Hawa ni baadhi ya WanaCHADEMA waliokamatwa ndani ya wiki moja tu na kunyimwa dhamana. Who is next?

Hili lichama ni la kihuni tu..lakini waTanzania baadhi hamuonagi,sijui hua mna macho gani na fikra gani. Chama cha wahuni hiki wala msisingizie eti serikali inatenda mabaya,hua wanatafuta kitu chenye kuvunja sheria wazi wazi ili wakikamatwa watengeneze story, ukitaka kujua hawa ni wahuni tazama wanavyo jiendesha na tazama majuzi na jana jinsi hiyo CCM ilivyo kua ikiendesha mambo yake LIVE kila mtu anaona,kundi kubwa la watu wengi wao wakiwa na hekima na busara,lakini upande wa pili wako kihuni huni tu hata hawaeleweki
Uhuni wake ni upi?

Kufanya shughuli zake kiseheria?

Policcm wanaowakamata na kuwafanyia unyama ndio werevu?

Ukishashiba makande ficha ujinga wako.
 
Haya matumizi mabaya ya vyombo vya dola ndio yatakayokuja kuifagia amani tulio nayo na tunayoendelea kujinasibu kuwa Taifa la amani! Kuna mambo ya hovyo sana yanayofanywa na jeshi la polisi kwa maelekezo ya CCM! Lakini wao CCM wakiyafanya hutalisikia mtu amekamatwa, hata hivi sasa ukipita mitaa karibu yote ya Dodoma kumezagaa bendera za CCM, lakini sijamsikia mkurugenzi wa jiji wala polisi wakiamuru ziondolewe, lakini tumeshuhudia kule Dar es salaam wakati wa vikao vya kamati kuu na Halmashauri kuu ya CHADEMA, bendera za CHADEMA zilimriwa kushushwa kwa nguvu na mkurugenzi wa jiji. Leo hii mgombea wa CCM hata akikusanya mji mzima kusindikiza kuchukua form hutawasikia polis, lakini akifanya hivyo mgombea wa CHADEMA, haraka sana polisi wanamuibukia! Wagombea wa CCM sasa hivi utawasikia wakigawa vifaa vya michezo na misaada ya kijamii kwa makundi mbalimbali, Takukuru wapo kimya, lakini wagombea wa CHADEMA wakifanya hivyo tayari wanakamatwa eti wametoa rushwa! Huu mtindo wa kufanya mambo ya mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa binamu mchungu, yatakuja kutupeleka pabaya sana! CCM itambue kuwa amani iliyopo sasa kamwe haiwezi kulindwa na kustawishwa kwa kukamata na kutisha aua kukandamiza wengine, bali kwa kuheshimu na kumtendea kila mmoja haki anayostahili! Kilichopo hadi sasa kinachotunza amani yetu sio uzalendo bali woga na uvumilivu wa wapinzani, hivi vyote kwa binadamu huwa vina ukomo wake!

Jukumu la polisi ni kuleta chuki nchini kwa kuifarakanisha ccm na wananchi kwa kuwatesa wapinzani.Japo awalijui Hilo.Polisi wanasaidia Sana kuuimarisha upinzani nchini,
 
Back
Top Bottom