Hawa ndio watangazaji wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndio watangazaji wetu!

Discussion in 'Entertainment' started by mtanzaniaraia, Aug 24, 2009.

 1. m

  mtanzaniaraia Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijana tuu kigi kuu ya Vodacom Tanzania bara imeanza wakati Mnyama akiwararua wana lizombe wa Songea huku Dar Wananchi wakitoana jasho na watoto wa mbagala(African lyon).Katika mchezo wa Dsm kati ya Yanga na A/Lyon mtangazaji wa redio ya taifa(TBC) Juma Nkamia alileta burudani ya pekee pale alipojikanganya na matamshi yake mwenyewe.
  1).Pale wachezaji wa Yanga walipokuwa wameotea(off side) na mashabiki wao walipokuwa wanamlalamikia mwamuzi,Juma Nkamia alisema"wapenzi wa Yanga wamwachie mwamuzi kwani yeye ndiye ajuaye mtego wa kuotea" .Lakini walipokuwa wanaotea African Lyon Juma alisema"Waamuzi wetu bado kujua sheria za offside"
  2).African Lyon ilipopata penati Nkamia alisema"Yule Hamisi Yusuf wa Yanga anastahili kupewa kadi kwa mchezo mbaya aliofanya japo mwamuzi hakutoa kadi,tena baada ya kipa wa Yanga kuokoa penati Nkamia akaendelea"Mwamuzi inaelekea hajuhi sheria ya kuokoa penati kwani kipa wa Yanga ametoka golini ndio maana ikawa rahisi kuokoa penati hivyo ilitakiwa penati irudiwe.
  3).Wakati mchezo unaendelea na mashabiki wa Yanga wakimshutumu Nkamia kwa utangazaji wake wa upendeleo,yeye akasema"Hii ni kazi yangu mimi ndiye ninayejua jinsi ya kutangaza kama kuna watu wanataka kutangaza wapeleke maombi yao TBC wakishinda usaili waende kutangaza kwani kazi ya kutangaza ni ya watangazaji na sio washangiliaji!
  Sasa kinachonishangaza ni kuwa,yeye Nkamia amekuwa akimshutumu mwamuzi Owden Mbaga kuwa anaboronga wakati kazi ya kuchezesha mpira ni ya refarii inakuwaje anaposhutumiwa yeye ajibu kazi ya kutangaza ni ya mtangazaji na si ya washangiliaji kwani yeye hakuliona hilo?Kuwa mstaarabu kwani upenzi wa timu haufahi ukiwa kazini,tekeleza wajibu wako!Na kwavile wewe Juma Nkamia ni mwana JF natumahi ujumbe utakuwa umefika mahali pake.
   
 2. M

  Magehema JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Usinichekeshe, kumbe wewe mgeni kwa Nkamia, ingekuwa amri yake Yanga ingeshuka daraja.
   
Loading...