Hawa ni miongoni mwa watu wanaonifanya nizidi kufurahia 'ulevi' wangu

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
211
1,000
Nimekuwa napenda kusoma. Imekuwa ndio 'ulevi' wangu mkubwa kwa mda mrefu. Napenda kusoma uandishi wa waandishi mbalimbali, iwe ni maswala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi au michezo na burudani. Napenda kusoma na ninatumia mda mwingi kusoma kuliko kuangalia movie au kusikiliza musics.

Siku zote nafurahia 'ulevi' wangu kwasababu najifunza mambo mengi sana. Wafuatao ni TOP 6 ya watu ambao nilikuwa/nimekuwa nawafatilia na kila nikipata nafasi lazima niwasome. Popote walipo wajue mimi ni shabiki yao sana na najifunza/burudika kupitia uandishi wao.

6. Amani Martins
Huyu jamaa nilianza kusoma makala zake instagram mda mrefu sana hasa ile segment ya CHAMP ON MONDAY. Ni fundi wa kutumia lugha ya kifasihi kufikisha ujumbe. Siku hizi simfatilii sana maana post zake nyingi ana zidisha sana manjonjo hadi inakuwa kawaida. Ila popote alipo namshukuru kwa kuwa sehemu ya kufurahia ulevi wangu.​

5. Ali Kamwe
Huyu ni mtu wa soka. Nimekuwa namsoma huyu jamaa toka anaandika makala ya FAIR PLAY katika gazeti la dimba hadi leo ambapo anaandika MAMBO 10 YALIYOTOKEA KATIKA MECHI za ligi kuu bara.. Mzee wa NB :D:D.​

4. Edo Kumwembe
Kipindi fulani cha maisha yangu, nilikuwa nanunua gazeti la mwanaspoti jumamosi. Page ya kwanza kusoma ilikuwa ni namba 17, hapo lazima utakutana na NYUMA YA PAZIA. Huwezi kumuelewa akiwa anachambua mpira redioni ila huwezi kuacha kuenjoy makala zake gazetini. Maisha yapo kasi sana..Maisha bila unafiki hayaendi..Moja ya misemo yake maarufu.

3. Sirjeff Dennis
Sijawahi kuingia instagram bila kupita kwenye ukurasa wake. Madini anayoandika yananifanya nisichoke kumfatilia. Anaandika contents ambazo zinakupa mwanga na motisha ya kupambana zaidi kusaka pesa. Kuna muda unaweza ukachukia 'makavu laivu' anayoandika kama vile yeye mwenyewe ambavyo huwa anadai hawezi kuandika vitu vya uongo ili kufurahisha watu kwa sababu lengo lake ni kuwakomboa hasa vijana kifikra, ila huwezi kuchukia 'content' anayoitoa...Salute mzee wa Jeffism.​

2. Malisa G.J
Niseme nini juu ya huyu mtu!..Anajua sana sana sana. Na makala zake zimejaa madini sana. Kuna muda anakupa historia ambazo hujawahi kuzijua. Kuna muda anakupa references kwa kutumia quotes na theories za economics na physiscs, Kuna muda atakupa elimu ya maswala ya kisheria, kuna muda atakurudisha kwenye taaluma yake ya habari. Napenda reasoning yake katika maswala mbalimbali 'neutral' anayoyajadili.. Huyu jamaa ni Akili kubwa sana. Huwa najiuliza anayajua vipi yote haya???..Akili kubwa.

1. The Bold
Sitaki kuandika chochote kuhusu huyu mtu..anajua, anajua, anajua tena. Mtiririko wa makala zake hauchoshi. Ana uwezo wa hali ya juu wa kuunganisha stories bila kumchanganya msomaji. Ukimsoma huyu ndio unagundua kuwa uandishi ni kipaji na ni passion pia. Japokuwa hadi leo nafsi yangu haijamsamehe kwa kutomalizia VIPEPEO WEUSI ila no way out, I am his number one fan.

Kuna wengine wanaoandika vitu logical kama hawa?, naomba niwajue maana ndio ulevi wangu mkuu kwenye free time...!​
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom