Hawa ni watu (public figures) watano ambao Taifa linapaswa kujivunia

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,042
2,000
Katika jamii yoyote ile ni lazima kuwe na watu ambao Taifa linapaswa kujivunia nao. Kwa taifa Leo tumejaaliwa watu wengi ambao tunajivunia nao, Ila kwa Leo nitawazungunzia watano. Kumbuka hakuna binadamu asiye na mapungufu, hivyo suala la mapungufu liweke kando kwanza kwa kuwa hakuna malaika.
Hawa watu wana akili sana na inakupasa uwe na akili sana kuwaelewa, ile kwa wale hoyahoya hawawezi kuelewa.

1) Paul Makonda "Field Marshall"
- siku moja uzeeni huko tutakuja kusimulia kuwa kuliwahi kuwa na kijana mmoja shupavu sana na jasiri sana ambae haogopi. Kwanza akiwa anazungunza Jambo basi hata kama ulikuwa na shughuli zako utaacha na utaanza kumsikiliza. Kwa kifupi ana sauti ya mamlaka na ushawishi mkubwa sana. Nathubutu kusema kwa East Africa sijawahi kuona mtu mwenye ushawishi kama Paul Makonda. Hali iliyopelekea hadi watu kuanza kumuita Field Marshall. Ana akili sana na Mara nyingi huwa anakuja na mbinu ya kutatua tatizo katika jamii inayomzunguka. Huyu ndio "the most fearless person in Tanzania"

2) William Malecela "Le Mutuz"
- Ana degree tatu kutoka majuu, huyu ni moja ya watu ambao ni underrated sana Ila ana madini kuliko kawaida. Ana akili nyingi sana na anatumia akili kubwa sana kwenye kufanya au kuamua mambo mengi ambayo yanaonekana ni kama controversial.
Lemutuz anatumia muda na akili sana kwenye kuongea, kujadili au kuandika Jambo lolote. Huwa hakurupuki na ana ushawishi mkubwa sana kwenye social media. Watu wa hivi huwa wanapaswa kutumiwa sana kwenye issue yoyote ya kijamii ambayo ipo controversial.

3) Nikki wa Pili
- Kwa mara ya kwanza alianza kuonekana kwenye masuala ya muziki wa hiphop na huko akafanya maajabu aliyofanya. Ila kubwa ni pale alipoanza kushiriki kwenye shughuli za kijamii, Nikki ametumia muda mwingi na akili nyingi sana kusaidia jamii.

Ana akili sana, ukimsikiliza na akiandika kitu basi huwezi kutoka hivihivi lazima kuna jambo utalipata. Nikki amesadia vijana wengi pale alipokuwa akitumika kwenye "fursa" iliyoendeshwa na clouds media kwa miaka mingi sana. Hivyo watu kama hawa wanapaswa kutumiwa zaidi ya hapa.

4) Alberto Msando
- Ni mwanasheria nguli sana katika hii nchi, nathubutu kusema huyu kwangu ndio mwanasheria bora kabisa ukanda huu wa East Afrika. Hii inatokana na uwezo wake mkubwa sana na wa akili sana kwenye kushughulikia jambo lolote unalojua. Alberto ni mtu ambae akitumika miaka mingi basi taifa litafaidika sana na yatupasa kumtumia sana.

5) Steve Nyerere
- Huyu ni moja ya watu ambao wamekuwa viungo wakubwa sana kwenye jamii na taifa. Ana akili kubwa sana ya kuorganize jambo lolote gumu katika taifa. Ni mchekeshaji Ila ana akili sana, kama una jambo lako gumu basi mtafute huyu bwana Hilo jambo litakuwa jepesi sana na kwa mafanikio makubwa.

Screenshot_20210704-185745_1.jpg
Screenshot_20210704-193248_1.jpg
Screenshot_20210704-193331_1.jpg
Screenshot_20210704-193008_1.jpg
Screenshot_20210704-193351_1.jpg
 

nduza

JF-Expert Member
Feb 7, 2019
1,230
2,000
Namkubali Nikki kuna wengine humo ambao ni smart lakini siyo kwa kiwango hicho cha taifa kwa Makonda umechemka siwezi kumpa hata mwenyekiti wa mtaa kama nikiwa kwenye nafasi ya kuamua hilo.
 

Snowden E

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
540
1,000
Hakuna hata mmoja hapo anayenizidi, ila wao wanacheza na media tu ili wanacho kifanya kionekane.

Amini nakwanbia.
 

MARTIAL20

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
324
1,000
PUBLIC FIGURE maanake ni nini? Basi kama ni hivyo muongezee na IDRISS SULTAN kabisa kwenye list yako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom