Hawa Ng’umbi kutoa ushahidi wa kumng’oa Mnyika kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa Ng’umbi kutoa ushahidi wa kumng’oa Mnyika kesho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Mar 20, 2012.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kada wa CCM na Mkuu wa zamani wa Wilaya mbalimbali nchini kesho ataanza kutoa ushahidi wa kumng'oa kijana wa CHADEMA John Mnyika asiwe mbunge wa Ubungo.

  Kada huyo ataambatana na wanachama wengine wa CCM kutoka kata mbalimbali ambao nao wamejiandaa kutoa ushahidi mzito wa kumuunga mkono Mheshimiwa Ng'umbi.

  Kesi hiyo itasikilizwa katika mahakama ya kazi iliyopo mjini jirani na vyuo vya CBE na DIT kuanzia saa 3 asubuhi.

  Kesi hiyo imetajwa leo mbele ya Jaji Msuya na Wakili wa Hawa Ng'umbi ametakiwa kuwasilisha leo vielelezo vya ushahidi huo mzito dhidi ya Mnyika ili kesho Ng'umbi aweze kutoa maelezo yake.
   
 2. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Wabunge wa CDM watapukutika wote mwaka huu. Lema ndiyo huyoo amekalia kuti kavu.

  Kumbe karibu wote wana kesi? Inaonekana walicheza faulu nyingi wakati wa uchaguzi.
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kwani Mnyika naye alikimbia na masunduku ya KURA kama Dk. Makongoro Mahanga? CDM mwaka huu wana kazi kwani baada ya kuikombea Arumeru itabidi waende tena Segerea. Sidhani kama Makongoro atapona? Waziri mzima anaiba masanduku ya kura?
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ningekuwa mimi na ngumbi ningefuata ushauri wa salakana wa moshi mjini wa ccm hata uchaguzi ukirudiwa leo hii utashinda kama jawabu ni NO why contest ni kuwapotezea muda wananchi tu. sababu zote atazozitoa ngumbi haziwezi ku justify tofauti kubwa ya kura nyingi namna ile.
   
 5. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana UBUNGO hatumtaki mnyika na tumeshafafanua kero zetu zote, kwanza hatujui kama anaishi dar na tunamuona kwenye TV tu, nitawaunga mkono hao watu na ikibidi uchaguzi uitishwe mara moja, UBUNGO tupo kama mayatima hatujui nani mbunge wetu, anasubiri magufuli aje afungue kituo cha daladala ndo aonekane.
  Inshort tunajuta kumchagua kuwa mbunge na hatutorudia kosa hili kamwe na yeye anajua hili.
   
 6. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mnyika yuko busy na maandamano ya kudai maji; huku akitakiwa mahakamani wiki hii ya maji; MAKUBWA!!!
   
 7. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Mie ninachojua kesi zinazosikilizwa kwenye mahakama ya ardhi huwa zinahusiana na mambo ya ardhi, sasa kesi hiyo itamng'oa vipi ubunge? hapo niweke wazi mkuu.Kesi ya kumg'oa mbunge cheo hicho ni kesi ya uchaguzi ambayo sina uhakika kama inazungumziwa ktk mahakama ya ardhi. Naomba muweka mada utueleze vizuri kesi hiyo ya ardhi mnyika alifanya nini?
   
 8. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  HAKI iliyopotea ni wajibu kuidai; Hawa Ngumbi yuko katika mstari
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli unaweza kuamini kwamba wapinzani walikuwa na nafasi ya kucheza mchezo kwenye huo uchaguzi??? Sehemu nyingi walizoshinda wapinzani zina matatizo kwa vile yalikuwa created na CCM wakati wakijitahidi kuyashikilia mpaka waliposhindwa kabisa ndiyo wakaachia. Sasa wanataka kuitumia humihili wa mahakama kuwafanyia mazingaombwe ambayo NEC yaliwashinda.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  CCM wasipate shida ya kujishika na mahakama. Waitishe chaguzi kesho asubuhi Ubungo na Arusha mjini. Very simple!
   
 11. L

  LAT JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mahakama ya kazi? hii ni kesi inayohusu nini?
   
 12. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  We mwana ubungo wa wapi usio kuwa na akili na una chembe ya wizi na ufisadi
   
 13. a

  abujarir Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu hawa ngumbi anampotezea muda mnyika wa watu ,ni imani yangu kwamba jamaa ni jembe hivyo alishinda kihalali kwa kura za wakazi wa ubungo,hizi ni tapatapa za mfa maji
   
 14. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kakalia kuti lp?Hujui kuwa magamba mmelamba dume kwa lema!!?Lema ni dawa ya magamba.
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Kwani wale aliowatisha kwenye mdahalo kuwa atawafungulia mashitaka kishawapeleka kwa pilato?
   
 16. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  CCM Kituko tu,wakishinda wao hata kama ni kwa makaratee,poa tu..wakishinda upinzani hawastahili.
   
 17. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  We hamnazo kweli.
   
 18. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Ndugu LAT: Ninafikiri ni typos hizo mleta hoja alikuwa na maana ya Mahakama ya KADHI.

  Kama kesi iko mahakama ya KADHI I'm sure itakuwa ni kesi ya MIRATHI na TALAKA. na wala sio kesi ya uchaguzi.
   
 19. F

  FredKavishe Verified User

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unavyoandika inaonekana si mkazi wa ubungo kwa taarifa yako ww ni kibaraka niona thread yako ya jinsi ya ccm kuimaliza cdm
  Ngoja nikuambie kijana o jike mnyika anafanya kazi na atapiga kazi na anaiweza kazi jimbo la ubungo ndo lenye wakazi wengi sana
  Mnyika juzi alikuwa kwenye ufutialiaji wa maji mm mkazi wa ubungo na najua anachofanya
  Anafanya mikutano kusikiliza kero za wananchi na kuzitekeleza na baadaye kutoa ripot
   
 20. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hayo masanduku ya kura za wizi ndio yaliyompa uwaziri,
   
Loading...