Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,676
- 729,842
Ni sentensi maarufu sana kwenye ngwe hii ya Magufuli 'watumishi hewa'
Mtumishi hewa ni nani.
Kila anayeitwa mtumishi hewa alishawahi kuwa mtumishi kamili lakini kutokana na mfumo mbovu wa ajira na ulipaji wa mishahara, kusitisha ama kufukuzwa kazi au kazi na utumishi, mlolongo mrefu wa formalities nyingi hivi vitu ndio vimeleta watumishi hewa...
1. wale walioajiriwa lakini wakaacha kazi baada ya muda fulani...mfanyakazi wa serikali asipoonekana eneo lake la kazi bila sababu na bila taarifa yoyote huyu inapaswa kusimamishwa malipo yake na baada ya hapo kusimamishwa kazi. .taarifa ya kusimamishwa kazi inabidi ifike kote kunakohusika kwa maandishi na kwa muda unaotakiwa
2. Wale waliofukuzwa kazi. Mtu akishafukuzwa kazi isiishie tu kumpa barua yake ya kufukuzwa bali kwa muda sahihi taarifa hizi zifike kote kunakohusika
3. Marehemu, hao nao ni vile vile. Mtu kafa lakini taarifa zake hazibadilishwi na kufutwa kwenye kitabu cha ajira
Kufuatilia udhaifu wa kimfumo kitengo cha mishahara popote pale waliweza kuunda syndicate yao ya upigaji....na hapa ndipo watumishi hewa walipotokea na katika hili kuna ma master minds ambao wanaratibu kila kitu mpaka pesa itoke.
Utaratibu unaofanyika sasa hivi wa kuthibitisha ajira ya kila mtu na kila mtumishi wa umma kulipwa moja kwa moja toka hazina utaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa sana hili tatizo japo huu ni ufumbuzi wa muda mfupi tu...