Hawa Ni Wanandoa Ama Ni Wahuni Wanaoishi Pamoja?

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,676
Watu wanajiita wanandoa lkn kila mtu ana mambo yake.

Mke kutwa kwenye mitandao akichat na mabwana, hali kadhalika mume kutwa anachati na mademu. kwann mliingia kwenye ndoa?

Mko kwenye ndoa lkn mavazi yenu na maongezi bila kusahau kampani zenu bado ni za kihuni. Badilikeni.

Mkitoka kwenda sehemu hata mkiwa kwenye gari yenu binafsi njia nzima hamuongei. Mlilazimishwa Kuoana?

Wanandoa gani mumejawa jazba usoni? Hamtaniani hata kidogo?

Kosa dogo tu mtabwatukiana mpk mtaa mzima ujue na kurekodi kwenye simu zao. Ama mtatwangana mpk mmoja alale kwa mjumbe ama polisi.
Ambao bado hawajaingia kwenye ndoa wanapo yaona haya mioyo yao hupata baridi yabisi wakiifikiria ndoa.
 
Kuchekeana kila wakati haimaanishi ndoa inafuraha kama wenyewe wameridhia kuishi kimikausho poa tu! mapenzi hayana formular, wengine ni full of hugs and kisses ila kumbe ni mapenzi ya kitamthilia tu ili kuridhisha wavimba macho kama wewe!
 
Wanaita usawa wa kijinsia, mwanamme akinuna, eti mwanamke naye ananuna, mwanamme akichepuka eti mwanamke naye anachepuka, mwanamme akichat na mademu kwenye mtandao eti mwanamke naye anachat na mabuzz kwenye mtandao, mwanamke akipakwa kofi eti na yeye anarudishia au anaomba talaka.
 
Raha ya ndoa ni kuheshimiana na kufarijiana, kila mmoja aone wikend kama hii ni fupi mno. Siyo mume kaa la moto na mke jivu la moto, mume akisema fyoko mke anajibu nyoo.

Mke Ngunguri, Mume Ngangari. Huu ni uhuni.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom