Hawa ndio wasomi wetu: IFM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa ndio wasomi wetu: IFM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kasyabone tall, Sep 15, 2009.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Wanafunzi wanaswa wakifanyiana mitihani

  WATU watatu, akiwamo mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam wamekamatwa wakiwafanyia mitihani wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wanaosoma ngazi ya stashahada ya juu pamoja na shahada.

  Mwanafunzi huyo, Frank Kaduma, aliyekuwa anamfanyia mtihani mwanafunzi aliyemtaja kwa jina moja la Tina, alikuwa ameahidiwa na mtu aliyemuunganisha na mtahiniwa huyo kuwa baada ya kutoka kwenye mtihani huo angelipwa sh 150,000.

  Tanzania Daima ilimshuhudia mtuhumiwa huyo akihojiwa na Michael Andekisye, ambaye ni Msajili wa Wanafunzi chuoni hapo.

  Msajili huyo alisema kuwa kitambulisho alichokuwa akikitumia kumfanyia Tina mtihani kilikuwa na jina la Christian Mbago, mwanafunzi wa mwaka wa tatu.

  Kaduma alifafanua mbele ya ofisi hiyo kuwa aliitwa na rafiki yake ambaye hata hivyo hakutaka kumtaja jina, na baadaye alimuunganisha na mtahiniwa na kukubaliana kiasi hicho cha fedha baada ya kazi hiyo kumalizika.

  "Mimi ninasoma Azania, nachukua PCM (Fizikia, Kemia na Hisabati), rafiki yangu anasoma masomo ya biashara na mtihani wa leo una hisabati, hivyo juzi nilikuja naye ili anionyeshe darasa na leo ndiyo nimekuja kumfanyia mtihani," alisema Kaduma.

  Wakati mwanafunzi huyo akihojiwa, mwanafunzi mwingine, John Kapinga, alikamatwa na kupelekwa katika ofisi ya msajili baada ya kukutwa akimfanyia mtihani mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo, Joel Mlengule, anayesoma Stashahada ya Juu ya Hifadhi ya Jamii (Advanced Diploma in Social Protection).  tutarajie nini kutoka kwa wasomi hawa wanaosomeshwa kwa kodi yetu
   
 2. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kumbe yule mdau aliyesema IFM ss hivyi ni wazugaji tu ni sawa.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,318
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Ndo elimu yetu ilivyo. Halafu tukiingia kazini tunafikiria kupiga deal za kulala maskini na kuamka matajiri maana elimu yenyewe imekuwa ya kuunga unga tu kama inavyoonyeshwa na matatizo haya.Kazi kweli kweli
   
 4. Amosam

  Amosam Senior Member

  #4
  Sep 15, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vyuo vingine vinasindikiza watu tuu hawana jipya
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,318
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Kweli nakubaliana na wewe...na kuendekeza kuuza sura tu kila kona. Tunajisahau kuwa education helps us to realize our potential. Ni level 8, Savana na Bills kwa kwenda mbele!!
   
 6. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  haya watanzania serikali na mikakati yake ya kuchukua wasichana waliofaulu kiwango cha chini ndo hayo wakifika vyuoni,tutafika kweli?
   
 7. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia suala la ku-cheat lipo karibu vyuo vyote, UDSM wameishakamatwa watu kibao wanafanyiana mitihani na kuwa-discontinued.

  Suala hapa si ubora wa chuo katika elimu au ubora wa kusajili wanafunzi wenye sifa, suala kubwa ni je utungaji wa mitihani, usimamizi wake na usahihishaji wake upo katika kiwango kinachokubalika?.

  Ukiona wanafunzi wanafanya vitu kama hivi kuna mambo mawili, 1. Ni weakness ya system ambayo inatoa mianya ya watu kufanikiwa katika udanganyifu, 2. High risk taker students, the higher the risk the higher the return (mwanafunzi anajua akikamatwa kaharibu maisha ila asipokamatwa atapa A) vitu hivi viwili ndiyo sababu hasa za ku-cheat.

  Nakumbuka UDSM kuna wakati tulikuwa na msemo mmoja "It is very risk to use "desa" in a tough examination, but it is very very risk not to use it-because you'll fail and be discontinued forthwith"- a notion which I always disagreed with

  Kwa kuwa IFM, UDSM wameshakamata watu wengi sana wakifanya udanganyifu na kuwa-disqualify, basi ukweli unabakia kuwa wanafunzi wa siku hizi ni risk takers. Kulaumu chuo ambacho kimeweza kuwakamata wanafunzi wawili wakifanya udanganyifu ni kutokitendea haki, kwani ni umakini pekee ndiyo unaweza kubaini udanganyifu hata kama mwanafunzi afanye nini.

  Ninampongeza msajili wa wanafunzi IFM kwa kuwa na timu makini ya usimamizi na kuwa na utaratibu mzuri wa kubaini identity ya candidate. Katika kipindi hiki cha kuwa na wanafunzi wengi darasani ni dhahiri kazi hii si ndogo.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kwa vyov yote vile IFM/CBE huwa vilaza ni wengi na hasa watoto wa wakubwa/wenye pesa. Kwa akina dada unajua tena pale ni city center kwa hiyo kujirusha kwa sana halafu wanakumbuka shule ikiwa muda umekwisha.
   
 9. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Naaam Naamini kabisa Hususani waichana wengi Saana Hapo mjengoni IFM wanakwenda kujiuza tu pale hakuna kusoma Kila siku wanabadilisha mabwana toka BOT sasa ndio dalili zao hizo wazazi angalieni Mabinti wanaaga kwenda kusoma kumbe kujiuuza Karo zinateketea wao wanawakatikia Ma PDG
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  wewe huijui IFM vyema, hiki niuchuo ambacho huwezi kucheat ukakamatwa ukaachwa, huyo mtu anaetajwa kama Andendekisye Mark kwa sasa ni msajili wa chuo, aliwahi kumkamata mkewe katika sup,

  tofauti na vyuo vingine IFM ukikamatwa jamii nzima hutaarifiwa , na kwa hilo huwa somo kwa wengine wote.

  vyuo vingine hii hubaki kuwa siri ya ndani.

  Ukitaka kujua IFM NI NOMA NENDA PALE BOARD YA UHASIBU KAULIZE NI NANI ALIENGOZA MWAKA JANA KWENYE cpa, Huyu anaitwa Hansigar, mwanafunzi bora wa jumla katika mwaka wa masomo uliopita, Hongera Andendekisye kwa kumkamata huyo mdanganyaji wa mitihani.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  wewe huijui IFM vyema, hiki niuchuo ambacho huwezi kucheat ukakamatwa ukaachwa, huyo mtu anaetajwa kama Andendekisye Mark kwa sasa ni msajili wa chuo, aliwahi kumkamata mkewe katika sup,
  tofauti na vyuo vingine IFM ukikamatwa jamii nzima hutaarifiwa , na kwa hilo huwa somo kwa wengine wote.
  vyuo vingine hii hubaki kuwa siri ya ndani.
  Ukitaka kujua IFM NI NOMA NENDA PALE BOARD YA UHASIBU KAULIZE NI NANI ALIENGOZA MWAKA JANA KWENYE cpa, Huyu anaitwa Hansigar, mwanafunzi bora wa jumla katika mwaka wa masomo uliopita, Hongera Andendekisye kwa kumkamata huyo mdanganyaji wa mitihani.
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mfanyaji na mfanyiwaji wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.
   
 13. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kimsingi IFM pameoza kwa huu usanii haiwezekani kilasiku watu wanasoma kwa ujanja ujanja kumbe wanafanyiwa mitihani dah sasa watanzania tunakwenda wapi manake hizi ndizo dalili za kutaka kufaulu sana GPA kubwa kumbe msomi bogus
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kinachofurahisha zaidi ni pale mwanafunzi wa form 6 anapomfanyia mtihani mwanafunzi wa stashahada
   
 15. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  haya tunashukuru kwa yote
   
 16. Qulfayaqul

  Qulfayaqul JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 471
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kufanya generalization katika ishu kama hii ni uvivu na ufinyu wa kufikiri bwana nguvumali, si kweli kwamba ifm/cbe hakuna wanafunzi smart na walio na akili just be specific to those who cheated, usihukumu na wasio na makosa. Hivi ni vyuo vilivyo makini na vinaongozwa na watu makini na wengi wao wametoka katika vyuo bora na vyenye sifa kama udsm,mzumbe na hata nje ya nchi,

  kuwahukumu jamii yote kuwa ni mbovu ni makosa jaribu kufikiri mheshimiwa.
   
 17. MduduWashawasha

  MduduWashawasha JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 1,567
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  mambo ya shule ni kama dhehebu au kabila.mtu akisoma university of Nairobi basi watu wa vyuo vingine ni kama ngedele vile.kwa taarifa yenu cheating iko sehemu zote.mfumo wa elimu TZ umeoza kwa sasa.mimi huwa napitia mitihani ya siku hizi ya form four na six hamna kitu pepa mchekea na mijitu bado inafeli.anayebisha akatafute mitihani ya kidato cha sita ya kuanzia 1970 mpaka kwenye 1985.compare na ya sasa ndo utaona.hawa watu wanaingia vyou tofauti sio IFM pekee.tuache ushabiki na tuliangalie hili kama tatizo la mfumo mzima.sio kukandiana vyuo huo ni utoto.sasa ni mimi niliyesoma University of Natal na Monash University nitaviongeleaje vyuo vya hapa ?MFUMO JAMANI
   
 18. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mkuu maneno yako yakweli kulaumu chuo ni makosa tatizo lipo kwa wanafunzi wenyewe hawataki kusoma kizazi cha sasa ni lege lege sana watu wantaka vitu virahisirahisi tu wana kuwa ma risk takers kwakuwa hawana future plan,ila mi naomba serikali irudishe jkt tuondoe unyoro nyoro huu(chungulia pipa)
   
 19. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu mie nakubaliana na wewe kwani hata muhimbili kwa sasa kucheat kumeongezeka sana kiasi cha kutia wasiwasi tutakuwa na madaktari wa aina gani.Ila kuongezeka kwa wanafunzi ambako hakuambatani na kuongezeka kwa miundo mbinu kama madarasa na kadhalika kunachangia kwa kiasi kikubwa tatizo hili kuongezeka.Suala la kufanyiana mitihani ni tatizo karibia kila chuo.kuna haja ya wasimamizi kuongeza umakini na ukali pia.
   
 20. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tukumbuke pia Jumuiya ya afrika masharika hiyooo iko njiani.Tutauweza ushindani kwa staili hii.
   
Loading...