kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Mpaka wa namanga ulifungwa kwa tangazo la mtumishi kutoka wizara ya afya
Holili akafunga RC Kilimanjaro na Kuacha Rongai na Tarakea wazi.
Horohoro Tanga kafunga Rc Tanga
Sirari Mara bado hatujajua atafunga Nani.
Hii mipaka yote ni Kati ya Tanzania na Kenya, waliofunga kila mtu alitoa maelezo amefunga Nini na Nini kinaruhusiwa.
Wafungaji wa mipaka wote kinadharia au kwa ufahamu wao au kwa namna walivyotoa matangazo ni kana kwamba mipaka hii siyo ya nchi Bali Ni mipaka ya mkoa, mfano RC Tanga anaeleza katika taarifa yake kwamba asilimia 90 ya wakenya wanategemea bidhaa kutoka Tanzania.
Kwa aliyefika horohoro ataelewa RC alimaanisha mzunguko wa biashara mpakani unawategemea zaidi wakenya kuja kununua kwa 90% hivyo mchango wa manunuzi ya Watanzania mpakani hapo ni 10%. Means tumewaambia wafanyabiashara wa Tanzania wajiandae kufanya biashara na 10% ya wateja wao huku tukiwaambia 90% ya wateja watafute bidhaa kutoka nchini mwao.
Katika mkutadha huu, Ni ipi nafasi ya wizara na Mawaziri kwenye mipaka yetu? Mamlaka ya kufunga mpaka wa nchi kisheria ipo kwa Nani?
Wakulima waliovuna watauza wapi mazao yao Kama tumewadhibiti wanunuzi kwa 90%
Hatuoni kwamba tunawaambia wakenya kisaikolojia kutoitegemea Tanzania na kutafuta soko jipya?