Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Rais mpya wa Marekani Donald Trump ni baba wa familia ya watoto watano.
Katika maisha yake amekuwa katika ndoa tatu mfululizo, mbili zikiwa zile zilizovunjika kwa talaka na moja ni ile aliyopo kwa sasa, kubwa kilichopelekea Trump kuishi katika ndoa tatu tofauti ni ile dhana yake ya "I am married to my bussiness".
1: Donald Trump Jr.
Huyu ndiye kijana mkubwa wa Rais Trump mwenye umri wa miaka 38, ni mfanyabiashara maarufu akifuata nyayo za baba yake na ndiye Executive Vice President wa miradi ya baba yake inayojulikana kama Trump Organization, huyu ndiye anategemewa zaidi kushikilia uendeshaji wa miradi ya baba yake yote pindi atakapokuwa Ikulu.
2:Ivanka Trump
Huyu ndiye binti mkubwa wa Rais Trump na mtoto wa pili mwenye umri wa miaka 35 na ni mama pia wa watoto wawili, ni mfanyabiashara mzuri aliyejikita katika mambo ya mavazi(fasheni na mitindo), biashara ya vito vya thamani pamoja na mahoteli.
Pia baada ya mzee wake kuingia Ikulu atasaidiana na kaka yake Donald Jr. kuendesha biashara za familia katika Trump Organization.
3: Eric Trump
Huyu ndiye kijana wa tatu wa Rais Trump mwenye umri wa miaka 32, mara nyingi alichukuliwa kama "mtoto wa mama" ndani ya familia yao, japo interest yake ni mambo ya ujezi lakini ni mfanyabiashara mkubwa wa mvinyo na kupitia taasisi yake ya Eric Trump Foundation hutumia utajiri wake mwingi katika taasisi za kiafya na tafiti katika kusaidia watu hususani watoto wenye shida mbali mbali za kiafya.
Tayari ameshawekeza zaidi ya Dollar Milion 28 sawa na Bilioni 60 za kitanzania katika kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali, na inategemewa baada ya baba yake kuingia madarakani huwenda akachukua na kuiendesha taasisi ya baba yake ya kutoa misaada sambamba na ile ya kwake kwa sababu ya uzoefu wake katika kuendesha taasisi hizo .
4:Tiffany Trump
Huyu ni mtoto wa nne wa Rais Trump na binti wa pili mwenye umri wa miaka 23, ni muhitimu wa chuo na binti wa tofauti sana katika familia yao, tofauti na ndugu zake hana interest kabisa na mambo ya kibiashara, ana interest na ulimwengu wa sheria.
ila hupenda maisha ya anasa na kuuza sura mitandaoni.
5:Barron Trump
Huyu ndiye mtoto wa Rais Trump wa mwisho mwenye umri wa miaka 10, kihaiba ni mtoto anayefanana sana na baba yake kati ya watoto wake wote kwa tabia yake ya kupenda kufanya mambo "from the scratch" na akipata matokeo anayoyataka huyavuruga kabisa na kuanza upya tena na kupenda pia kusimamia kile anachokiamini.
Kifupi huyu ndiye kipenzi cha Trump na anaishi na baba yake kama babu na mjukuu wake kwenye golf utawakuta pamoja, kwenye kula bata utawakuta pamoja, kwenye dinner wako pamoja nata matembezi utawakuta pamoja, kwenye familia yao huitwa jina la utani "Donald mdogo" kutokana na ufanano wake na baba yake kimuonekano na kitabia.
Kwa msaada wa mtandao.