Hawa ni watanzania wenye mvuto zaidi na wasio na mvuto kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ni watanzania wenye mvuto zaidi na wasio na mvuto kabisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Observer2010, Apr 5, 2011.

 1. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ninaposema mvuto hapa simaanishi wa sura, bali watu ambao jamii kubwa ya Watanzania inawakubali sana kwa kipindi hiki, hawa ni watu ambao wakijitokeza kutoa kauli zao zinaheshimika na kusikilizwa na Watanzania walio wengi.

  Hawa wengine ni wale waliopoteza kabisa kukubalika katika jamii kubwa ya Watanzania na wanaonekana kama ni watu wasiopendwa kabisa nchi hii, hata wanapozungumza jambo lolote watu wanawapuuza kabisa.

  Watanzania watatu wanaokubalika zaidi.

  1. Mchungaji Ambilikile Mwasapile.

  Miezi michache iliyopita, hili jina lilikuwa halifahamiki kabisa, ila kwa yale yanayoendelea huko Loliondo, babu amegeuka kuwa lulu kwa Taifa. Babu kwa sasa ni mtu ambaye anatengeneza headlines nyingi zaidi katika vyombo vya habari kuliko mtu yoyote ndani ya nchi hii kwa sasa. Habari zake ndizo zinaongoza kwa kusomwa katika magazeti kwa wakati huu, na nyumba yake ndiyo inaongoza kwa kupokea wageni wengi zaidi kwa wakati mmoja katika historia ya nchi hii. Hana makuu, na ametokea kuwa ni mkombozi wa wengi.

  2. Dr Wilbrod Slaa

  Kabla ya kuibuka kwa babu, Dr Wilbrod Slaa ndio alikuwa ni mtu anayeongoza zaidi Tanzania kwa kuwavutia walio wengi. Hoja zake za msingi, uimara wake katika kutetea maslahi ya Taifa na Watanzania wengi walio katika hali duni ya kimaskini na pia ujasiri wake wa kuzungumza pasipo uoga wowote vimemfanya awe ni mtu wa kipekee sana katika hii nchi.

  3. Samwel Sitta

  Kama kuna watu wachache ndani ya CCM wanaokubalika kwa sasa katika jamii ya Watanzania walio wengi basi huyu ndio anaongoza. Amekuwa imara sana katika kutetea maslahi ya taifa toka alipokuwa Spika, japokuwa siku za mwanzoni mwa Uspika aliteteleka kidogo ila baadaye akasimama imara. Hajaonesha kurubuniwa kwa kupewa uwaziri, bado amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia yale anayoamini ni maslahi ya Taifa. Kupigwa zengwe kwake kwa kuondolewa katika Uspika kuliwasononesha watu wengi sana.


  Na hawa ni Watanzania wasiokubalika zaidi na kila wanayoyafanya yanaonekana ni kero kubwa sana kwenye jamii.

  1. RA

  Ni Mtanzania anayeongoza kwa kashfa nyingi za kifisadi, popote palipo na harufu ya ufisadi lazima jina lake liambatanishwe. Hela zake nyingi zimekuwa ni kero kubwa kwa Watanzania, amejaribu kununua vyombo vingi vya habari ili kujisafisha lakini bado hajaweza kurudisha imani ya WaTz.

  2. YM

  Maneno yake mengi ya kejeli na kashfa yamekuwa ni matusi kwa Watz. Huwa ni mtu anayeonekana ni mlopokaji muda wote na asiye na staha kabisa. Kutokuwa kwake makini katika mambo mengi kumefanya chama tawala kipate ufa mkubwa zaidi katika historia ya nchi hii.

  3. EL

  Huyu amekuwa akiambatanishwa na kashfa nyingi sana za kifisadi km RA. Juhudi zake kubwa za kujisafisha bado hazijawarudishia imani Watanzania. Hawa ndio mzigo mkubwa kwenye uongozi wa nchi hii na chama tawala. Amewekeza nguvu nyingi sana kwa ajili ya 2015. Asilimia kubwa ya Watanzania walio katika hali ya kawaida hawataki hata kumsikiliza.  :ranger::ranger: :peep::peep:
   
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sijui umewaza nini ila nakugongea senksi
   
 3. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  upo mbali sana,
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna hata mmoja mwenye mvuto hapo.
  Babu kasababisha watu wengi wamepoteza maisha huko kwa kutoa dawa isiyoeleweka. Eti inatolea mahali pamoja na mtu mmoja na haihamishiki na pia kudanganya inaweza kutibu magonjwa sugu.
  Dr Slaa; Huyu yupo in between. He has done goods and bad for his country. Kafichua saana ufisadi na amejitahidi kuwa mkweli, tatizo personal attributes zake hazilingani na ukweli na haamini kwenye kushinda.
  Samwel Sitta. He was good. Lakini sasa hivi anajifanya kukosoa mfumo unaompa maslahi. Kama anaweza atoke huko.
  RA; Licha ya kwamba hajapatikana na hatia yoyote, hajafanya jitihada za kujisafisha na tuhuma zinazomkabili.
  YM: Ohpss hachagui cha kuongea na huenda huwa hatafakari kabla ya kuongea
  EL; Huyu ni mchapakazi kweli lakini tatizo anavimeritis ambavyo ni ngumu kuviacha, km hana basi atoke hadharani ajisafishe kuliko kuwa kimya
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  kipi kipya hapa?
   
 6. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  sijui watu nyie physically mukoje? Umeanza kwa hamna yeyote,alaf kwa maelezo yako mwenyewe ukamsapoti mleta mada kwa kujadili kadri ya alivoelekeza. Anyway mi sitoi mchango kwa ili.
   
 7. Ibrahim K. Chiki

  Ibrahim K. Chiki Verified User

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mi naona mmoja tu, Dr wilbroad slaaa, wengine wote tupa kule.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huyu EL na wapambe wake wanajitahidi sana kujisafisha ili awe mgombea wa CCM kiti cha urais 2015; ukweli ni kwamba kama ccm itafanya kosa hilo wajue wazi kwamba itakula kwao na mgombea wa upinzania atapeta!! Angalizo ni kwamba 2015 hakutakuwa na uchakachuaji!!
   
 9. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Babu ameleta tumaini lililokwisha kupotea miongoni mwa Watanzania. Wengi wanamponda kutokana na wivu.
  Dr. Slaa amefanya mengi ambayo wengi wamekuwa wakiogopa kuthubutu.
  Sitta,amekuwa role model kwa kuweka maslahi ya nchi mbele.
  RA,ana kashfa zisizofutika na amekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo Igunga.
  EL,Huenda akawa mtu safi ila hakusoma alama za nyakati vizuri.
  JK,ni raisi aliyefeli kwa kiwango cha juu zaidi.Huenda hakustahili nafasi ya pili. Wananchi kukimbilia loliondo ni matokeo ya ubovu wake.
  Ngeleja,ingekuwa uongozi ni filamu basi angekuwa perfect vilain.
  James Mbatia, hafai kumwamwini hata kidogo,hana sifa za uongozi,he is just another pupet.
  Lyatonga,ukiacha pembeni undumakuwili ni mchapakazi hasa ila hafai kuwa mfano wa kuigwa.
  Anne Makinda,hasara kwa nchi ukichukulia anaongoza mhimili wa serikali huku akiwa na mahaba kwa chama na kutaka kulipa fadhila.
   
 10. B

  BENTA Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wewe ujumbe umefika sasa tusonge mbele.
   
 11. Gold Digger

  Gold Digger Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is garbage analysis, with the exception of Dr Slaa
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Kikwete sura nzuri sana kwa hiyo anamvuto pia.............
   
 13. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  .... YOTE MIJIZI TU!
  Cha ajabu sana na cha kusikitisha ni kwamba bado hii mijizi na wengine wa aina yao ndani ya Chama chao wanao wafuasi lukuki.
  Ndio, Ujinga uliokithiri ni pamoja na sababu na visingizio kibao ukiacha ukweli kwamba wote hawa na wafuasi wao wengi ni WASWAHILI tu! Adui namba 4
   
 14. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  :crazy: wewe nenda Loliondo
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Pumba hizoooo.
   
Loading...