Hawa ndio watia nia jimbo la Geita Mjini

vevenononombo

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,289
1,500
Baada ya mbuge wa Geita kuaga dunia, hawa ndio baadhi ya wawania jimbo hilo na mmoja wao anaweza kuwa ndiye mbunge nitawapanga kwa uzito wa mgombea na nafasi yake ya kushinda.

1. Ndg Rogers Luhega(CHADEMA) huyu kwa sasa ndiye gumzo la mji ,ni msomi wa elimu ya miamba,tatizo kubwa kwake ni viongozi wenzie ndani ya CHADEMA,ila ikiwa atapitishwa na chama basi ushindi ni asubuhi na mapema.

2. Joseph Msukuma, huyu ni mfanyabiashara mkubwa na mwenyekiti wa CCM mkoa na diwan wa kata ya Nzela,kielimu ni standard seven,ingawaje anakubalika pia miongoni mwa wanageita.

3. Ernest Mabina huyu ni Mbunge wa zaman wa jimbo la Geita ni msomi mzuri,na anahusiswa na kuwa kwenye kitengo maalum ktk serikali,anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa wapinzani.

4. Mangilima huyu ni kiongozi ndani ya mgodi wa Geita GGM,ana pesa na anaweza kuwa mtu wa pili kwa ushawishi ndani ya CHADEMA baada ya Rogers ingawaje bado si mtu wa kuaminika kwa siasa za upinzani.

5. Misalaba huyu ni mfanyabiashara mzuri na anajijenga kwa sasa kimtandao elimu yake ni utata kidogo ingawaje anaweza kusimama vizuri.

6. Sikwambi huyu naye amejitosa na ushawishi wake si mkubwa sana.

7. Innocent huyu nae yuko ktk mbio hizo ni msomi wa chuo kikuu na mwanaharakati isipokuwa,hana mke,aoe kwanza ndio aje tumfikirie kumpa madaraka.

8. Vick Kamata huyu ni viti maalum lakini ni ngumu sana kupitishwa na CCM.

9. Jonathan huyu ni Mzee na msomi mzuri lakini itakuwa ngumu sana kuteuliwa na chama chake.

10. Robert Muta huyu nae ana nia ila ni Mhaya wa Bukoba anaetaka jimbo la Geita.
 
respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,539
2,000
Mkuu sina shaka umemuweka Rodgers namba moja kutukana na kumpenda wewe binafsi.!!

Anyway kiukweli mara nyingi ninaposikia siasa za Geita, Jina linalosikika sana kwa upande wa Upinzani hususani Chadema ni Rodgers. Inaonekana jamaa anajua sana kujitangaza, ila natabiri kimbembe kati yake huyo na Hili tajiri la Madini toka Ugambani, Msukuma. Kiukweli Cdm inatakiwa wazichange vizuri karata zao ndani ya kura za Maoni. Vinginevyo tunaeza kulikosa jimbo hilo wakati kila dalili za ushindi zinaonekana.

Tena wampitishe mtu mwenye nia ya dhati na uwezo mzuri kiuchumi ili kukwepa hujuma za kununuliwa na huyu Msukuma kiasi anaweza kumshawishi kujitoa ili Msukuma apite bila kupingwa.

BACK TANGANYIKA
 
Jamaa anakubalika kiukweli watu WA geita mjin ni mashuhuda WA hili
 
respect wa boda

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
4,539
2,000
Jamaa anakubalika kiukweli watu WA geita mjin ni mashuhuda WA hili

Mkuu sina shaka kwamba huyu jamaa anakubalika, maana ukishatangaza nia tu kupitia Cdm kazi ya kujiuza ni nyepesi sana. Sasa mashka na hofu yenu ni nini? kuna kizingiti gani cha kumzuia huyu jamaa kupitishwa na chama huko Geita? Msikilize @Idumilwa hapo juu..!

BACK TANGANYIKA
 
vevenononombo

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,289
1,500
Mkuu sina shaka kwamba huyu jamaa anakubalika, maana ukishatangaza nia tu kupitia Cdm kazi ya kujiuza ni nyepesi sana. Sasa mashka na hofu yenu ni nini? kuna kizingiti gani cha kumzuia huyu jamaa kupitishwa na chama huko Geita? Msikilize @Idumilwa hapo juu..!

BACK TANGANYIKA[/QUOTE viongozi vibaraka ndio chanzo cha yote
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,178
2,000
teamRogers mnamchafua kamanda MANGILIMA KWA KUWA MNAJUA KUWA JAMAA YENU KWENYE KURA ZA MAONI NDANI YA CHAMA ATAPIGWA ASUBUHI NA MAPEMA!

Hakuna mfanyakazi aliyeuzwa na mangilima!

JENGENI HOJA NA SIO KUCHAFUA WENGINE BILA SABABU!

Rogers ni mchovu!
 
vevenononombo

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,289
1,500
teamRogers mnamchafua kamanda MANGILIMA KWA KUWA MNAJUA KUWA JAMAA YENU KWENYE KURA ZA MAONI NDANI YA CHAMA ATAPIGWA ASUBUHI NA MAPEMA!

Hakuna mfanyakazi aliyeuzwa na mangilima!

JENGENI HOJA NA SIO KUCHAFUA WENGINE BILA SABABU!

Rogers ni mchovu!

Hakuna timu Fulani hapa ila kiukweli bwa Rogers kakisaidia chama kwakujitolea mno na kukifikisha hapo sio mchezo
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,178
2,000
by vevenononombo;
Hakuna timu Fulani hapa ila kiukweli bwa Rogers kakisaidia chama kwakujitolea mno na kukifikisha hapo sio mchezovevenononombo tatizo lenu mko bize kujenga jina la mtu badala ya chama! hii tabia ya Uayatolah MNAYO SANA(na hivi anatokea huko!)

rogers ni mwanachama kama wanachama wengi wslivyojitolea kujenga chama hapa Geita, hii ya kumpa kichwa kuwa yeye ndio kila kitu, BILA YEYE CHADEMA ITASHINDWA NDIO ITAMGHARIMU BAADAYE!

"kimsingi chama kisiponipitisha mm mjue tu chadema tutashindwa"~by rogers

Jiandaeni kisaikolojia anaweza kupita kwenye kura za maoni au asipite na hii ndio demokrasia! msianze kuleta fikra bila rogers geita hamna chadema, CHADEMA IPO IMARA KWA MGOMBEA YEYOTE ATAKAYETEULIWA NA CHAMA!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom