukumu kwa kifo hapo ataonesha wazi kuwa hana msimamo, pia fuatilia alichokisema mkuu SCARS kwenye comment ya #3.

Sio ukristo tu hata uislamu utakufa, kadri siku zinavyokwenda watu wa dini wanaachana na hizi dini baada ya kugundua kuwa hizi dini ni za michongo.
kwa kweli za mchongo lol.
 
Religion is Opium,
Yaani ukiwa mfuasi wa Dini lazima ukubali kua nyumbu,hivi Hawa watu wamefungwaje akili,mbona Mimi naona Kabisa Dini na Imani za Mungu,miungu,mashetani,
mapepo,mizimu,majini nk ni propaganda tu ila still Watu Bado wanaamini tu!
Daaaa Mimi nimeshindwa Hata Kwa kujilazimisha!
Aiseeeh mie pia nimeshashindwa hata kujilazumisha kukubali huo ufuasi wa dini.
 
Hapa kuna funzo kubwa sana, Nami nitaongezea kisa kimoja nilichopata kusimuliwa na watu ninaowaamini.
Miaka ya hapa kati (2010-2015) kanisa moja la Anglican tena ni kanisa kuu la diocese lilikuwa linafanya sherehe za kutimiza karne moja tangu kuanzishwa kwa diocese hiyo, moja kati ya diocese kongwe hapa Tanzania.
Basi Siku hiyo kulikuwa na maandamano ya waumini na viongozi wa kanisa kutoka mahali ambapo ndipo palikuwa na kanisa la kwanza kabisa la dayosisi hiyo mpaka lilipo kanisa kuu la sasa ambalo nalo ni la zamani sana.
Basi maandamano yalikatiza mitaa ya katikati ya mji wakiongozwa na kiongozi wa maandamano aliyebeba MSALABA mkubwa wa mbao.
Waandamanaji walipofika maeneo ya katikati ya mji akatokea bwana mmoja aliyekuwa mchukuzi maarufu wa maeneo hayo kwa jina maarufu CHENGO, basi yule bwana CHENGO alicheka kwa kejeli na kutoa maneno ya kuudhihaki msalaba, alizidi kutoa maneno machafu kwa Waandamanaji na juu ya ule MSALABA MTAKATIFU.
Baada ya maandamano kupita na kuisha katika maeneo yale yule bwana alipata ajali ambayo mpaka leo hakuna ajuaye BWANA CHENGO aligongwa na chombo gani. Hakuna gari iliyoonekana kwa macho ikimgonga lakini ndiyo hivyo yule bwana akapoteza uhai siku ileile tena muda mfupi baada ya kuunanga MSALABA MTAKATIFU

Tuweke akiba ya maneno
Hakna lolote n uongo mtupu,
 
Nitwaminije ya kwamba Hii kweli na si chai,je tutajuaje kama wale Watu wa Dini walimfanyia tukio Ili ionekane eti aliukashifu msalaba na amepigwa tukio na huyo Mungu,
Kisa chako kina walakini kwanza Mimi najua mbinu za hao wanaojiita watu wa Dini kutengeneza matukio Ili kuwatisha na kuwahadaa watu na Hapo wakiita ni miujiza,
Kwangu Mimi hilo tukio naona ni coisendence ya kawaida tu au Kuna figisu alifanyiwa huyo bwana ila swala la kusema ni laana au sijui miujiza nooop!
Umemaliza kabisaaa, ndyo ukweli wenyewe.
 
watu wasomuamini mungu hua na mtindio wa ubongo, mungu amekua jawabu la mambo mengi ambayo science wanayoitukuza imeshindwa, mfano; vipimo na matibabu ya kisayansi yanamwambia mtu hawezi kupata mtoto isipokua kwa kupandikiza bt ukija mbele za mungu utapata mtoto bila hata kupandikiza.
huu ni uongo wa wazi kabisaa, nyie wafia dini hapana kwa kweli. Khaaaah
 
Ngoja nijibu maswali yako

1. Mimi ni mtu naye tambulika kwa majina matatu niliypewa na wazazi wangu

2. Kabla ya kuwepo, sikuwepo. Kuuliza mahali nilipokuwa wakati sipo ni contradiction

3. Hapa nipo kwasababu ya juhudi zangu za kjjiepusha na hatari zinazoweza kufanya nisiwepo, nipo hapa kwasababu cell zangu hazichachoka. Kwa hiyo hakuna nguvu yeyote inayonisukuma

4. Nikitoka hapa kwa namna gani? Kama una maanisha kufa, basi jibu ni simple, kilichokufa hakiwezi kufanya movements yeyote ya kwenda sehemu nyingine, labda kama unakusudia kuzikwa

Kwa hiyo hayo maswali ulivyokosa majibu ndio yalikusababisha mpaka ukaamini Mungu?
Ewaaaaaaaah.
 
acha kutishia nyau mtu mzima bwana mkubwa zile zama za uongo uongo,maigizo,ndio Mzee,Amen nk zilishapita tunataka fact hapa sio hekaya za kiyahudi na kiyunani katika civilization ya Digital, Science and technology hivyo vitisho mlishavifanya Kwa kina
Galileo Galilei zama hizo za dark ages!
mbavu zangu mie lol.
 
Back
Top Bottom