Hawa ndiyo JK anawaita wawekezaji wa kukaribisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndiyo JK anawaita wawekezaji wa kukaribisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Dec 19, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::12/19/2009Mkorea aichezea serikali ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata[​IMG]Na Sadick Mtulya

  MVUTANO uliojitokeza kuhusu kusuasua kwa utengenezaji wa barabara ya kilomita 64 ya Bagamoyo-Msata kwa kiwango cha lami, umeingia sura mpya baada ya kubainika kuwa raia mmoja wa Korea ndio kiini cha tatizo hilo.

  Habari za uhakika ambazo Mwananchi Jumapili imezipata zinaeleza kuwa chanzo cha mvutano huo ni baada ya Mkorea huyo aliyeingia nchini kama mwekezaji na 'kuwashika' baadhi ya vigogo serikalini kuchota Sh9 bilioni kati ya Sh13 bilioni zilizotolewa kwa kampuni kadarasi ya Tanzania Korea Partnership (Takopa) ambayo ni muungano wa kampuni za SUMA-JK inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), na kampuni ya Shinwoo na Chungmoo zote kutoka Korea.

  Pia kumpuni hizo zimeshindwa kutekeleza baadhi ya makubaliano ya mkataba, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuleta wahandisi na vifaa vya kufanyia kazi.

  Habari zinasema kuwa kupitia kampuni hizo, Mkorea huyo, ambaye anasemekana kuwa yupo karibu na vigogo serikalini, alijichotea kiwango hicho cha fedha na kukipeleka kwao.

  Takopa ndio iliyosaini mkataba wa miaka miwili wa kujenga barabara hiyo ambayo hadi sasa imejengwa kilometa moja tu. Barabara hiyo iliyotengewa Sh82 bilioni ni moja kati ya ahadi zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuijenga.

  Kusimama kwa barabara hiyo kumeelezwa kunatokana na SUMA- JKT kuhoji mahali zilipo fedha hizo.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, mgogoro huo ulianza baada ya Suma JKT kutaka kupewa maelezo ya kina ya jinsi Mkorea huyo alivyozichukua fedha hizo ambazo zilitolewa kama sehemu ya utaratibu wa mkataba wa malipo ya awali ya asilimia 15 ya gharama za ujenzi.

  Katika fedha hizo Suma JKT walichukua Sh4 bilioni kwa ajili ya kununulia vifaa vya kufanyia kazi ya ujenzi.

  Katika makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo, Suma JKT pamoja na kampuni hizo za Kikorea walikubaliana kuwa kila kampuni itoe wataalam na vifaa vya kufanyia kazi ya ujenzi, lakini ni Suma JKT tu ndio waliotekeleza makubaliano hayo.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, katibu mkuu wa Wizara ya Miondombinu, Dk Omari Chambo alikiri kwamba kuchelewa kukamilika kwa barabara hiyo kunatokana na makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo kutokwenda kama ulivyopangwa.

  Alifafanua kwamba hali hiyo ilitokana na mshirika (kampuni za Kikorea) kushindwa kuleta wataalam pamoja na vifaa vya ujenzi.

  “Siwezi kuingilia matatizo ya ndani ya Takopa, lakini ninachojua mimi ni kwamba tangu kusainiwa kwa mkataba hawa Wakorea ambao ni wabia na Suma JKT wameshindwa kuleta wataalam na vifaa vya kufanyia kazi,” alisema Dk Chambo.

  Hata hivyo, habari za uhakika zinasema kuwa Suma-JKT ilifikia hatua ya kuuliza fedha hizo baada kugundua kuwa kuna mazingira tata na yasiyofuata utaratibu katika matumizi.

  Kutokana na mazingira hayo, Septemba 29 mwaka huu kikao cha kujadili suala hilo kilifanyika na kuhudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi pamoja na katibu mkuu wa wizara hiyo, Mkuu wa Majeshi, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Mkuu wa JKT, Waziri wa Miundombinu, Shukuru Kawambwa, Tanroads na pamoja na wawakilishi wa kampuni hizo za Kikorea.

  Katika kikao hicho Suma–JKT ilitangaza uamuzi wa kujitoa katika ushirikiano huo pasipo kuandika barua ili kuifanya Takopa isivunjike kwa vile kwa kuandika barua ingekosa sifa za kuwa kampuni.

  Pia habari zilisema uamuzi wa kujiondoa pia ulichangiwa na majibu ya kebehi ya kuibana Suma JKT kuwa kwa nini inafuatilia zaidi fedha zilizochukuliwa na Wakorea katika mradi huo, kauli ambayo inadaiwa kuwa ilitolewa na mmoja wa vigogo wa kutoka Wizara ya Miundombinu

  “Suma-JKT imejiondoa katika ushirikiano huo baada ya kugundua kuwepo kwa mazingira tata ya matumizi ya fedha ya Sh9 bilioni, lakini haikujiondoa kwa kuandika barua kutokana na ukweli kwamba ingefanya hivyo, fedha zote za Watanzania zingekwenda na maji kwa kuwa Takopa isingekuwepo,” kilisema chanzo chetu.

  “Na hali hii imetokana na Mkorea huyu kuwa na nguvu za ajabu serikalini, na amekumbatiwa na vigogo wakubwa.”

  Waziri Kawambwa hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo baada ya simu yake kupokelewa na mtu aliyesema: “Waziri Kawambwa ana kazi nyingi ofisini hivyo hawezi kuzungumza na wewe, acha ujumbe nitamfikishia.”

  Mwananchi Jumapili ilikuwa imemtafuta kwa zaidi ya mara saba kabla ya kupata jibu kutoka kwenye sauti hiyo.

  Meneja wa Tanroads mkoani Pwani, Gabriel Mwikola alisema katika mradi huo Tanroads mkoani humo imehusishwa kwa kiwango kidogo.

  “Ni kweli mradi huu upo katika mkoa wa Pwani, lakini sisi tumehusishwa kidogo... kwa majibu ya kina kuhusu mradi huu wasiliana na Tanroads makao makuu. Kwa upande wangu utakuwa unanionea kwa kuwa si mtu sahihi na sina majibu ya kina kuhusu sakata hilo,” alisema Mwikola.

  Katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani hivi karibuni, wajumbe walitoleana uvivu na kutaka ukweli juu ya kusuasua kwa barabara hiyo inayotia doa ahadi za rais.

  Kutokana na kuibuka kwa malumbano katika kikao hicho kwa kila upande kumtupia mpira mwenzake, Mkuu wa Mkoa huo Hajjat Amina Saidi aliamua kuunda kamati ya watu saba ikiongozwa na Profesa Idrisa Mtulia ambaye ni mbunge wa Jimbo la Rufiji kutafuta ukweli wa sakata hilo.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu, Profesa Mtulia alisema kamati yao bado haijaanza kazi kutokana na kukosa vielelezo vya nyaraka kuhusu sakata hilo.

  “Ninavyozungumza na wewe kamati yetu bado hajaianza kazi na hii ni kutokana na kwamba hatukujua tuanzie wapi kwa kuwa hatujapewa vilelezo vyovyote hadi sasa,” alisema Profesa Mtulia.

  Profesa Mtulia alisema kamati yake inatarajia kukutana Desemba 22, mwaka huu ili kuangalia uwezekano wa kupewa nyaraka zitakazowasaidia kutafuta kiini cha ujenzi huo.
  “Na ninafikiria hadi mwakani ndio tunaweza kuanza kufanya kazi na mara tutakapomalizia ripoti yetu tutaikabidhi kwa mkuu wa mkoa,” alisema.
  Tuma maoni kwa Mhariri
  [​IMG]Facebook
   
 2. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kwa nini hawa viongozi hawaongelei kutoka "JELA"?

  Ni mkataba gani ambao hawa viongozi wameu-sign usiokuwa na mauzauza?

  Matapeli wote wa nje wameshajua Tanzania ina viongozi mabwege, wasiojua kusoma na kama wanajua kusoma basi uelewa wao mdogo sana.
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duuh kama kuna uwezekano wa kubadilisha Raisi Mwakani; Huyu jamaa basi tena hivi kuna hata tenda moja ambayo aiambatani na ufisadi huko. hapana hawa jamaa wamezidi sasa.

  We need changes quickly to save our nation; seriously this is too much basi kila kukicha tu tanzania imetapeliwa tanzania imekopa looh hapana. Maana hamna hata siku nimesoma humu ndani something went right na wapambe wao waliojaa humu.

  Maanake hata ukisema huyu jamaa apewe chance hatadili na watu wake wapunguze tabia mbaya ndio things are getting worse by the hour enough kwa kweli.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Sina shaka kabisa kigogo anaemkubatia huyo Mkorea ni lazima awe Shukuru Kawambwa na ndiye wizara yake yenye mawaa mengi sana yanayoashiria harufu ya rushwa!! Huko TRL ndio yeye anawakingia kifua wahindi; ukija ATCL yeye ndiye analazimisha ukodishaji wa ndege zinazotia shirika hasara licha ya kumg'an'gania muwekezaji wa Kichina ambae ametoweka kiainaaina; sasa ndio hizo billioni 9 za barabara tena jimboni kwake nazo lazima amekatiwa na ndio maana mkorea analeta jeuri. Sasa kwa mwendo huu muungwana ataficha uso wake wapi mbele ya watanzania? Hapo ndipo anaposhinikizwa kufanya maamuzi magumu hata yanapowahusu jamaa zake!
   
 5. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  kuna mwingine yupo Gurumeti,ni kaburu anamwakilisha Jones Tudor II...JK anamwogopa kama nini,mby zaidi jamaa keshajua,so na yeye anatumia jina la JK kufacilitate wizi wake...
   
 6. N

  Nakandamiza Kibara Senior Member

  #6
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watanzania wa Mugumu wana hali mbaya sana sana . Grumeti ni jeshi la uana haramu jamaa ni mbaya anaogopwa hata kuliko Serikali Mkoani Mara na wilaya Mugumu . Nimepata kufika hapo nikasimama na gari getini nakueleza nilivamiwa na wazawa kama mie ni mwizi mie nikatulia baada ya makelele yao nikawa hoji sana wakapata akili wakasema si wao ila Kaburu ni mbaya mno na anawakomoa mno nma Serikali Mugumu kazi yao ni kusujudu kwa Kaburu na Mkoa mzima . Hili la Kawambwa hawezi kuondoka maana ni home boy so tutapiga kelele hadi tuchoke JK hana mpango wa kusikiliza .
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280

  kikwete..
  meno unayo lakini hung'ati yyyyyyyy?
  kwanini??
  wapiga kura ako unatuangusha...
  hakika raisi wetu huna roho ya uzalendo hata kidogo...
  utajali maslahi ya mabepari hadi lini???
  jaribu japo kidogo kurudisha imani kwa wapiga kura wako...
  angalia mjomba.... ushindi wa sunami ulioupata mwaka ule unaweza ukashangaa unakuwa ushindi wa kijiko cha sukari....
   
 8. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I am happy it is happening in Bagamoyo anakotoka huyu shukuru na ndugu yake JK sijui mwakani watawaeleza nini wananchi wao. Wanafisadi hadi nyumba may be their brain have stopped thinking.
   
 9. N

  Nakandamiza Kibara Senior Member

  #9
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 17, 2007
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa JK na kundi lake Mzalendo ni mtu mwenye kutoa kidogo na kuchukua zaidi toka Tanzania wao hawajali maana wanapata %
   
 10. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lunyungu,

  Asante sana kwa hii Post. Kwa kweli inasikitisha sana. Ni matumaini yetu kuwa JK atachukua hatua. Kwa upande mwingine tunapata fundisho kuwa tunahitaji sasa kufanya uamuzi wa kuiwezesha SUMA JKT na kuwa kampuni kubwa ya kiwango cha kimataifa. Binafsi nawaamini sana SUMA JKT.

  Nchi yetu ina Kilomita za barabara kama 85,000 ukiacha zile za TANAPA zinazokadiriwa kufikia elfu 30. Iwapo tutaiwezesha SUMA JKT kwa vifaa, wataalam (CoET washirikiane nao) na fedha, naamini kabisa ndani ya miaka mitano barabara zetu zote zisizo na lami zitakuwa bora na kuweza kupitika muda wote wa mwaka bila matatizo.

  Tunamuomba sana Rais achukue hatua na aiwezeshe SUMA JKT na kuifanya kuwa kampuni kubwa na bora ya kimataifa.
   
 11. t

  tibwilitibwili Senior Member

  #11
  Dec 20, 2009
  Joined: Sep 12, 2006
  Messages: 181
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ili JK na jamaa zake wasikie maombi haya lazima kujua kama SUMA JKT wakataka mapesa kwa wadau wa CCM kama hakuna basi uwezo wao bni bure tutawapa wakorea tu mtake msitake
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hii nchi kazi kweli kweli.
   
 13. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naamini Rais hatakaa kimya kwenye hili tatizo. Lazima atachukua hatua. Vinginevyo hakuna haja ya kujenga barabara za lami. Ni bora mara mia fedha hizo tuziwekeze kwenye ICT na S & T na tuwe na barabara za vumbi ambazo zinapitika hata wakati wa masika. Nchi itaendelea tena kwa kasi kubwa zaidi.
   
 14. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hivi kwanini kila kitu tunataka JK ndio achukue hatua? Yeye ni nani? SUPERMAN?

  Kwa nini vyombo husika na wizara husika isichukue hatua? Huyo mkuu wa Tanroads mkoani amesha-raise flag kwa wahusika? Kwa Bunge? Kwa TAKUKURU?

  Bunge sasa linatakiwa lipewe meno zaidi na pia MIKATABA YOTE IPITISHWE NA BUNGE kwani ndio linalowajibika direct kwa wananchi.

  Wizara zisiwe na uwezo tena wa kuidhinisha hii mikataba hewa.
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Toa ushauri nani aelekezee hizi habari maana yeye ndiye anawachagua mawaziri na makatibu wakuu , ma IGP na Takukuru kama hao hawatendi basi aulizwe nani ?Tupe mbadala maana hata Bunge lina dharauliwa
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  JK ni Dr. Al Haj Kanali Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, Amiri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM, Mkuu wa watendaji wote wa serikali na mashirika ya UMMA.

  Mwenye jibu ni JK aliye na madaraka ya kuwateua, kuwawajibisha na kuwafukuza wakizembea. Kumbuka the buck stops with the President.

  Juzi Waziri wa Sheria kwa baraka za JK katamka mchana kweupe kuwa Bunge halina madaraka wala ubavu wa kuiwajibisha serikali na sera ianyoongoza serikali ni ya CCM.

  Unaposema wizara una maana gani - kuna tofauti gani kati ya wizara na serikali na huo uwezo wa kuidhinisha mikataba apewe nani ?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Tunaowafata TZ isiyokuwa na umeme wa kutosha hata kuwashia bulb ni matapeli kama wale wanaowaita.Period!
  Na uzuri ni kwamba urefu huu wa safari umetupa wasaa kujua kwa kina ukweli kuhusu wahusika
   
Loading...