Hawa ni wapigania demokrasia

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,586
1,678
Imenijia fikra kuona jinsi gani wakati una uwezo mkubwa wa kugeuza kila kitu: fikra, madhehebu na hata hulka za watu. Hapo zamani Watanzania- miongoni mwa watu wote wa Afrika Mashariki- ndio waliokuwa wakisifika kwa uchapa kazi na uaminifu. Tazama hii leo! Hayo tuyaache. Napenda kuzungumzia juu ya fikra ya uhaini na upigania demokrasia. Kwa wale ambao wamezaliwa baada ya miaka ya themanini pengine hawajui kuwa hata Tanzania imepoteza wana wake mashujaa katika kupigania demokrasia. Ila kwa msamiati wa wakati huo, hawa walikuwa wanaitwa wahaini. Watu kama marehemu Tamimu ambaye kila alilotaka ni kuwa Tanzania iwe na mfumo mwingine wa siasa na sio siasa ya ukandamizaji na kuguguna uhuru wa watu. Huyu aliuawa kwa kupigwa risasi. Kuna wengine walipata bahati na kuishi, ingawaje kwa taabu, akina Bi Titi Mohamed, Kambona na hatimae vijana akina Yasin Memba.
Kwa kweli umefika wakati wa kusafisha majina ya watu hawa na kuwatoa katika kundi la wahaini na kuwaita wapigania demokraasia, kwani wakati umegeuka. Wadhania akina marehemu Tamimu angeendesha kampeni zake wakati huu angeitwa mhaini?
Kwa kweli mimi binafsi simwoni mhaini mtu yeyote anayetaka kuleta mabadiliko katika nchi ambayo hakuna nyingine ya kuleta madadiliko kwa amani- hata kama ametumia mtutu wa bunduki.
 
Kwa Tanzania watanzania wa sasa wamejifunza mengi kutokana na hawa waasisi wa vuguvugu la haki na utawala bora . Watu wameamua kujichotea mafursa na mihela kwani kujifanya mfurukutwa unaishia kufurukutwa. Tazama kilichompata Tamim(RIP), alitandikwa risasi na afisa wa serikali ambaye kwa sasa anajifanya kinara wa demokrasia. Yasin memba alinyongwa namakachero wa serikali alipojifanya anataka kurudi tanzania kushiriki katika mageuzi. Mapalala aliishia kuteswa na kukaa gerezani na hatimaye kuporwa chama chake na watu wanaojifanya ni watetea siasa bora. Ndo maana sasa mwendo ni mmoja tu - chukua chako mapema.
 
Back
Top Bottom